Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Binafsi naamini kabisa Raisi yuko sahihi, wanyama hawali madini.
Mama yetu inabidi tuendelee kumwamini kama tulivyomwamini kwenye sakata la bandari, na tusikate tamaa kumtetea. Hizi fitna za kuzuia Madini yasichimbwe ni Propaganda za Kikatoliki kwasababu wananufaika na hizo mbuga, endapo tutaanza kuchimba madini ni lazima maslahi ya kanisa yataguswa.
Halafu makampuni ya UAE yakichimba madini hayawezi kuharibu mazingira. Kama Ortello Hunting wako miaka na miaka na hakuna uharibifu wowote ule, sembuse kuchimba madini ? Hawa ndugu zetu waarabu wana mitaji mikubwa na wana ustaarabu sana kwenye mazingira. Waliweza kuigeuza Dubai kutoka jangwa kuwa jiji la kitalii, sidhani kama wanaweza kuharibu mazingira.
Kama tulimwamini Raisi kwenye makubwa kama Bandari, basi na hili la mbuga tumwamini.
Mr Q
Watalii watakuja kuangalia mashimo yatakayoachwa baada ya uchimbaji wa madiniSasa ile Royal Tour ilikuwa ya nini.?
Umesahau cc MahondawNa akikosea aelekezwe lakini asisutwe...
Nimeshakusoma GT🤣Mkuu JokaKuu naona na wewe umeingia kwenye kundi la wahafidhina na wadini wa Tanganyika ambao wana lengo la kumkwamisha Raisi. Jambo moja ambalo inabidi uelewe ni kwamba Uraisi ni taasisi na Raisi amefanye Informed Decisions, hajakurupuka tu.
Wawekezaji ambao tunawaleta hapa ndiyo walewale tuliowaleta bandarini, waarabu wa UAE, ambao ni watu wema sana na wana maendeleo makubwa kuliko sisi. Dubai ilikuwa jangwa lakini wakaibadilisha kuwa jiji la kisasa kabisa, hivyo hawawezi kuanza kuchimba madini bila kufanya Environmental Impact Assesment (EIA) za kiwango cha juu.
Kuhusu wanyama, nao tutawahamisha tu kama tulivyowaamisha wamassai. Wengine watauzwa, maana hili tumeshaanza kulifanya kama ulivyoona juzi alivyokuja yule kiongozi wa Uarabuni. Hivyo ni lazima Tanzania iendelee kwa namna yoyote ile.
Kina Mzee Nyerere walikosa sana busara, kuanzisha hifadhi sehemu zenye madini na kuyafukia tu ilhali Tanzania inahitaji maendeleo. Hivyo nakuomba sana ndugu yangu, kama ambavyo tulimwamini Raisi kwenye jambo kubwa la Bandari na DP World, basi tumwamini kwenye hili dogo la madini.
Mama ni mtu Smart na Muungwana sana.
Labda anamaanisha mbuga za kwao huko Zanzibar.Tunakoelekea ni kubaya zaidi jamani. Viongozi waliotangulia wangekuwa wanapambana kuuza kila kitu yeye angekuta nini? Hizo hela wanazopokea baada ya mauzo zinafanya nini zaidi ya kuliwa na wajanja wachache?
Kwani ni lazima rasilimali zote ziuzwe in her regime? Yani napata ile feeling ya mzazi kutaka kuuza mali zake sababu amezeeka ili atumbue kabla hajafa bila kujali kizazi cha wajukuu zake kitakuja kuanza kuhangaika upya.
MbegelesiNimeshakusoma GT🤣
Mungu akubari!!..Serengeti ni mbuga maarufu kuliko zote hapa nchini, na katika ukanda wa Afrika.
..Pia Serengeti ndiyo mbuga inayotupatia mapato makubwa kuliko mbuga zote hapa Tanganyika.
..Serengeti ina historia na jina kubwa duniani. Kazi za kuitunza na kuitangaza Serengeti imefanyika kwa miaka mingi sana.
..Thamani na umuhimu wa Serengeti kwa Tanganyika, ni sawa na thamani ya Mapiramidi kwa wenzetu wa Misri.
..Serikali ya Misri ikichukua uamuzi wa kuchimba madini ktk maeneo yaliko Mapiramidi lazima wananchi wa Misri watahoji, na dunia itawashangaa viongozi wao.
..Ziko mbuga na hifadhi hapa Tanganyika serikali inaweza kuchimba madini, au hata kuzifuta, na wananchi wasishtuke. Lakini sio Serengeti, Ngorongoro, na Mlima Kilimanjaro.
..Serengeti ni URITHI wa vizazi vya Watanganyika. Ni "mboni" ya uhifadhi na utalii hapa Tanganyika. Kila Raisi anayeingia anapaswa kuitunza.
Tena utalii hauharibu mazingira. Pesa zinaigia kwa watalii kupepesa macho tu.Hizo za madini zote zimeingia serikalini?au za makampuni ya nje serikali imeambulia mrabaha na kodi?..utalii ukiingiza hela unaingiza zaidi kuliko madini
Taarifa inasema TANAPA wamekataa madini yasichimbwe. Sasa kama taasisi yenye wataalam na yenye wajibu wa kutunza hifadhi za taifa inaona jambo hilo sio sahihi na rais asiyejua a,b,c,d za uhifadhi anasema madini yachimbwe ni wazi kwamba rais anatakiwa apunguziwe mamlaka ya kujiamulia tu mambo anavyoona yeye.Hii waki iweka vizuri kuna pesa mingi
Nawa shauri serikali ukiachana na kodi zitakazo lipwa kama kampuni ya uchimbaji
Serikali inatakiwa iwatoze pia kama watalii maana watakuwa wana chimba huku wana angalia wanyama na hii haiwezi kuwa burebure
Kumbe ile 'Royal Tour' ulikuwa ni usanii, hakuna lolote alilo jifunza?Tunakoelekea ni kubaya zaidi jamani. Viongozi waliotangulia wangekuwa wanapambana kuuza kila kitu yeye angekuta nini? Hizo hela wanazopokea baada ya mauzo zinafanya nini zaidi ya kuliwa na wajanja wachache?
Kwani ni lazima rasilimali zote ziuzwe in her regime? Yani napata ile feeling ya mzazi kutaka kuuza mali zake sababu amezeeka ili atumbue kabla hajafa bila kujali kizazi cha wajukuu zake kitakuja kuanza kuhangaika upya.
You're actually" showing off" your own ignorance big time here!Don't show off you're schoolless behavior
Viongozi dhaifu, wasio maono kama huyu bibi ni mzigo kwa taifa.Juzi Rais Samia kasema madini yachimbwe kwenye mbuga, cha muhimu hela. Hii kauli si sahihi kabisa tena sio sahihi kutoka kwa Rais wa nchi.
Si tayari ameshaolewa?Wakati wa Magufuli niliwahi andika hapa kama Magufuli anao watu wa kumwambia ukweli na akawasikiliza, nilitoa mfano wa Fidel Castro alivyokuwa anaogopwa na watu wengi sana lakini walikuwepo watu wawili walikuwa wana uwezo wa kumwambia ukweli Raul Castro mdogo wake na Comrade Che Guevara. Hawa wawili walikuwa na uwezo wa kumwambia ukweli na makosa yake bila kupepesa macho na akawasikiliza.
Juzi Rais Samia kasema madini yachimbwe kwenye mbuga, cha muhimu hela. Hii kauli si sahihi kabisa tena sio sahihi kutoka kwa Rais wa nchi.
Rais alipaswa kwanza kupata elimu ya kutosha kuhusu uchimbaji wa madini na athari za mazingira, lakini la muhimu zaidi alipaswa kuniuliza kwanini Viongozi kabla yake wote walisita au kukataa kutoa vibali vya kuchimba Mbugani?
Je hata kama tukikubaliana na Rais cha muhimu hela, kwani Rais hajui utalii ndo unaingiza hela Tanzania kupita madini?
Rais hajui au hana ushauri wa kumwambia kuwa athari za kimazingira huko Mbugani zinaweza moja Kwa moja kuathiri utalii na kupunguza mapato kuliko hata kuongeza hayo mapato?
Rais hajui kuwa hayo makampuni ya madini huwa yanaahidi sana mambo mengi mazuri lakini mwisho hushindwa kutekeleza kuanzia Kodi hadi taratibu za kulinda hayo mazingira? Kampuni ya madini inaweza sababisha sumu kwenye vyanzo vya maji ya wanyama hadi binadamu, na hili sio nadharia imewahi tokea na ushahidi upo.
Madini yanaweza chimbwa yakaisha na mapato ya maana yasipatikane, imeshatokea..na haitakuwa la ajabu ikitokea tena.
Mbuga za Wanyama zilzopo Tanzania haipatikani tena kwingine duniani, ni urithi wa dunia. Mbuga kama Serengeti ina Wanyama Wengi kupitia Mbuga yeyote duniani, hii Peke yake ni dhahabu kuliko dhahabu yenyewe.
Mbuga kama Selous ukubwa wa Ardhi tu ni zaidi ya nchi ya Belgium, halafu leo tunaanza tena kuruhusu uharibifu wa mazingira Mbugani mradi ipatikane hela? tuharibu kuku anaetotoa mayai ya dhahabu ili tukatafute mayai mengine tumboni?
Rais akikosea aambiwe hadi aelewe.