Rais Dkt. Mwinyi amteua Maalim Seif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Rais Dkt. Mwinyi amteua Maalim Seif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Uko sahihi kabisa boss, sasa fanya hivi, hebu anzisha chama chako tuje tuone utendaji bora. Au ni mambo ya motivational speaker?
Mimi siyo mwanasiasa na wala sina interest na majukumu ya kisiasa, ila ninajua kuona ukweli. Wakati wa mgogoro baina ya Zitto na Chadema, katibu mkuu alikuwa Slaa, na nadhani unajua jinsi alivyoshughulikia mgogoro ule.
 
Wanasiasa wana mahitaji yao.

Na sisi wananchi tuna mahitaji yetu.

Ila sasa sisi wananchi tumewatelekeza wanasiasa, wameamua kufanya yao.

Maana sisi pia tuko busy kufanya yetu, ukiachana kubwabwajaaaa tu hakuna jipya tunafanya.

Lissu nusra auawe, Mdude yuko Jela, Mawazo hatunaye, Mange anaogopa kuja.

Sisi tuko busy kula bata na kuwapa pesa na kuwapigania celebrities kwenye mishow ya Wasanii wasio na mchango wowote wa mageuzi.

Wabongo akili zetu tunazijua wenyewe, tunapenda kupewa vitu vizuri tukiwa tumekaa na kustarehe yaani.

Anyway,

Nadhani sasa ni kuisoma namba kikamilifu ili kila mtu sasa atoke ndani,lugha iwe moja!
Mkuu ukiona hivyo basi jua wananchi wanaoana fresh tu kwao mambo swafi. Siku wakichoka hawatahitaji hata kuambiwa wataingia wenyewe barabarani kulianzisha. Kwasasa kama wanakula bata basi jua muda bado. Wakati na majira
 
Haya ni wakati wakuamka...gutuka hapo ulipo uwahi kazini, vinginevyo ukisalia hapa utakatwa mshahara
 
Jambo moja hua tunasahau ni kua wananchi tuna maslahi yetu na wanasiasa wanamasilahi yao.Huku nje tunaweza chaniana mashati lakini wao wanakunywa mvinyo pamoja.Sudan Kusini wamepigana weeee mwisho Machar ameenda kunywa mvinyo kir.

Mwisho wa siku kunakitu hua kinaitwa 'AGENDA'hii hufichwa na wanasisa wote kwa wananchi.Pale tunapoachana wengine wanakunania hapo hapo. 🙂 🙂 🙂 🙂 🙂
Munjombe umemaliza kila kitu😁😁😁😁
Ndio maana wakati watu wanatoleana tambo kwenye kampeni wengine tuliomba kuanzia October 28 tuendelee kukutana hapa kupeana pole na kupongezana

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais John Pombe Magufuli
 
Nafikiri kuna kitu ACT wazalendo wamefikiri. Ni vigumu kupambana na adui ukiwa nje ya mfumo kwani hata wanamapinduzi walikuwa ndani ya mfumo, ebu tumwacha Maalim Seifu, tutamuelewa baadae.
 
Pongezi kwa CCM kwa ukomavu wa kisiasa, hongera ACT kwa kukubali kwamba maendeleo hayana chama.

Tuliwaasa sana ndugu zetu kwamba hakuna upinzani Tanzania ila kuna wachumia tumbo na vibaraka wakatukatalia, ila nadhani sasa wataelewa.

Mungu ibariki Tanzania
Mama D, hatimaye hao mmewanasa, ccm mna sumaku KWA wapenda mabadiliko wanatakiwa kujiadhali Sana hata KWA kuwasogeleni, mnasumaku sio ya dunia hii Yani mtu anashutuka yuko kwenye kumi nane zenu, bila kujitambua,
Sema ncha za sumaku yenu zinakinzana na za CHADEMA kila mkilenga zinakwepana, na hamtaipata yenye ncha sawa na ya kwao maana Wana upgrade kila siku,
 
Wanasiasa nimewavulia kofia leo! Siku nyingine mkipigana siamulii. Nitakamata jembe na kuelekea shambani. Ningefanya hili wakati wa kampeni, leo hii labda ningekuwa navuna.

Wanasiasa wanajua kutongoza.. Watakutongoza utakubali tu tena
 
Mimi siyo mwanasiasa na wala sina interest na majukumu ya kisiasa, ila ninajua kuona ukweli. Wakati wa mgogoro baina ya Zitto na Chadema, katibu mkuu alikuwa Slaa, na nadhani unajua jinsi alivyoshughulikia mgogoro ule.
Ni kweli ww sio mwanasiasa wala huna interest na majukumu ya siasa, lakini utakuta ulikuwa au ni muajiriwa ambaye toka umeingia mpaka umetoka haujawahi kuleta mabadiliko yoyote ya maana kwenye taasisi uliyopo.

Huyo Slaa alishughulikia vipi suala la Zito, au unataka kuleta sifa za marehemu? Usidhani mgogoro wa Zito na cdm ni ww miaka 200 iliyopita, hivyo hatuna kumbukumbu. Kama ni taarifa tulikuwa tunazipata, na bado Zito alimlaumu Dr. Slaa kuwa anamkandamiza kwa maagizo ya Mbowe. Ingekuwa Zito hakuondoka hiki kilemba cha ukoka kwa Dr. Slaa kungekuwa na maana.
 
Haya sasa Maalim umeshaingia madarakani kawatoe wale masheikh wa Uamsho!!
 
Mie kama mzanzibari naungana na ACT na uongozi wake kushiriki serekalini. Nadhani kama ukiniuliza mimi nachukulia kususa ni sawa na suicide, hata 2015 uchaguzi uliorejewa wakati ule CUF wangeshiriki tuu uchaguzi huo wa Jecha na kushiriki SUK.

Nadhani wengi wanafahamu athari za upinzani kutoshiriki au kuwemo ndani ya muhula wa pili wa Shein, ambayo ndio hayo maafa na arubaini. Zanzibar hatuhitaji siasa za kuandamana wala kupigana wala kuuwana kwa sasa. Tunahitaji kutafakari kwa kina kipi muhimu, harakati za kuandamana au kuelekeza nguvu katika umoja wa kitaifa.

Nadhani umoja wa wazanzibari ni muhimu zaidi, kuingia ndani ya serekali kutaweka mazingira ya utulivu na kusonga mbele.

Maasalaam
 
Nafikiri kuna kitu ACT wazalendo wamefikiri. Ni vigumu kupambana na adui ukiwa nje ya mfumo kwani hata wanamapinduzi walikuwa ndani ya mfumo, ebu tumwacha Maalim Seifu, tutamuelewa baadae.

Alikuwepo kwenye serikali ya kitaifa na Dr. Shein, mbona uchaguzi wa 2015 matokeo yalipinduliwa kimachomacho?
 
Mie kama mzanzibari naungana na ACT na uongozi wake kushiriki serekalini. Nadhani kama ukiniuliza mimi nachukulia kususa ni sawa na suicide, hata 2015 uchaguzi uliorejewa wakati ule CUF wangeshiriki tuu uchaguzi huo wa Jecha na kushiriki SUK....

Mtu akiangalia anaweza kudhani una point za maana kwakuwa umeandika kwa busara. 2010-2015 mlikuwa kwenye serikali ya umoja wa kitaifa, mbona hiyo haikufanya matokeo ya uchaguzi yaheshimiwe? Au huo umoja wa kitaifa ni sharti ccm ndio wawe madarakani bila kujali ridhaa ya wengi?

Zanzibar hamuhitaji siasa za kuuwana wala kuandamana, lakini wakati wa uchaguzi lazima muuwawe ili ccm wakae madarakani! Sasa sijui ni kuuana kupi unakuoongelea.
 
Ndiyo muwe na akili sikuzingine mkiambiwa mkaandamane msikubali unafikiri waliopoteza maisha akati wa kura walipofanya maandamano si kama vile wamejinyonga tu wenyewe ona sasa watu wanaenda kula kuku kwa mrija wakigongeana glass na mwinyi wewe umekaa nyumbani unauguza mguu uliokatwa kwa uzembe wako kuweni na akili japo za kuvukia barabara
 
Back
Top Bottom