Pre GE2025 Rais aweka jiwe la msingi ujenzi wa daraja la Mto Pangani la Bilioni 107, Urefu wa Mita 525

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Rais Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Daraja la Mto Pangani na Barabara ya Bagamoyo (Makurunge), Saadani, na Tanga Pangani.

Ujenzi wa Daraja la Mto Pangani utagharimu shilingi bilioni 107 hadi kukamliika kwake, na litakuwa na urefu wa mita 525.

Soma: Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Rais Samia yupo mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi ambapo anazindua miradi mbalimbali na kuzungumza na wananchi.

Your browser is not able to display this video.


Your browser is not able to display this video.
 
Funguni kumekucha hapa....mh.Waziri Awesso yuko jukwaani muda huu....
 
Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mha. Mohamed Besta akizungumza na viongozi mbalimbali katika sherehe ya Uwekeji wa Jiwe la Msingi katika barabara ya Mkange - Pangani - Tanga ( km 170 .8) pamoja na Daraja la Mto Pangani (m 525).l wilayani Pangani tarehe 26 Februari, 2025.
 
Iyeeena iyeeena.... Iyeeena iyeeena, iyeeena.... Iyeeena, Mama Samia nambari waniii!
 
Njia fupi kabisa kulifikia bwawa la Nyerere na Hifadhi ya Nyerere ni kupitia Kisarawe lakini karibu miaka 30 barabara hiyo ujenzi wake haujafika hata kilometa 30 kutoka Pugu Kajiungeni ambapo kuna mpaka wa Ilala na Kisarawe.
Huu ni ubaguzi wa waziwazi kwa watu Kisarawe kwa sababu hakuna barabara nyingine yoyote yenye lami wilaya nzima zaidi ya hiyo.
 
Daraja la Magufuri busisi kilometer 3 ujenzi wake ni bilion 99 halafu hili daraja la pangan urefu wake Miter 500 gharama yake bilion 107

Endeleen kutupiga

Kwahiyo daraja lenye thamani ya bilioni 20 kwa wastani, awamu hii wanajenga kwa bilioni 100
Acha tupigwe tu. Maana kenge aelewi hadi atoke damu
 
Hotel ya nyota Tano,Magufuli aliweka jiwe la msingi!
Hadi Leo hakuna mkandarasi site
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…