Rais avunja rasmi tume ya Warioba

Rais avunja rasmi tume ya Warioba

Nguvu ya Hoja

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2012
Posts
276
Reaction score
125
Rais Jakaya Kikwete amevunja rasmi tume ya kukusanya maoni ya katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph warioba. Hii ni kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 81 la Machi 21 mwaka huu.

====

TANGAZO LA SERIKALI KUHUSU KUVUNJWA KWA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

Mhe. Rais aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katika kwa mujibu wa kifungu cha 5 na 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 kwa Tangazo la Serikali Na.110 la Mwaka 2012.

Tume ilikusanya maoni na kuandaa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imewasilishwa kwenye Bunge Maalum.

Kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 3, Rais amepewa mamlaka ya kuvunja Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa Bungeni.

Mnamo tarehe 18 Machi, 2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba aliwasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum. Kutokana na hatua hiyo, na kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano alivunja rasmi Tume ya Mabadiliko ya Katiba tarehe 19 Machi,2014 kwa Tangazo la Serikali Na.81 la tarehe 21 Machi, 2014.

Hivyo kwa Tangazo hilo, shughuli zote za Tume ya Mabadiliko ya Katiba zimemalizika rasmi tarehe 19 Machi, 2014.

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
Dar es Salaam.

25 Machi,2014
 

Attachments

Kwa tangazo hilo Warioba tayari kazibwa mdomo maana ataongea kama nani sasa?
Hii si sawa nadhani kuna jambo zaidi tusubiri.
 
Kwa tangazo hilo Warioba tayari kazibwa mdomo maana ataongea kama nani sasa?
Hii si sawa nadhani kuna jambo zaidi tusubiri.

Kama Raia wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,ama kama Waziri mkuu msitaafu au kama Jaji mstaafu n.k
 
Hapa ndo naona wakati muafaka wa jaji kufunguka kama Raia wa kawaida na kama Waziri mkuu mstaafu,na kama Jaji.......!!!

Duh sheria bwana zina mambo! Kwa hiyo Waryoba hana tena uenyekiti!!
 
Yale magari hawajaweka mnadani wauziane wao kwa milion 2
 
Hana 7bu za kujichosha kazi alisha maliza kawakabidhi wabunge zaidi ya 600. Ss huyo alietoa semina elekeki nae nijukumu lake. Nahata hivyo hilo bunge ni rubber stump tu. Mbn mengi yana fanywa kwanza baadae linakuja bungeni kwa mipasho na hitimisho ni NDIOOOO
 
Rais Jakaya Kikwete amevunja rasmi tume ya kukusanya maoni ya katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph warioba. Hii ni kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 81 la Machi 21 mwaka huu.

Source: Ikulu.

Hongereni sana Tume, mnaweza kwenda kupumzika sasa, achieni mamlaka nyingine zifanye kazi yake!
 
Hongereni Tume ya katiba... kazi yenu haitoenda bure... Tanganyika is back now or then...mtaingia kwenye historia na vizazi vitawakumbuka kama mashujaa thabiti wa kupigania hoja na mataka ya wananchi.. kauli ya Tume ni kauli ya wananchi na ni kauli ya Mungu...
 
Data zipi alitoa mtaani?

tehe tehe tehe tehe

maoni ya wananchi 17,000 ni haramu na hayapaswi kuwasilisha mawazo ya watanzania milioni 45

halafu nasikia jamaa alisoma uchumi hivyo anajua nini maana ya random sampling.

hah hah hah hah Kweli mtu mwenye vidonda vya tumbo Tanzania amejitakia tu, yani pamoja na comedy zote hizi bado mtanzania anapata stress zinazopelekea vidonda vya tumbo!!!!
 
Back
Top Bottom