Rais Abdel Fattah El-Sisi afafanua kwanini hawezi kuruhusu Wapalestina waingie Misri. Asema itakuwa ni ujinga na kuisaidia Israel katika malengo yake

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Katika mazungumzo yake na chansela wa Ujerumani muda mfupi uliopita, Raisi El Sisi wa Misri amesema hawezi kufanya maamuzi ya kijinga kuruhusu wapalestina kutoka Gaza waingie nchini humo kama wakimbizi.

Akasema hilo inaonekana kama ndio lengo la Israel ilipowataka warudi kusini mpakani na nchi yake na kwa kuwakatia maji.

Amesema kufanya hivyo ni kama kuruhusuj Israel ije kuifanyia Misri ugaidi huko mbeleni kwani wapalestina wataendelea kuidai nchi yao kutokea majangwa ya Sinai na kwengineko Misri.

Vile vile maamuzi hayo akiyafanya yatasababisha ghasia zaidi kutoka kwa wanachi wake watakaonza kuingia mabarabarani kumpinga.

Kwa upande mwengine waziri wa mambo ya nchi za nje wa Jordan ameonesha hasira kubwa kwa namna Israel inavyoendeleza mgogoro huo na kusema kinachotakiwa kwa sasa ni kusitisha vita mara moja na si mazungumzo.

Hayo ameyasema wakati raisi wa Marekani akianza safari za kujaribu kufanya mazujngumzo na nchi za Kiarabu.
 
Hii vita imetengenezwa kwa ufundi na ustadi Mkubwa sana kupenyeza agenda kuu za kudunia.

eneo pekee ambalo Vita vikilipuka Dunia nzima hupata mafua ni mashariki ya Kati.

Mashariki ya Congo watu wanateseka kinyama lakini ni kama vile watoto wanacheza kidali poo.
 
Pindi Israel iliposhambuliwa hatukuona shtuma au matamko kutoka kwa waarabu na waislamu kipindi Ukraine ilipovamiwa na urusi waukraine walikufa wengi wenu mlimuunga mkono urusi sasa Israel inaamua kujilinda yenye tunaona makelele kote duniani ndio mjue dunia imejaa unafiki na upendeleo.

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app
 
Jamani waswahili tujikite kwenye mambo yanayo tuhusu, mbona hatujawahi kua na nyuzi nyingi kukemea Uganda na Rwanda wanao semekana kuitesa Kongo ambao ni majirani zetu kabisa miaka nenda rudi🤔🤔 au kukemea vita vinavyo endelea kwenye nchi nyingi za kiafrika🤔🤔tuache unafki waswahili.
 
Hawa waarab hukaa kimya israel inaposhambuliwa ila huleta vidomo domo israel anapojibu
Mkuu bila shaka mzozo huu umeanza kuufuatilia baada ya Hamas kashambulia Israel wiki iliyopita.

Kimsingi jeshi la Israel limekuwa likivamia na kutwaa makazi ya Wapelestina kila siku. Ni vile mainstream media haziripoti tu.

Hakika wanaofuatilia vitendo vya jeshi la Israel kwa Wapelestina wanaelewa lengo la Hamas kufanya shambulio hilo.

Kwanini Netanyahu alikuwa anaisaidia serikali ya Ghaza kujiimarisha hadi shambulio hili ndio kawaona wabaya?
 
Mpaka leo jeshi la Kongo linapambana na RDF waliojivisha nguo za M23.

Watu wapo kimya kutwa kumsifia Ngongoti humu kwamba anakuza uchumi wa nchi yake lakini maumivu na gharama wanazoingia Wakongo zinafumbiwa macho.

Rwanda kaiga tabia mbaya ya utwaaji wa ardhi ya Wakongo kwa taifa ya Israel eti kisa jumuiya ya kimataifa anayatambua mataifa haya kama wahanga wa ethnic cleansing na genocide.

zitto junior Mtu Chake
 
Kaka watu wanaendeshwa na mihemko ya kidini na sio kingine. Kuna wanaosapoti Israels hao Christians kuna wanaosapoti palestina na hamas hao Muslims though watakuambia not all Palestinians are Muslims na jews are only 2% Christians ahhahh.
 
Hila zake zinajirudia rudia na watu wameshazielewa
Huyu Israeli karibu kitampata kilichompata kule Ujerumani, dunia karibu itawachoka na ukatili wao. Hata wale waliokua wakiwatetea kwa mtazamo wa kidini wameanza kuelewa Waisraeli ni wahuni tu hawana dini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…