Rais akikosea aambiwe ukweli hadi aelewe

Nchi yetu inaribiwa na ushabiki wa kisiasa, Kwenye maswala muhimu kama haya hatuna umoja, Upinzani ukipinga hili vijana na wanachama wa chama tawala wataingia kati kulisapoti hata kama lina madhara
 
Kwahiyo fedha za kigeni sio mapato.....

Ni kama market cap flani hivi
 
Lakini kwani huwezi chimba Madini katika namna ya kudhibiti uharibifu wa mazingira na baadae mbuga kurejesha uoto?
Uchimbaji madini unaambatana na matumizi ya kemikali, makundi makubwa ya watu, ukataji miti ovyo, jambo hilo litaleta usumbufu mkubwa kwa viumbe wanaoishi hifadhini na wengi wataangamia.
Hifadhi zetu ziachwe na jukumu lake moja tu.
Mwambieni mama aachane na shuguli za kibinadamu hifadhini.
 
Ndio maana ya EIA ,kabla ya kufanya hivyo lazima hiyo kitunifanyike kuonesha namna ikolojia italindwa.

Kwani ni Tanzania pekee ndio wa kwanza kuchimba Madini hitadhini? Huko Amazon inafanyika hivyo na kwingine.

Sijaona hoja ya msingi yaani Kila kitu ni kupinga tuu.

Bwawa la Nyerere limefanyika hitadhini na hakuna kilichoharibika.
 
Huko nyuma baadhi ya watu walisema hiyo wizara kupewa Mavunde sio bure kuna kitu wanatengeneza.

Huyu mama ni predictable ukiona mtu anapewa majukumu ambayo kama vile makubwa kwake, basi ana mikakati yake huko.

Ghafla Kijaji nae mazingira wawekezaji wasisumbuliwe huko na process ndefu za environmental impact assessment.
 
We chawa, huwezi linganisha bwawa la umeme na mgodi wa madini...kimadhara, ni vitu viwili tofauti kabisa.
Jielimishe!.
 
Nasikia wamebadilisha pori sasa hivi wanakuepeleka makaburini moja kwa moja
 
Katiba, kumpa Raisi maamuzi makubwa kama nchi ni yake binafsi, ndiyo haya. Mimi naona kwa vyote alivyofanya. Na aina ya wananchi wa Tanzania, ambao wanaendekeza ushabiki wa kisiasa kwa tujipesa.

Ni bora tukae kimya tu, akimaliza kwenye mbuga, amalizie na sehemu ya misitu iliyobaki, akimaliza Rasilimali zote. Ahamie na makazi ya watu, abomoe nyumba zote awape wawekezaji. Watanzania si wanaona sasa hayawahusu. Naomba ifike huko, sijawahi ona watu aina ya watanzania. 🤬
 
We chawa, huwezi linganisha bwawa la umeme na mgodi wa madini...kimadhara, ni vitu viwili tofauti kabisa.
Jielimishe!.
Una uhakika? Kwamba Kuna mgodi ambao utawekezwa Kwa Trilioni 7 hapo Serengeti? Acha upuuzi.

Harafu kazi za uchenjuajinhiwa zinafanyika Nje ya Hifadhi sio ndani,vitu hamjui ila mnapayuka tuu.

Nimewauliza na Tzn tuu ndio Madini yanachombwa hifadhini?
 
Huyu akichimba madini Serengeti halafu dunia nzima ikasusa kuja Tanzania ndiyo atajua hajui.
 
labda hata hakumbuki na wala hajui kama alisema hivyo, mambo ya kuandikiwa hotuba kusoma tu kukamilisha ratiba, ndo maana namkubali D.Trump yeye anakwenda offscript hivyo anasema kile anachokiamini na kilicho moyoni mwake …
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…