Rais Dkt. Magufuli tuko katika Majonzi makubwa, lakini Kocha wa Yanga ametutukana Watanzania wote. Akamatwe upesi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Hii haivumiliki na GENTAMYCINE nasema tena kuwa hii haivumiliki na namuomba Waziri wa Michezo aamuru Jeshi la Polisi nchini Tanzania chini yake IGP upesi sana wamsake (wamtafute) popote pale alipo Kocha wa Yanga SC Raia Ubelgiji Luc Eymael kwa ‘ Matamshi ‘ ya Kuidhalilisha Tanzania na hadi Sisi Watanzania.

Muda si mrefu Kituo cha Redio cha Wasafi FM katika Kipindi chao ‘ Maarufu ‘ cha Michezo Kiitwacho ‘ Sports Court ‘ kimetoka Kucheza ‘ Sauti ‘ ya Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga SC ambayo kiukweli aliyoyasema huko ‘ hayavumiliki ‘ na naenda kuweka hapa baadhi ya ‘ Kashfa ‘ zake Kwetu Watanzani
  1. Tanzania ni nchi ya Kipuuzi sana
  2. Viongozi wa Tanzania ni Wahuni
  3. Mashabiki wa Yanga SC hawajui Mpira ni kama Nyani au Sokwe (a.k.a mpya ya Yanga SC sasa ni Sokwe Nyani SC badala ya Utopolo SC )
  4. Shirikisho la Mpira nchini Tanzania lina Watu Wajinga mno na Wanaipendelea mno Simba SC
  5. Watanzania wengi ni Watu ambao hawana Elimu na wapo wapo tu
  6. Uongozi wa Yanga SC ni wa Watu Wapumbavu na Waongo nitashangaa Klabu ikipata Maendeleo chini yao
  7. Viwanja vingi vya Soka vya Tanzania ni vya Kufugia Mbwa na hata huu mnaousifia nao ni Mbovu tu
Na kutokana na ‘ Maadili ‘ kuna maneno yake mengine ya ‘ Matusi ‘ makubwa makubwa Kocha huyu ‘ Katutukana ‘ Sisi Watanzania. Japo ‘ Hasira ‘ zake nyingi zilikuwa ni kwa ‘ Mashabiki ‘ wa Yanga SC na Uongozi wake lakini pia ‘ ametutukana ‘ sana Watanzania na Rais wetu JPM nae ni Mtanzania vile vile.

Kwa wale ambao mtapenda Kusikia ‘ Kashfa ‘ hizi nzito za Kocha wa Yanga SC Mbelgiji Luc Eymael kwa Watanzania na Klabu ya Yanga SC Kesho Saa 2 na Nusu hadi Saa 5 Kamili asubuhi tegea Sikio Wasafi FM hasa katika Kipindi chao cha Michezo cha ‘ Sports Arena ‘ ambapo wameahidi Kuirudia hiyo ‘ Sauti ‘ huku wakisema kuwa Kesho ni Siku ya Kocha wa Yanga SC Luc Eymael.

Kwa ‘ Udhalilishaji ‘ aliousema Kocha wa Yanga SC Luc Eymael nitashangaa kama kuanzia Usiku huu hadi Kesho kama ‘ hajakamatwa ‘ na Mamlaka husika. Na kwa msiojua hii ni mara ya Pili Kocha huyu ‘ Mpumbavu ‘ anaichokonoa Tanzania kwani alipokuja alishawahi ‘ Kuhitilafiana ‘ na Shirikisho la Soka nchini na ‘ Kutishia ‘ kuwaambia Wazungu huko Ulaya kuwa wasije Kutalii nchini Tanzania.

Kwa wale mliopo katika Makundi ya WhatsApp ya Wanahabari za Michezo nadhani hivi sasa mnaisikia hiyo ' Clip ' ya huyu Kocha. Ni balaa tupu
 
Kama ni kweli kaporomosha hayo matusi, awahishwe korokoroni kwa usalama wake

Mkuu yaani unaambiwa hata hao Wasafi FM kuna maneno imebidi ' Waediti ' Kimaadili lakini ' tumetukaniwa ' hadi Mama zetu na Viungo vyao pia.
 
Tungekuwa na elimu,tungekuwa na akili unadhani ccm ingetutawala for 60 good years? Hata hivyo viwanja vya kufugia mbwa ccm walijimilikisha na still wameshindwa kuvitunza?

Kwa ujumla if I can summary yote aliyosema ni kuwa.Watu wenye akili hawawezi kutawaliwa na CCM,watu wenye akili hawawezi wakaambiwa na mwanasiasa tena akiwa amejifungia kijijini kwake kuwa Covid_19 imeisha wanakubali kirahisi, kumuamini na Kisha kujiachia Kama wanavyofanya watanzania.
 

Sasa kama ID yako tu inasema ' Sijijui ' unadhani Sisi wenye Akili zetu timamu kabisa na zinazofanya Kazi tutaweza Kukujua Mpuuzi kama Wewe?
 
Yanga ya mwaka huu ni majanga matupu kuanzia kocha, wachezaji na viongozi wote nidhamu sifuri sijui wamewezaje kushika namba mbili

Kwani hata pamoja na Kushika hiyo Nafasi ya Pili ' anafaidika ' na nini labda? Ukimuangalia tu Kocha wao utagundua alitoroka Mirembe ya Kwao.
 
Ingawa kuna mengine aliyosema ni kweli hasa kuhusu Yanga lakini amevuka mipaka sana,naona kibarua chake kikiota nyasi,labda alishaona Yanga inamwacha akaona aporomoshe matusi aondoke zake
 
Hajatutendea haki watanzania, tuna mlipa mshahara, tumempa work permit bado anatukana nchi pamaja na raia wake kutuita nyani, seriously!

Kuna sehemu kasema Uongozi wa Yanga SC haujampa Gari, Nyumba, haijamuwekea Dstv na inamtesa Mkewe na pia Maisha Duni ya Yanga SC.
 
Naomba serikali inipe kibali indirect way...nikusanye wahuni na mafuta yetu ya mgando ya babycare tunaweka rundo la mafuta kwenye sikio alafu uone majibu mpaka keshokutwa Kama atarudia ujinga wake...na huu uhuni kafundishwa na Morrison...alikua kijana mzuri tu huyu alipokuja bongo
 
We kweli hujijui
 
Ingawa kuna mengine aliyosema ni kweli hasa kuhusu Yanga lakini amevuka mipaka sana,naona kibarua chake kikiota nyasi,labda alishaona Yanga inamwacha akaona aporomoshe matusi aondoke zake

Na mwisho wa hiyo ' Clip ' nadhani akijua kabisa kuwa ' ametudhalilisha ' Watanzania na hatutomwacha akasema huwa hajali anataka Kuondoka.
 
Mkuu Wewe unayelazimisha uwepo wa corona unahisa na huu ugonjwa? Kama ulikuwa umetuletea mabarakoa na masanitizer uwauzie watu na baadae korona imesepa jua umeula wachuya

Mbona ulazimishe uwepo wa kitu wakati wewe sio mtaalamu wa fani hiyo,rais pamoja na wataalamu wa afya wamekili kuwa korona haipo,wewe mtu wa mitandaoni unalazimisha kuwa ipo.

Kama ndivyo hama nchi uende ambako hawana korona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…