Rais Biden ashauriwa kutogombea uraisi wa Marekani, sababu analiaibisha na kulivua nguo taifa lake

Ya chini ya carpet inasemekana kuwa sasa hivi nchi inaendeshwa na Blinken, japo Joe ameendelea kuwepo pale kama raisi kimvuli.
 
Kama ni kweli kuwa anafanya hivyo kwa sababu za kisiasa basi atakuwa hajui kuwa anajiaibisha sana yey na nchi yake mpaka muda mungine unaona mkewe akihisi aibu machoni.

Mbona miaka ile ya obama hakuwa hivi au pale uzee na ugonjwa alionao sasa ulikuwa haujazidi?
 
 
Trump huwa anamtania sana Biden huwa nacheka kweli[emoji3]

Ila kiukweli naungana na wewe Biden apumzike kwa usalama wa afya yake I wish Blinken aingie mzigoni kwenye kuufukuzia Urais binafsi nafikiri anafaa kabisa kuwa Rais wa U.S
Kuna video Moja anamuigizia anayotoka jukwaaani then anazulula bila kujua anakwenda

Kisha anawaambia watu kwenye mkutano
"Yeye mwenyewe BIDEN akitoka jukwaaani ajui aelekee wapi anabaki kung'aang'aa macho ajielewi kama zombie(huku akimuigilizia anavyokosa direction akitembea kama zombie mikono akiwa ameiweka dizaini mazombie yanavyotembea sura kaibenjua)
Sasa unadhani mtu kama huyu anaweza kujua analipeleka wapi taifa letu"

Basi watu na waandishi wa habari wanacheka
Huwa nacheka kishenzi trump amiwa anamuigizia biden
 
Kadiri umri wake unavyoenda ndivyo hali hiyo inazidi pia, kujumlisha tatizo lake la kigugumizi.

Ila mbali na hilo, Joe Biden ni kati ya watu wenye akili sana na anajua kucheza na saikolojia ya watu, hususan kwa vile vyombo vya habari asilimia kubwa ya ripoti zao ni hasi dhidi yake.

Kuhusu kujiharibia taswira ya taifa, sidhani kama hicho kinaweza kuwa suala zito kwa sababu kwa mujibu wa tathmini ya afya yake, yuko imara kutekeleza majukumu yake.

Fuatilia intavyuu yake anayozungumzia tatizo lake la kigugumizi na jinsi alivyosaidiwa kitaalamu na daktari wake hadi akamudu kwa kiasi kikubwa.

Bottom line, Joe Biden ni msanii sana. Akili nyingi ndizo zinakuwaga hivyo. Laiti angeupata mapema urais alioutafuta muda mrefu sana, huenda angekuwa maarufu mno.

Baada ya kusema hayo, Wamarekani wajitahidi kumrudisha Trump madarakani mwaka huu ili dunia itulie kidogo kwenye amani ila ichangamke katika utendaji na uwajibikaji.
 
Us inaongozwa "Deep state" kule hata maiti inaweza kuongoza nchi ili mradi hiyo maiti iweze kusoma na kuongea kilichoandikwa na hiyo deep state...Iko siku USA itakuja kuongozwa AI technology na binadamu tusiligundue hilo, tatizo muda tu..
 
Nchi ambayo ina-well intergrated systems haihitaji kiongoz mkuu kufanya maamuzi! Kwasababu kila kitu kinajulikana kitaende hv au vile.
 
Biden amekuwa kama robot linaloongozwa na remote kufanya majukumu yake. Ni aibu kwa taifa lenye watu makini kama Marekani kuendelea kuongozwa na yeye.
 
Mficha maradhi kifo humuumbua. Mtaendelea kusema kuwa Biden anaingiza ili ajipatie umaarufu kumbe mzee wa watu ndo anajiishia hivyo kimya kimya.
Ki ukweli kwa nchi kama Marekani haiitajiki raisi kuishi kama robot ili kujipatia umaarufu wa kisiasa. Nina imani kuwa Biden ni mgonjwa ila media za upande wake zinajaribu kuficha ukweli huu ili kulilindia heshima taifa isionekane kuwa wameruhusu robot litawale nchi.

Ongea yake, tembea yake na matendo yake vyote kwa pamoja vinaonesha clear kuwa yule mzee ana matatizo makubwa yanayofichwa fichwa na mamlaka yake.
 
Daah kweli we maandazi! Unachukua Habari kutoka magazeti ya propaganda unaleta huku, hiyo picture hapo ilikuwa ni video na wameikata ili aonekane naongea mwenyewe ila alikuwa naongea na huyo komamdo aliyeshuka na parachute. Na huyo si mke wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…