Rais Faye wa Senegal aanza visingizio baada ya kushindwa kutimiza ahadi alizotoa baada ya kuapa kuwa Rais. Awashutumu wapinzani kumkwamisha Bungeni

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Miezi 6 baada ya Rais wa Senegal Basirou Diomaye wa Senegal na Waziri wake Mkuu Ousmane Sonko wameanza kuleta visingizio Kwa Kushindwa Kutimiza Baadhi ya ahadi zao walizodai watazitatua ndani ya siku 100.

Serikali ya bwana Faye inasingia Bunge Kumkwamisha ambalo lina Wabunge wengi wa Upinzani(zamani chama Tawala).👇👇

My Take: Naendelea kuwakumbusha watu kwamba ni mjinga tuu ndio ataamini kwamba Wapinzani ndio watawatatulia shida zao.

Nawaambiaga mara nyingi kwamba Wanasiasa wote ni matapeli na siasa ni kazi kama kazi zingine so unapotumia Rasilimali zako hadi.kuandamana kulala risasi uwe unapima kama unachopigania utanufaika

Kwa taarifa yenu tuu Wapinzani hata Hawa wa hapa Tanzania Wana maneno meengi yasiyo na msingi na Wala hawana njia za kutatua Changamoto zenu sana sana wanachotafuta ni madaraka tu.

Imetokea Ghana, Malawi, Kenya, Senegal,Zambia na nk, and won't be different Kwa Tanzania.

Kumbuka ukiitiwa fursa jua wewe ndio fursa. SSH Anatosha na chenji inabaki.

==========

Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, anaonekana kupata ugumu kutumiza baadhi ya ahadi zake wakati wa Kampeni, miezi sita baada ya kuchaguliwa kuongoza taifa hilo la Afrika magharibi.

Serikali ya Faye ikiongozwa na waziri wake mkuu, Ousamne Sonko imeendelea kutuhumu bunge la taifa kwa kuwa kizingiti kwa sera za serikali yao, kwani idadi kubwa ya wabunge ni wa upinzani, Sonko akikataa kuwasilisha sera za serikali bungeni kwa misingi kwamba bunge hilo halitambui cheo chake.

Rais Faye amekuwa mstari wa mbele kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na mataifa washirika, akiwa mpatanishi kati ya muungano wa Ecowas na matifa ya Mali, Niger na Burkina Faso ambayo yalitangaza kuijiondoa katika muungano huo.

Hata hivyo wakosowaji wake wanadai ni hiyo mbinu ya kuepuka majukumu yake nyumbani katika hilo ambalo linashuhudia uhaba wa juu wa ukosefu wa ajira kwa vijana na deni la taifa.

Serikali ya Faye pia inatuhumiwa kwa kukosa kuizngatia usawa wa kijinsia katika teuzi mbalimbali za serikali.

Raia wengi wa Senegal aidha wanadai taifa lao halijasonga mbele tangu kufanyika kwa uchaguzi, wakati huu waziri mkuu Osmane Sonko akidai huenda bunge likavunjwa na rais Faye ili kutoa nafasi ya uchaguzi mpya wa wabunge.

Pia soma Rais wa Senegal avunja Bunge kwa madai ya Kuvutana na Mhimili wa Serikali

Soma zaidi hapa Ushauri: Rais Mteule wa Senegal BD Faye Asikubali kuwa Kivuli na Kuendeshwa na Sonko.Kuna Watu Lazima Waishie Kuwa Ngazi
 
Kale kajamaa nilijua tu katachemka. You can'tmake a tigerbout of a cat.
Give him time.
Kuna vyama viko madarakani miaka 63 Sasa wanafunzi bado wanakaa kwenye vumbi chini, mradi mdogo tu wa mwendokasi umeeashinda kuendesha. Sehemu kubwa ya Dar haina maji ya bomba. Ndani ya miezi 6 Senegal Wana mabasi ya mwendokasi ya umeme.
Ni kawaida MTU mfupi anaona Raha Sana kuona MTU mfupi kuliko yeye.
Huwezi kumpima kiongozi kwa miezi sita jamani, give him time.
 
Hoping for the best.
 
Hapa Tanzania ccm tumewapa nchi miaka 60+ hakuna cha maana walichokifanya, kila kitu ni hovyo hovyo. Acha tujaribu watu wengine. Hata mke ukioa akakushinda utaoa mwingine, hoja kwamba huyo mwingine atakua wa hovyo kuliko wa sasa haina mashiko, ni hoja ya mke wa sasa kutaka aendelee kuwepo hivyo atatafta kila maneno ya vitisho kukutishia usiongeze mke mwingine.

SSH unaemsema ndio worst case kabisa. Huyu ndio yuko tayari hata auze nchi ili mradi awe rais, hana mipango yoyote na hakua na maandalizi yoyote, hajui afanye nini na nini asifanye, yeye ni kama anapokea maelekezo kutoka kwa watu wengine. Hajawahi kukaa atuambie anatamani nchi ielekee wapi, yeye kila kitu ni mkalitazame na hilo, kina nani wakalitazame?

Samia anachukua mikopo isiyo na kichwa wala miguu huko wb ama imf lakini hatuoni hiyo mikopo inafanya nini, unakopaje kulipa mishahara na matumizi ya serikali. Katika sehemu Tanzania tuliruka mkojo na kukanyaga mavi ni kwa ssh.
 
Profesa

Profesa asad alisema Tanzania unamuona mtu kiongozi lakin yupo pale hajui afanye nn manake tunachagua viongozi wako shallow sasa kiongozi anachukua kipaza sauti anaanza sema dereva wake alikua akitapeli sie inaruhusu nn
 
kuongoza nchi hakuhitaj majaribio hii alishasema mwl j.k. kelele kelele ooh miaka 63 hamjapata maji .wakipewa wao
 
Yaani wewe unaingia kuongoza nchi za kiafrika halafu unataka kuleta mambo ya democrasia na vyama vya upinzani, nchi wahisani na wawekezaji unategemea utafika mahali? Yaani ukitaka kuiongoza Afrika ipate maendeleo itabidi utumie mkono wa chuma yaani wewe ujali nchi na watu, wake na maendeleo na usiwe tayari kusikiliza ngonjera zozote zile cha zaidi uwe tayari kuacha legacy no matter what can happen to you, ujitoe sadaka kwa ajili ya watu kama alivyofanya masiha Jesus christ.

Afrika ingepata wazalendo naamini miaka 20 tungekuwa na reli za SGR zinazoliunga bara zima na tungeimarisha usalama na kuwa na free trade na tungeishi kama tupo paradise ila ndio hivyo tena athari za watawala wa kikoloni bado zinatutafuna kuamini we can do nothing without whites, ndo maana dada zetu wanateseka na kudhalilishwa huko ulaya na uarabuni hii ni liana kwa watawala wetu waliopewa mamlaka ya kusimamia rasilimali zetu kwa niana yetu kisha wao wanazitumia vibaya kwa manufaa yao na wale waliowatesa mababu zetu. Naamini wazee wetu huko walipo huwa wanalia sana kuona sisi kwa sisi tunatesana kwa ajili ya kuwafurahisi watesi wao.
 
Wazalendo ndio watu gani? Hao wazalendo pesa wangezitoa wapi? Taja mfano wa hao Wazalendo waliofaulu Afrika.
 
Miezi minne(4) tu madarakani umeshamfanyia tathimini na kujua ameshindwa ila CCM ina miaka zaidi ya 60 madarakani na huambiliki kuihusu, mahaba kama yote! Ama kweli mtu mweusi bado ana safari ndefu ya civilization.
Mimi ndio nalalamika au yeye? Tathmini Huwa ni siku 100 na huyo kakaa miezi 6
 
kuongoza nchi hakuhitaj majaribio hii alishasema mwl j.k. kelele kelele ooh miaka 63 hamjapata maji .wakipewa wao
Ndio maana nawaonya Watanzania wasije kupoteza mda na makelele ya Wapinzani wakidhani Wana pepo wakati ni matapeli tuu wanatafuta madaraka.
 
Profesa

Profesa asad alisema Tanzania unamuona mtu kiongozi lakin yupo pale hajui afanye nn manake tunachagua viongozi wako shallow sasa kiongozi anachukua kipaza sauti anaanza sema dereva wake alikua akitapeli sie inaruhusu nn
Tuna watu wengi wanadhani kuongea sana ndio kuwa Kiongozi kuanzia Upinzani na huko Serikalini.
 
Hayo malalamiko wanatoa kina nani?

Wa senegal wenyewe bado wana imani naye kubwa sana.

Bunge linamkwamisha bado wana hasira. Ila mwezi Dec si mbali atavunja bunge. Maana kwa sasa hawezi kuvunja mpaka bunge litimize miaka miwili tangu wachaguliwe.
 
Back
Top Bottom