Rais anayetawala kwa kutegemea alivyoamka ni hatari sana kwa Taifa

Rais anayetawala kwa kutegemea alivyoamka ni hatari sana kwa Taifa

Magu is the right presidaa at the right time! kila afanyacho mi namkubali asilimia 200 nisichopenda kwake ni kimoja tu ni kuumizwa wapinzani, kwanini anaruhusu hayo? kwanini hajiamini? si awaache tu wale mbu wapige kelele tu zisizochana chandarua? tume ya uchaguzi iko mfukoni presha yanini? au mbu wana kelele kubwa hata hapati usingizi? namsihi sana baba yetu aachane na siasa hizi za majitaka awe bora kuliko hata Mwalimu!!

miradi ya miaka yake kumi tu inapita miradi yote ya miaka yote ya marais wote wengine, kila mtanzania hata mtoto mdogo anajua yeye ni rais bora na wa mfano duniani sasa kwanini kina DJ waviziwe na kuvunjwa miguu for what motive? isijekuwa yule mzee kijana Slow times two anampotosha! sisi wa kijani wenzake tulioko kijiweni na msoto tumechoka kusikia matukio ya kihalifu kuumiza wapinzani nao ni jamaa zetu tuko nao kitaa!tumezoea nchi yetu ni ya amani kwanini inageuzwa Burundi?

Tangu aingie madarakani vyovyote anavyoamka ni bora tu kwa taifa ameanzisha utamaduni mpya wa viongozi kuweka wazi mambo na kuacha kufunika uozo mfano akimtumbua mlevi anatangaza hili lilevi tumelitoa hakika Magu ni chuma cha pua!!
 
Back
Top Bottom