Rais anapata wapi mamlaka ya kuagiza Spika asilipe posho za Wabunge?

Rais anapata wapi mamlaka ya kuagiza Spika asilipe posho za Wabunge?

Kuna kitu watu mbumbumbu hawakielewi

Yan Rais, spika na Waziri, mkuu wa mkoa na wilaya mtaji wao n chama Cha siasa na chama Cha siasa kinaongozwa na mwenyekiti Taifa Hadi Kaz ya chini ya mjumbe wa shina.

Sasa hao wote wanamabosi wao kwenye vyama vyasiasa Yan mwenyekiti wa chama mkoa husika anapotoka Spika au waziri fulan na anaweza kumkanya au kumfuta uanachama na ukifutwa uanachama automatically unakosa sababu ya kuwa waziri au Spika au Rais ndomana Vyama vya siasa wanajitahid kumpa mtu potential kwa chama ndan ya muda sahihi nafasi kubwa Kama mwenyekiti ili kuzuia Mambo ya conflict ndan ya chama na Dola.

MFano mbowe hawez kuwa mwenyekiti wa mkoa wa Kilimanjaro tuu bila kuwa mwenyekiti Taifa sababu anajua akiwa hvyo n rahisi mwenyekiti wake kumfuta uanachama kwa sababu ambazo wataona zifaa.

Haya Mambo ya siasa yanavitu vingi mno Ila ubaya wengi humu waposiasa darasa la nne Yan ndo kwanza wanaotegemea kufanya national exam mwaka huu wakati siasa yenyewe ilishagrauate ma PhD Kama ya the late Robert Mugabe.

Ndo wengi humu wanahoji mstari bila kuhoji Mana nzima ya kitabu
 
Kuna mtu anaitwa Katibu wa Bunge, huyu ni mteule wa Rais, ndio Mlipaji Hapo DODOMA. Kupokea maelekezo ya Mwajiri wake Sio hoja
Katibu wa Bunge kuteuliwa na Rais ni mfumo tu (Procedure) lakini hawezi kufanya mambo (Kama anajielewa) Kinyume cha Kanuni za Bunge, Hata hivyo haijawahi kutokea wabunge kulipwa posho bila ya kuwepo Bungeni!!??
 
Kwanza tumia akili ya kawaida tu kutafakari ni kwa jinsi gani Posho huwa zinalipwa. Hivi unaweza kulipwa posho bila ya kuwepo kwenye eneo litakalosababisha ulipwe posho? Tunaweza kuthibitisha pasipo shaka kwamba tangu wabunge wa CHADEMA waache kwenda bungeni kwamba walikuwa wanalipwa posho?

Bunge halitoi "Justifications" yoyote ili lipewe hela bali huwa linakaguliwa na CAG. Ndio maana CHADEMA ilitaka kuwe na mfuko maalum wa Bunge na Mahakama lakini CCM wanakataa kwa hoja kwamba mifuko ya Bunge na Mahakama duniani huwa inawekwa kwa kigezo cha asilimia ya Bajeti ya Taifa.

CCM wanadai ukiwepo mfuko wa Mahakama na Bunge itakuwaje kama bajeti ya nchi ikiwa ndogo? Sasa utaona mna dhana potofu kwamba bunge "linaomba" kupewa pesa na ni serikali ina hiyari ya kukataa ama kukubali kulipa Bunge fedha za kujiendeshea. Hii ni DHANA POTOFU KABISA!!
Kitu mnachokosea ni kila hoja kuwekwa UCCM na UCHADEMA. Angalia sheria, kanuni na taratibu za Tanzania zinasemaje kuhusu posho, na si CCM wanasema nini.
 
Angalia sheria, kanuni na taratibu za Tanzania zinasemaje kuhusu posho, na si CCM wanasema nini.
Swali langu ni rahisi tu, kwamba kabla ya Rais kutoa tamko la kuzuia Posho kuna Mbunge yeyote wa CHADEMA ambaye aliwahi kulipwa Posho wakati hahudhurii vikao au kushiriki kazi za kibunge??
 
Swali langu ni rahisi tu, kwamba kabla ya Rais kutoa tamko la kuzuia Posho kuna Mbunge yeyote wa CHADEMA ambaye aliwahi kulipwa Posho wakati hahudhurii vikao au kushiriki kazi za kibunge??
Nilishakujibu kwamba muulize Katibu wa Bunge.
 
Wakuu, ile dhana ya uwepo wa Mihimili Mitatu inayojitegemea ni DANGANYA TOTO TU. Magufuli amedhihirisha hilo leo kwa kuagiza Ndugai asilipe posho za Wabunge walioamua kujiweka "karantini".

Kama Rais ana mamlaka ya kuliingilia Bunge, vipi kuhusu Mahakama? Atashindwaje kutoa maagizo yanayofanana na hayo kwenye Tume yake ya Uchaguzi hapo Oktoba?

My take: Tuna utawala wa Mkono wa Chuma, tusitarajie Uchaguzi Huru hapo Oktoba mwaka huu.
Jbu unalo mwenyewe kwa kanuni usipoudhuria kika posho hupewi hamna kosa hapo.Piga kazi baba
 
Nilishakujibu kwamba muulize Katibu wa Bunge.
Hapa kwani tunajadili mambo ya Katibu wa Bunge ama Kauli ya Rais!! Kama ni mpaka Katibu wa Bunge aulizwe ni kwa nini mnashangilia kama vile wabunge wa CHADEMA walikuwa wanalipwa posho na sasa hizo posho zitazuiwa??
 
Hapa kwani tunajadili mambo ya Katibu wa Bunge ama Kauli ya Rais!! Kama ni mpaka Katibu wa Bunge aulizwe ni kwa nini mnashangilia kama vile wabunge wa CHADEMA walikuwa wanalipwa posho na sasa hizo posho zitazuiwa??
Wewe unataka uthibitisho wa wabunge kulipwa ili uone kama kauli ya rais ipo sahihi au hapana na ndio maana muulize katibu wa bunge.
 
We acha kujidanganya

Rais is on top kwa kila kitu

Kwani bunge wanatoa wapi hela? Wanauza maandazi?

Mwenye hela na jeshi ndio kila kitu

Wewe sema tu mhimili mitatu

Kaishi USA
Siku hizi amjadili hoja iliyopo mezani bali mnajadili hisia za mkuu; hoja ni serikali au rais anaweza kusema kua kuanzia leo Bunge lisilipwe posho? au Rais anaweza kusema kuanzia leo nataka nilipwe mshahara wa Bilioni 200 kwa mwezi?
Mmebaki tu kusema Bunge linakusanya kodi..au wakati katiba inaandaliwa hawakujua kua Bunge halikusanyi kodi? Naona Rais amepanda juu ya wananchi adi akapanda juu ya wawakilishi wa walipa kodi na kodi zao, ila mwambieni huyo jamaa anapotoka akiwa na stress zake.
 
Kuna siku atasema jaji usipomhukumu mtuhumiwa flani upewi mshahara; ni ujinga kuchekelea kauli zinazovunja taratibu tulizojiwekea kama nchi na mtu mmoja ambae ni mpita njia tu tena wa miaka mitano.
 
Wewe unataka uthibitisho wa wabunge kulipwa ili uone kama kauli ya rais ipo sahihi au hapana na ndio maana muulize katibu wa bunge.
Hoja yangu ni kwamba posho huwa hailipwi kwa wabunge ambao hawapo Bungeni na si jambo jipya, kusema wasilipwe ni sawa na kusema kuwa Jogoo ni kuku dume!!
 
Chadema nao warudi bungeni wapitishe bajeti ya wananchi , sidhani kama kuna mwananchi yuko tayari *kodi* yake ikalipe watu waliojitoa kazini kwa hiari yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Speaker wa bunge anaamrishwa Kama mtoto, wakati anajua kabisa bunge ni muhimili unaojitegemea, Hv pesa na uhai kipi muhimu? Yani Yuko radhi wabunge wake wage kwa kushinikizwa na kamtu kamoja,Mbowe anaakili Sana,Sasa hapo mtoto ni nani? Kati ya wabunge wa chadema na ndugai anaamrishwa na rahis,Akili za kuambiwa changanya na zako

Sent using Jamii Forums mobile app
Speaker na Bunge lake wanajipendekeza kwa rais.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom