Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Katika mazungumzo yake na chansela wa Ujerumani muda mfupi uliopita, Raisi El Sisi wa Misri amesema hawezi kufanya maamuzi ya kijinga kuruhusu wapalestina kutoka Gaza waingie nchini humo kama wakimbizi.
Akasema hilo inaonekana kama ndio lengo la Israel ilipowataka warudi kusini mpakani na nchi yake na kwa kuwakatia maji.
Amesema kufanya hivyo ni kama kuruhusuj Israel ije kuifanyia Misri ugaidi huko mbeleni kwani wapalestina wataendelea kuidai nchi yao kutokea majangwa ya Sinai na kwengineko Misri.
Vile vile maamuzi hayo akiyafanya yatasababisha ghasia zaidi kutoka kwa wanachi wake watakaonza kuingia mabarabarani kumpinga.
Kwa upande mwengine waziri wa mambo ya nchi za nje wa Jordan ameonesha hasira kubwa kwa namna Israel inavyoendeleza mgogoro huo na kusema kinachotakiwa kwa sasa ni kusitisha vita mara moja na si mazungumzo.
Hayo ameyasema wakati raisi wa Marekani akianza safari za kujaribu kufanya mazujngumzo na nchi za Kiarabu.