Rais asibughudhiwe pindi amalizapo wakati wake, aachwe apumzike

Rais asibughudhiwe pindi amalizapo wakati wake, aachwe apumzike

mtimawachi

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
2,108
Reaction score
3,155
Habari wanajamvi!

Nazungumzia Rais kushitakiwa amalizapo muda wake (kama alifanya makosa akiwa madarakani).

Asili ya sisi Waafrika (watu weusi) ni kupenda kukomoana, majungu na visasi.

Inawezekana kabisa ukiwa madarakani ukafanya/ukasimamia jambo kwa mujibu wa taratibu lakini kwa kufanya hivyo ukagusa/ ukaharibu maslahi au mipango ya wengine.

AU unaweza kujistarehesha na hawara wa mtu bila kujua siku wakishika madaraka wao basi kwisha habari yako.

Sheria hii inafaa kwa jamii zilizostaarabika na kuelimika,sio kama huku kwetu ambako WASOMI NDIO WAJINGA WAKUU.

Nasisitiza Rais asibughudhiwe pindi amalizapo wakati wake, aachwe apumzike.

Mimi mwandishi itikadi yangu sio tu ni CCM, bali ni timu MAGUFULI
 
"Mimi mwandishi itikadi yangu sio tu ni CCM, bali ni timu MAGUFULI"

UMekuja kutetea legacy hapa. Japo mwanzo ulianza vizuri.
 
Hakika watu wagaelewa zaidi sentensi ya mwisho kuliko hata mantiki yako.

Hata mimi timu Mafuguli. Namngoja siku ya ufufuo tufufuke wote.
 
"Mimi mwandishi itikadi yangu sio tu ni CCM, bali ni timu MAGUFULI"

UMekuja kutetea legacy hapa. Japo mwanzo ulianza vizuri.
Hapana mkuu, kama wewe ni mtumishi au umewahi kuwa kiongozi utaelewa maudhui ya uzi
 
Hakika watu wagaelewa zaidi sentensi ya mwisho kuliko hata mantiki yako.

Hata mimi timu Mafuguli. Namngoja siku ya ufufuo tufufuke wote.
Hakika mkuu,nimeshaanza kuona viashiria
 
Mawazo ya wenye njaa kali ni shida sana, yaani kabisa mtu anaandika utumbo kama huu, Rais yeye sio Malaika stupid! Hawa ndio waleee ambao ndio mtaji wa mbogamboga.
 
Mawazo ya wenye njaa kali ni shida sana , yaani kabisa mtu anaandika utumbo kama huu, Rais yeye sio Malaika stupid! hawa ndio waleee ambao ndio mtaji wa mboga mboga

Mkuu umewahi kuwa kiongozi?
 
Mkuu umewahi kuwa kiongozi?
Thinking kama hii haihitaji usomi wa Phd kujua kwamba ni ya chini sana, kama huyo D.A.B amewatuma mmefeli tena sana, nchi haijawahi kuwa na kionmgozi wa hovyo kama huyo Daudi
 
thinking kama hii haihitaji usomi wa Phd kujua kwamba ni ya chini sana , kama huyo D.A.B amewatuma mmefeli tena sana , nchi haijawahi kuwa na kionmgozi wa hovyo kama huyo daudi
Amefanya jambo gani baya zaidi?
 
Si mwenyewe waona magufuli tumeacha kumbughuziii kama unavyosema rais asibughuziwe.

Ngoja aongoze malaika
 
KWA TAARIFA YAKO WANAOTUBUGUDHI WATANZANIA NI HAO MARAISI WASTAAFU. HAWARIDHIKI NA WAMEKUWA CHAWA NA WAPIGA DILI WAKUBWA. UNAONA VITOTO VYAO. MI NAONA NJIA BORA YA KUWAPUMZISHA NI KUWAOMBEA VIFO VYA MAPEMA KWANI HAWATOSHEKI.
 
Duh!
Mkuu sheria ya kuwashtaki maraisi ni nzuri ila si kwa jamii kama zetu za kishamba(samahani kwa kuziita hivyo) ambazo zinajikita kwenye kukomoana,

Swali la kizushi: Kati ya hawa walobakia unamwombea nani atangulie mapema?
 
Si sheria zipo kwamba rais asishtakiwe hata akisha toka madarakani? au mnataaka sheria gani nyingine?
Hivi nana anambughudhi Rais Mwinyi?
 
Back
Top Bottom