cassavaleaves
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 1,799
- 2,237
Mwisho wake umefika, hana jinsi yoyote ya kumbakisha madarakani.
Ila hii oparesheni ya waasi imenishangaza sana, ndani ya muda mfupi wamechukua nchi!
Imekushangaza kwa vipi? Hukuziona dalili za wazi dadangu! Waliyokuwa wakiibeba, ni Iran, Urusi na Hezbollah! Wote hao yamewazidi, Hezbollah ilibidi iondoe wanajeshi wake irudi nyumbani kupambana na Israel, hii ilikuwa pigo kubwa! Iran ina mengi mno....Ipigane na Israel, isaidie Hezbollah, na Hezbollah imewaangusha pakubwa! Urusi inabidi iongeze nguvu Ukraine.....Hukuona haya yote Nifah?