2019
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 3,130
- 4,735
Baada ya vyama vingi 1995 mpaka 2005 Mkapa alipondwa sana,ooh katili, fisadi n.k akatoka. Watu wakasema bora Mwinyi tu mzee wa ruksa.
2005-2015 Kikwete kasi mpya nguvu mpya ari mpya, rais kijana,mcheshi lakini alikumbatia wezi, majambazi mafisadi tuhuma zote ziliibukia kwake. Akatoka akapondwa sana mpole mno,mwizi sana.
2015-2021 Magufuli akasifiwa mwanzoni baadae akaanza kuonekana katili,mkali dikteta mkabila n.k. watu wakaanza kukumbuka mazuri na upole wa JK na wengine wakafikia hatua ya kusema bora Kikwete agombee tena.
Mungu si Athumani 2021- ... Samia
Anapondwa sana,ooh nchi inaongozwa na madalali sijui Kikwete ndio anaongoza sio mama. Je kwenye utawala wa Magufuli hamkumkumbuka JK? Kwanini sasa mnamkumbuka Magufuli baada ya Samia kushika usukani?
Je, ni rais gani alikubalika na watanzania wote akiwa madarakani? Leo Samia mtamwona ni bure lakini umuhimu utaonekana siku akitoka madarakani.
Vumilieni tu.