Rais Assad aripotiwa kuikimbia Syria, Majeshi ya Waasi yatangaza kuuchukua mji mkuu wa Damascus

Kwa Syria ni ngumu kuna makundi ya waasi ya jamii mbalimbali duniani, wachina, waturkey, warusi, wasaudi yaani magaidi yooote ya kundi la ISIS waliokuwa magerezani duniani waliachiwa wakapelekwa Syria, kilochowashangaza wamagharibi Moscow na Tehran kuruhusu nchi Assad aiachie pasipo mapigano na mauwaji ya kutisha, swali Syria itaelekea wapi na itaweza kudhibitiwa vipi iweze kutawalika, kumbuka wanajeshi wengi wa Syria wamerudi uraiani na wengine wamekimbilia nchi jirani na silaha zao mkononi kusikilizia game linaendeleaje!!!😀
 
Utawala wa kupokezana kifamilia umekwisha!
Harafu inaonekana tayari kulikuwa na Uasi ndani ya Jeshi la Syria.
Haiwezekani mapigano yachukue takribani wiki mbili tu harafu wanajeshi wakimbie!
 
Golani alikamatwa na wao Marekani wakamfunga jela miaka 6 na walipomtoa wakampa masharti kwamba aunde kundi (tawi la Al qaeda nchini Syria) la kumshughulikia Assad ndo akaunda Al- Nusra Front.

Na huyu kafanya kazi na Abu Bakri la Baghdad ambae alikuwa ni mkuu wa ISIS nchini Iraq.

Baadae Baghdad akasema ajiengua Al-qaeda na kuingia Syria ambapo alitaka kuimeza Al Nusra Front lakini Golani akakataa wazo hilo na Baghdad aka... mwaka 2019.

Kwa handlers Golani ndie alieonekana afaa kuliko Baghdad as simple as that.

Hivyo leo Golani akipewa heshima zote wala haishangazi.
 
Wanajeshi wa Assad wajinga tu bora ata na hamas walitoa upinzan
 
Bado kiduku ni swala muda tu
 
Monarch ipo kikatiba sio ya kujitungia. Kwa mfano Swaziland ni monarch kikatiba. Ila Syria sio Monarch kikatiba. Ni kama Tanzania Leo, atoke Nyerere urais halafu Makongoro awe Rais mpaka Leo huwezi kusema hiyo ni Monarch.
Hayo yote yanawezekana ukiwa puppert na western mkuu, huwa hawaangalii katiba ya nchi yako ukilinda maslahi yao, Hivi unaweza kuniambia kati ya Iran na Saudi Arabia nchi ipi ni katili sana kwa raia zake!?
 

Usikimbilie kupeleka lawama magharibi huu ndo udhaifu wenu,Asad alichokwa na raia wa Syria hakuna mmagharibi aliyemwaga damu hapo ktl mapinduzi haya Bali ni raia wa Syria kwa mustakabali wa taifa lao
 
Ndugu zangu wasuni na washia tuache kupigania

Mtume wetu akitusia adui yetu Ni mayahud na makafiri

Tuwaangamize Hawa ili mola wetu akatuzawadie katika zile bikra tamu alizotuahidia 😋
Mayahudi wana mkono kwenye haya machafuko. Labda Syria nayo inakwenda kuwa kama Lybia ilivyo sasa.
 
AMEENDA WAPI RAFIKI YAKE KIPENZI RUSSIA......AMEENDA WAPI RAFIKI YAKE KIPENZI IRAN....
Kama wanajeshi wako wameshindwa kutetea nchi Urusi na Iran wangesaidia vipi kumtetea!? Jifunze ukraine wanavyokufa wananchi wao itafika mahali ukraine wanaume itakuwa bidhaa adimu, wanajeshi wa Syria ndio wameuza nchi yao kwa ISIS....
 
Rusia si mshirika wa kuaminika
Kwa aina ya wanajeshi wa Syria walivyo kuwa wanapigana hata ungekuwa ww ungetema bungo.

Urusi, Iran na Hizbullah wametumia mabilion ya$ wamemwaga damu za wanajeshi wao wakakusaidia kukomboa ardhi kubwa alafu leo hii unakuja kuipoteza kizembe kabisa,hakuna wa kuvumilia hili aisee.

Hata Marekani alisha wahi kuikimbia na kuiteketeza serikali ya Afghanistan ikangukia mikononi mwa Talbani,pia walisha ikimbia serikali ya Vietnam kaskazini mwisho ikatekwa na wakomonisti, sasa hivi wanataka kuikimbia Ukraine kwa mgongo wa ya Trump.
 
Hii habari kama haijathibitishwa na FaizaFoxy au THE BIG SHOW au Webabu au Ritz au Koshugi sitaiamini hata kama imetolewa na Al Jazeera! Ahahahahaha!!!
 
Haya makundi yanayokuwa yameorodheshwa kama ya kigaidi mbona yana nguvu sana!!

Ina maana majeshi ya nchi husika huwa yako wapi kiasi nchi kuanguka!!

Nilianza kushangaa wakati Taliban anachukua nchi ndani ya mda mfupi!

Ina maana majeshi unakuta na wenyewe wamechoka na tawala zao ama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…