Rais ambaye hajawahi kugombea, ilitokea Marekani, itatokea tena huku

Wakuu,

Mwaka 1973 Spiro Agnew alijiuzulu nafasi ya makamu wa Rais wa Marekani kufuatia skendo ya rushwa na matumizi mabaya ya ofisi ikiwemo kukwepa kodi alikofanya wakati ni governor wa Maryland. Rais Richard Nixon akamteua Gerald Ford kuchukua nafasi yake.

August ya mwaka 1974, Rais Richard Nixon alijiuzulu kufuatia skendo ya Watergate. Hapo ikabidi makamu wa Rais, bwana Gerald Ford aapishwe kuwa Rais wa Marekani.

Unaweza kuona jinsi Ford alivyokuwa na bahati. Hakuwahi kugombea umakamu wa Rais au Urais wenyewe lakini alishika vyeo vyote hivyo kwa nyakati tofauti zinazofuatana.

Nimeandika hii habari kuonyesha yanayokuja soon.

Endelea kusubiri!
Kwani ameshamfuata Mume wake au
 
Magu haukutiki bwana! Samia aligombea mbona.

Labda useme round hii kwa sababu Ndejembi hajawai kigombea. Likitokea la kutokea ndiyo Uzi utatimia
Wakati anaingia aligombea uraisi au mgombea mwenza kwa ajili ya umakamu?
 
Alichaguliwa na wana-nchi kama mgombea mwenza wa Magu kiufupi aliwekwa hapo Kwa kura za wana-nchi.

Tofouti na Ndejembi ambaye hajawai kabsa kigombea/kushiriki uchaguzi wa hiyo Nafasi aliyo nayo kwahiyo. Amepata bahati kuwepo, ikitokea la kutokea ndiyo Uzi huu utatiki
 
Wakuu,

Mwaka 1973 Spiro Agnew alijiuzulu nafasi ya makamu wa Rais wa Marekani kufuatia skendo ya rushwa na matumizi mabaya ya ofisi ikiwemo kukwepa kodi alikofanya wakati ni governor wa Maryland. Rais Richard Nixon akamteua Gerald Ford kuchukua nafasi yake.

August ya mwaka 1974, Rais Richard Nixon alijiuzulu kufuatia skendo ya Watergate. Hapo ikabidi makamu wa Rais, bwana Gerald Ford aapishwe kuwa Rais wa Marekani.

Unaweza kuona jinsi Ford alivyokuwa na bahati. Hakuwahi kugombea umakamu wa Rais au Urais wenyewe lakini alishika vyeo vyote hivyo kwa nyakati tofauti zinazofuatana.

Nimeandika hii habari kuonyesha yanayokuja soon.

Endelea kusubiri!
Na Mimi nasubiri
 
Mkuu Tumia akili, heshima kwako sana.
Nimerudi kuusoma huu uzi wako wa mwaka 2020 na kwa kweli nimebaki nanyosha mikono juu kwako. Huu uoni wako wa mbali unathibitisha namna jukwaa hili linavyohifadhi vichwa vyenye madini ya hatari sana. Uchambuzi wako wa miaka sita nyuma kuhusu historia ya Gerald Ford ulikuja kuwa ukweli mtupu na wa mchana kweupe hapa nyumbani pale mabadiliko ya ghafla yalipotokea mapema mwaka 2021. Hongera sana mkuu, ulikisia pabaya!
Lakini tukirudi kwenye weledi na kulinganisha mifumo yetu ya kikatiba, hili dokezo lako linaibua ukweli mmoja mchungu sana kuhusu tofauti yetu na wenzetu:
Kwanza kabisa, kama Tanzania ingekuwa inafuata misingi ya Katiba ya Marekani (ile sheria yao ya mabadiliko ya 22), huyo Mama asingekuwa hata na sifa za kisheria kugombea na kuwepo madarakani hivi sasa baada ya ule uchaguzi wetu wa Oktoba 2025. Kule Marekani mfumo wao uko makini mno; muda ule wa mpito aliokaa baada ya mzee kuondoka ungehesabiwa kama muhula mmoja kamili, jambo ambalo lingeweka ukomo wa yeye kuendelea. Katiba yetu ya sasa ndiyo iliyompa huo mwanya wa kisheria ambao wenzetu walishaziba miaka mingi iliyopita.
Pili, ukiangalia mfano ule ulioutoa wa Gerald Ford kwenye uchaguzi wa mwaka 1976 dhidi ya Jimmy Carter, unaona ukomavu mkubwa sana wa kiongozi na taasisi. Ford alishindwa uchaguzi kwa kura chache sana, lakini kwa sababu ya kuheshimu misingi ya kidemokrasia na katiba yao thabiti, alikubali matokeo kiungwana kabisa na kukabidhi nchi kwa amani bila kuleta zengwe lolote.
Sasa njoo ulinganishe na uhalisia wa kwetu kwenye huu uchaguzi mkuu uliopita wa Oktoba 2025. Tofauti na ukomavu ule wa Gerald Ford, hapa kwetu mambo yalikuwa ni kinyume kabisa. Kuona ushindi wa asilimia 97.66 uliopatikana baada ya mazingira magumu ya kuwafungia wapinzani wakuu kama CHADEMA, kuwakamata viongozi wao kabla hata ya kampeni kuanza, na lile zoezi la kuzima intaneti kote nchini siku ya kupiga kura, inadhihirisha wazi kuwa mfumo wetu ulilazimisha matokeo kwa nguvu kubwa ya dola badala ya sanduku huru la kura.
Kama kweli tungekuwa na Katiba imara na Tume huru ya Uchaguzi inayozuia hila hizi za kisheria na matumizi ya mabavu ya vyombo vya dola kulinda viti, ramani ya kisiasa ya Tanzania ya leo isingekuwa hivi ilivyo sasa. Wenzetu katiba zao zinalinda matakwa ya wananchi, lakini ya kwetu inatumika kama kichaka cha watawala kujihakikishia kubaki madarakani kwa gharama yoyote ile.
Uchambuzi wako wa tangu mwaka 2020 umesimama kama darasa zuri na rejea dhabiti sana ya kihistoria. Asante kwa kuendelea kufungua macho ya wadau humu jukwaani!
 
Marekebisho yatafanyika atakapoingia "Brother" Uzi wake wa mwisho uliandika mambo yatakayokua kipaumbele!

Na dalili za original plan zinaonekana coz makam aliegombea 2025 na mwenyekiti ameshajiuzulu kwa kashfa za maadili na sasa tunatarajia "Rais ambaye hajawahi kugombea urais"kuwa rais AmBAR ni Maka. Wa sasa au mwingine kama huyu akionekana mwenye dosari!

Kifupi maandiko yake yanaishi!!
 
Kwahy ule uzi wa "Brother",unamuhusu huyu VP wa sasa?
 
kifupi tu,Tumia akili anaweza kuwa ni mtu wa mfumo na aliyekuwa anafahamu mipango yote kuhusu Magufuli au alikuwa karibu na watu wa mfumo hivyo taarifa nyingine zilivuja kwake kuhusu mipango hiyo.
 
Wakuu,

Mwaka 1973 Spiro Agnew alijiuzulu nafasi ya makamu wa Rais wa Marekani kufuatia skendo ya rushwa na matumizi mabaya ya ofisi ikiwemo kukwepa kodi alikofanya wakati ni governor wa Maryland. Rais Richard Nixon akamteua Gerald Ford kuchukua nafasi yake.

August ya mwaka 1974, Rais Richard Nixon alijiuzulu kufuatia skendo ya Watergate. Hapo ikabidi makamu wa Rais, bwana Gerald Ford aapishwe kuwa Rais wa Marekani.

Unaweza kuona jinsi Ford alivyokuwa na bahati. Hakuwahi kugombea umakamu wa Rais au Urais wenyewe lakini alishika vyeo vyote hivyo kwa nyakati tofauti zinazofuatana.

Nimeandika hii habari kuonyesha yanayokuja soon.

Endelea kusubiri!
Fantasy
 
Back
Top Bottom