Rais anapata wapi mamlaka ya kuagiza Spika asilipe posho za Wabunge?

Rais anapata wapi mamlaka ya kuagiza Spika asilipe posho za Wabunge?

Kwahiyo wewe ulitaka walipwe posho wakiwa wamwelala nyumbani huku wengine wapo kazini.
Huendi kazini hulipwi.
Asiefanya kazi na asile.
Wakuu, ile dhana ya uwepo wa Mihimili Mitatu inayojitegemea ni DANGANYA TOTO TU. Magufuli amedhihirisha hilo leo kwa kuagiza Ndugai asilipe posho za Wabunge walioamua kujiweka "karantini".

Kama Rais ana mamlaka ya kuliingilia Bunge, vipi kuhusu Mahakama? Atashindwaje kutoa maagizo yanayofanana na hayo kwenye Tume yake ya Uchaguzi hapo Oktoba?

My take: Tuna utawala wa Mkono wa Chuma, tusitarajie Uchaguzi Huru hapo Oktoba mwaka huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuliwaasa Chadema

Wabunge wa Chadema wakichaguliwa na Watanzania wakawawakilishe bungeni

Ila Mbowe kwa ubabe wake bila kushirikiana na Spika amewakataza wabunge wa Chadema wasihudhurie vikao

Kwanza ieleweke Mbowe huwakata wabunge wake zaidi ya milion kwenye mshahara wa mbunge

Leo anawakataza wasichukue hata posho ?

Mbowe ajitathimini akae pembeni akili imefika kikomo
HAONDOKI...., huyu ndo anawakosesha usingizi,Hatuweki mchumia tumbo ili mu mnunue.
 
Magu yupo juu ya Katiba.
Magu hayuko juu ya sheria, Bali anajifanyisha tu kuwa juu ya sheria.......

Hebu tujiulize si yeye mwenyewe ambaye aliapa kuwa ataitii na kuiitumikia Katiba ya nchi, iweje Leo atake "kuisigina sigina" Katiba halafu aachiwe hivi hivi tu??
 
Kuna mtu anaitwa Katibu wa Bunge, huyu ni mteule wa Rais, ndio Mlipaji Hapo DODOMA. Kupokea maelekezo ya Mwajiri wake Sio hoja
Nguvu ya kuteua sio nguvu ya kuamrisha. Rais anateua majaji, kwani wanapokea maelekezo kutoka kwake?
 
Bunge kama halijielewi lazima litapokwa madaraka yake !!
 
Binge wanapata wapi pesa zao za kuendesha shughuli za bunge??!!! At least mahakama ina vyanzo vya mapato. Bunge linategemea serikali kuu kwa almost kila kitu. Wao wanatumia tu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuna Jaji mstaafu Marekani aliulizwa, jambo gani anaona ni hatari zaidi kwa usalama wa USA. Akajibu, wananchi kukosa elimu ya uraia.

Sio kosa lako, jifunze kwanza theory ya separation of powers ndio utaelewa kwamba bunge kutokusanya mapato sio uzembe, na serikali kupeleka pesa bungeni sio hisani
 
Spika Bosi wake ni Mkuu wa CCM, ambaye ni Raisi wa JMTZ, na fedha yote ya Serikali ya JMTZ msimamizi wake ni Raisi wa JMTZ, Bunge linapewa fedha za walipa kodi wa JMTZ na msimamizi wa Kodi zetu ni Raisi wa JMTZ, ...

Thank you for the explanation! Sometimes I feel this platform has kids under 18, anyways I can see the end of the platform soon, if the moderators are not taking note of all the nonsense here.
 
Ingependeza kama speaker wa bunge amjibu rais kama alivyofanya speaker wa Uganda juzi kwa rais Museven ili kuonesha nguvu ya bunge kama mhimili unaojitegemea na wenye maamuzi yake so rais auheshimu.
Spika yupi,huyu mtaalamu wa kukagua "vinyeo" vya kuku???
 
Speaker wa bunge anaamrishwa Kama mtoto, wakati anajua kabisa bunge ni muhimili unaojitegemea, Hv pesa na uhai kipi muhimu? Yani Yuko radhi wabunge wake wage kwa kushinikizwa na kamtu kamoja,Mbowe anaakili Sana,Sasa hapo mtoto ni nani? Kati ya wabunge wa chadema na ndugai anaamrishwa na rahis,Akili za kuambiwa changanya na zako

Sent using Jamii Forums mobile app
Bunge linajitegemea katika maeneo gani mkuu?!
 
Ukisoma hii thread utaona tuna safari ndefu sana. Somo la separation of powers ni gumu sana. Kama "the enlightened" wa JF hawaelewi sijui ndugu zangu huko vijijini.

"Democracy cannot survive too much ignorance" - Justice David Souter
 
Wakuu, ile dhana ya uwepo wa Mihimili Mitatu inayojitegemea ni DANGANYA TOTO TU. Magufuli amedhihirisha hilo leo kwa kuagiza Ndugai asilipe posho za Wabunge walioamua kujiweka "karantini".

Kama Rais ana mamlaka ya kuliingilia Bunge, vipi kuhusu Mahakama? Atashindwaje kutoa maagizo yanayofanana na hayo kwenye Tume yake ya Uchaguzi hapo Oktoba?

My take: Tuna utawala wa Mkono wa Chuma, tusitarajie Uchaguzi Huru hapo Oktoba mwaka huu.
Too much politics. Bungeni hutaki kwenda halafu unataka wapate posho.
 
Ivi swala la posho navyojua ni pale mbunge anapohudhuria kikao na kusaini kama yupo bungeni.

Magufuli alikuwa mbunge na waziri kwa miaka zaidi ya 20 inamaana hajui mbunge asipohudhuria kikao halipwi posho? (Sitting allowance).

Ivi yeye huwa anaingiliwa kama anavyoingilia mihimili mingine? Ivi bunge au mahakama ilishawai kumwamlisha rais kutekeleza jambo lolote?

Kuna swali kuwa bunge ni rubber stamp ya rais kuna anayebisha?
 
Back
Top Bottom