mzeewaSHY
JF-Expert Member
- Aug 31, 2021
- 8,916
- 8,630
Huwezi kinganisha enZi za nyerere na hasani mwinyi kwa kuwa zile zilikuwa Enzi za giza
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huwezi kinganisha enZi za nyerere na hasani mwinyi kwa kuwa zile zilikuwa Enzi za giza
Sent using Jamii Forums mobile app
Syo nyie mlio muita mzee wa rhuksa??mkamchora palee chuo kikuu picha za ajabu?? eti anaongozwa na mkewe!!!!//siyo nyieMzee Ali Hassan Mwinyi
siyo nyie mlisema kajenga uwanja wa ndege kwao usio natija, mkabila dikteta, anakurupika siyo nyieHakuna wala hapatakiwepo Rais aliyekubalika Tanzania kama John Pombe Mahufuli.Kuanzia ushindi kwenye Sanduku la kura mpaka vichochoro vyote vya Tanzania.Kiongozi mwingine aliyefuatia ukimuacha Nyerere ni Edward Moringe Sokoine.Hao watu Mungu aliwaleta kwa kusudi maalum [emoji119]
kumbuka aliponapona kupinduliwa lkn!Mwalimu Nyerere alikuwa the best
Kama falsafa za Mwalimu zingefanikiwa kama alivyokuwa anataka Leo Tanzania ingekuwa mbali sana !! Angalia China walikuwaje miaka ya sitini na Leo wapo wapi !! Mkiendekeza kazi na bata mtasubiri sana !!!
Si rahisi kwa binadamu yeyote yule kukubalika na kila mtu kwa yale atendayo au asemayo. Hata jua likiwa kali wapo wanaoshukuru na wengine hulalamika.Baada ya vyama vingi 1995 mpaka 2005 Mkapa alipondwa sana,ooh katili, fisadi n.k akatoka. Watu wakasema bora Mwinyi tu mzee wa ruksa.
2005-2015 Kikwete kasi mpya nguvu mpya ari mpya, rais kijana,mcheshi lakini alikumbatia wezi, majambazi mafisadi tuhuma zote ziliibukia kwake. Akatoka akapondwa sana mpole mno,mwizi sana.
2015-2021 Magufuli akasifiwa mwanzoni baadae akaanza kuonekana katili,mkali dikteta mkabila n.k. watu wakaanza kukumbuka mazuri na upole wa JK na wengine wakafikia hatua ya kusema bora Kikwete agombee tena.
Mungu si Athumani 2021- ... Samia
Anapondwa sana,ooh nchi inaongozwa na madalali sijui Kikwete ndio anaongoza sio mama. Je kwenye utawala wa Magufuli hamkumkumbuka JK? Kwanini sasa mnamkumbuka Magufuli baada ya Samia kushika usukani?
Je, ni rais gani alikubalika na watanzania wote akiwa madarakani? Leo Samia mtamwona ni bure lakini umuhimu utaonekana siku akitoka madarakani.
Vumilieni tu.