Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Mtanzania huwa hana shukrani hata siku moja. Alimtukana Mwinyi wakati ndiye muanzilishi wa mageuzi aliikuta hii nchi imejaa watu wanaovaa vidabwada wakila ugali wa yanga, na bado wakamuona hafai kwa lolote.Baada ya vyama vingi 1995 mpaka 2005 Mkapa alipondwa sana,ooh katili, fisadi n.k akatoka. Watu wakasema bora Mwinyi tu mzee wa ruksa.
2005-2015 Kikwete kasi mpya nguvu mpya ari mpya, rais kijana,mcheshi lakini alikumbatia wezi, majambazi mafisadi tuhuma zote ziliibukia kwake. Akatoka akapondwa sana mpole mno,mwizi sana.
2015-2021 Magufuli akasifiwa mwanzoni baadae akaanza kuonekana katili,mkali dikteta mkabila n.k. watu wakaanza kukumbuka mazuri na upole wa JK na wengine wakafikia hatua ya kusema bora Kikwete agombee tena.
Mungu si Athumani 2021- ... Samia
Anapondwa sana,ooh nchi inaongozwa na madalali sijui Kikwete ndio anaongoza sio mama. Je kwenye utawala wa Magufuli hamkumkumbuka JK? Kwanini sasa mnamkumbuka Magufuli baada ya Samia kushika usukani?
Je, ni rais gani alikubalika na watanzania wote akiwa madarakani? Leo Samia mtamwona ni bure lakini umuhimu utaonekana siku akitoka madarakani.
Vumilieni tu.
Wakamtukana Mkapa wakati alianzisha TRA inayokusanya mabilioni kwa mabilioni yanayoendesha nchi kila kukicha, pamoja na taasisi nyingine za kiuchumi.
Wakamtukana Kikwete wakati ndugu zao wakivunjwa miguu kwa ajali za bodaboda wanakwenda kuungwa pale MOI.
Wanamtukana JPM wakati kajenga fly overs za kwanza tangu tupate uhuru pamoja na daraja la busisi na mambo mengi ya maana ameyafanya.
Mtanzania msikilize akiongea halafu tikisa kichwa kama ishara ya kukubaliana na anachosema, ukishaachana nae nenda endelea kufanya shughuli zako, kwa kifupi mpuuze.