Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Leo naandika tena kwa uchungu mkubwa nikiikumbuka Serikali yetu sikivu ambayo inajitahidi wakati huu wa kampeni kupita kila mahali kuomba kura kuwa ikumbuke dhulma iliyofanyika katika eneo la Chasimba inasikitisha mno.
Eneo la Chasimba linaulikana historia yake ambapo lipo chini ya Kiwanda cha Cement cha Wazo hill Dar es Salaam. Eneo hili licha ya kunyamaziwa na watu kuachiwa kuamua kinyemela na leo wanapitiwa miundombinu ya maji na umeme ni jambo linaloonesha uzorotaji mkubwa wa haki.
Ninaandika nikiwa na kumbukumbu nzito za machungu waliyoyapata Wazazi wangu baada ya kudhulumiwa eneo na watu waliovamia na kisha kuachiwa kuendelea na uamuzi huo kama kwamba ndiyo utaratibu.
Ninakumbuka nilivyokimbizwa na mawe nakulazimishwa kuhamisha mifugo ya Mzazi wangu kwenye eneo hilo na wavamizi mchana kana kwamba eneo hilo halikuwa halali kwa Wazazi hao ila ni halali kwa waliovamia.
Kesi juu ya kufuatilia haki ya umiliki wa eneo hilo zimeendeshwa sana nina na nina uhakika ofisi za ardhi Kinondoni zina kumbukumbu nzuri juu ya hili lakini mpaka leo hii ni mwaka wa 15+ hakuna dalili ya haki.
Niliwahi kuandika kwenye ukuta wa Facebook wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshiwa Paul Makonda juu ya hili na leo ninaandika tena ninaamini kabisa kuwa wewe ni mpendwa haki na hivyo ninkuomba uwatendee Wazazi hawa haki yao kama inavyowastahili.