Mimi sio Chawa wa Mama,wala sipo miongoni mwa watu wanaolipwa ili kumsafisha
Katika familia yapo mambo ambayo kiongozi wa familia anawajibika nayo kama mzazi na mengine ni ya wana familia wenyewe ( Watoto)
Kutoa Uhai wa mtu sio jambo jepesi kwakuwa linagusa dhamiri ya mtu,lina mgusa Mungu, linagusa jamii nzima,ile kwamba viongozi wamekupa amri haramu sio lazima uitekeleze.
Una utashi wa kuacha kazi kama unaona unachoamriwa kufanya kina kinzana na Nasfi,dhamiri, jamii na Muumba wako!
Tuwawajibisje Wauwaji,Mambao sasa wametamalaki kibinafsi, Wanaoua ni wauaji na wana Maslahi katika kila wanachofanya, hawamlindi Mama kwa kuua watu, wanajilnda wao na uovu wao
Baniani mbaya, lakini upatu wake apewe
Mungu ibariki Tanzania na watu wake!
Mkuu BOB LUSE, asante kwa kuja jukwani na kadi yako ya kujihami kuwa
"Mimi sio Chawa wa Mama." Inachekesha sana kuona mtu anaanza kujitetea kwa nguvu kabla hata hajaulizwa. Hiyo ni sawa na mtu anayeingia kwenye duka la nguo huku amevaa mashati matatu mapya halafu anasema
"jamani mimi sio mwizi." Utetezi wako wa mapema unathibitisha tu kuwa umerembesha mada hii kwa lengo moja tu: kumsafisha na kumtakasa bosi wako mkuu, huku ukitumia gia ya kuonekana uko
“neutral.” Huu ni u-chawa uliokomaa unaojificha nyuma ya falsafa za kubuni.
Katika aya yako ya pili, unapolinganisha muundo wa nchi na muundo vya familia ya mtaani inayoficha fimbo, unafanya kosa kubwa la ki-analojia na unadanganya jamii. Nchi haionzwi kwa mahusiano ya kifamilia, bali kwa mujibu wa
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayomweka Rais kama Amiri Jeshi Mkuu na kiongozi wa Mamlaka ya Utendaji. Vyombo vya usalama vinavyotekeleza mauaji ya Oktoba 29 hufanya hivyo kwa kutumia rasilimali, magari, na silaha zilizolipwa kwa kodi zetu. Kama huyo "mzazi" wako wa kitaifa hana habari au uwezo wa kudhibiti "watoto" wake wanaoua watu, basi hana sifa ya kusimamia nchi. Huwezi kutenganisha "watoto" watendaji na yule anayewapa rasilimali na madaraka ya kutumia nguvu hizo.
Ushauri wako kwenye aya ya tatu na nne kwamba watendaji wana amri haramu lakini wana
"utashi wa kuacha kazi" ni kichekesho cha mwaka kisichojua uhalisia vya sheria za kijeshi na vyombo vya usalama (Service Acts). Kwenye mifumo hii, muundo wa amri
(chain of command) umeshonwa kisheria kiasi kwamba mtendaji wa chini hawezi tu kuamua "kuacha kazi" kirahisi kwa sababu mfumo umejengeka kwenye hofu na uaminifu kwa mtoa amri mkuu. Kanuni ya sheria ya kimataifa ya Uwajibikaji wa Kikomandi
(Command Responsibility) inabainisha wazi kuwa kiongozi anapaswa kuwajibika ikiwa alijua au alipaswa kujua kuwa chini yake kuna makosa yanafanyika na akashindwa kuzuia au kuadhibu. Kwa kulaumu dhamiri ya mbwa mwitu badala ya mtu aliyemfunga kamba na kumwachia kwa wananchi, unalipotosha taifa kwa makusudi ili kumlinda aliyeko juu.
Mwishoni mwa uzi wako, unakiri mwenyewe kuwa
"wauaji wametamalaki na hawamlindi Mama bali wanajilinda wao." Hapa ndipo umefeli kabisa mtihani wa mantiki na kujikaanga kwa mafuta yako mwenyewe. Kama viongozi hawa wanajilinda katika uovu wao chini ya macho ya Rais pasipo kuchukuliwa hatua stahiki za kikatiba kama kuwafuta kazi, kuwakamata, na kuwashtaki, basi huo ndio uthibitisho mkuu kuwa uongozi wa juu umeshondwa au unabariki hayo matendo ili abaki madarakani.
Baniani hapa ni mbaya na upatu wake unapaswa kuvunjwa kuanzia kwa yule aliyemshika mkono na kumweka hapo alipo. Anayeshindwa kuwawajibisha wauaji chini ya utawala wake anapaswa kubeba lawama zote bila kukwepa!
Nimalize kwa kukukumbusha msemo mmoja wa kiingereza unaokuhusu sana unapojaribu kujivua u-chawa kwa lugha za kisomi:
"If you sound too good to be chawa, you are probably a chawa pro max!"