Rais hatakiwi kulaumiwa kwa mauaji ya Oktoba 29

Au sio
 


Mkuu BOB LUSE, asante kwa kuja jukwani na kadi yako ya kujihami kuwa "Mimi sio Chawa wa Mama." Inachekesha sana kuona mtu anaanza kujitetea kwa nguvu kabla hata hajaulizwa. Hiyo ni sawa na mtu anayeingia kwenye duka la nguo huku amevaa mashati matatu mapya halafu anasema "jamani mimi sio mwizi." Utetezi wako wa mapema unathibitisha tu kuwa umerembesha mada hii kwa lengo moja tu: kumsafisha na kumtakasa bosi wako mkuu, huku ukitumia gia ya kuonekana uko “neutral.” Huu ni u-chawa uliokomaa unaojificha nyuma ya falsafa za kubuni.

Katika aya yako ya pili, unapolinganisha muundo wa nchi na muundo vya familia ya mtaani inayoficha fimbo, unafanya kosa kubwa la ki-analojia na unadanganya jamii. Nchi haionzwi kwa mahusiano ya kifamilia, bali kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayomweka Rais kama Amiri Jeshi Mkuu na kiongozi wa Mamlaka ya Utendaji. Vyombo vya usalama vinavyotekeleza mauaji ya Oktoba 29 hufanya hivyo kwa kutumia rasilimali, magari, na silaha zilizolipwa kwa kodi zetu. Kama huyo "mzazi" wako wa kitaifa hana habari au uwezo wa kudhibiti "watoto" wake wanaoua watu, basi hana sifa ya kusimamia nchi. Huwezi kutenganisha "watoto" watendaji na yule anayewapa rasilimali na madaraka ya kutumia nguvu hizo.

Ushauri wako kwenye aya ya tatu na nne kwamba watendaji wana amri haramu lakini wana "utashi wa kuacha kazi" ni kichekesho cha mwaka kisichojua uhalisia vya sheria za kijeshi na vyombo vya usalama (Service Acts). Kwenye mifumo hii, muundo wa amri (chain of command) umeshonwa kisheria kiasi kwamba mtendaji wa chini hawezi tu kuamua "kuacha kazi" kirahisi kwa sababu mfumo umejengeka kwenye hofu na uaminifu kwa mtoa amri mkuu. Kanuni ya sheria ya kimataifa ya Uwajibikaji wa Kikomandi (Command Responsibility) inabainisha wazi kuwa kiongozi anapaswa kuwajibika ikiwa alijua au alipaswa kujua kuwa chini yake kuna makosa yanafanyika na akashindwa kuzuia au kuadhibu. Kwa kulaumu dhamiri ya mbwa mwitu badala ya mtu aliyemfunga kamba na kumwachia kwa wananchi, unalipotosha taifa kwa makusudi ili kumlinda aliyeko juu.

Mwishoni mwa uzi wako, unakiri mwenyewe kuwa "wauaji wametamalaki na hawamlindi Mama bali wanajilinda wao." Hapa ndipo umefeli kabisa mtihani wa mantiki na kujikaanga kwa mafuta yako mwenyewe. Kama viongozi hawa wanajilinda katika uovu wao chini ya macho ya Rais pasipo kuchukuliwa hatua stahiki za kikatiba kama kuwafuta kazi, kuwakamata, na kuwashtaki, basi huo ndio uthibitisho mkuu kuwa uongozi wa juu umeshondwa au unabariki hayo matendo ili abaki madarakani. Baniani hapa ni mbaya na upatu wake unapaswa kuvunjwa kuanzia kwa yule aliyemshika mkono na kumweka hapo alipo. Anayeshindwa kuwawajibisha wauaji chini ya utawala wake anapaswa kubeba lawama zote bila kukwepa!

Nimalize kwa kukukumbusha msemo mmoja wa kiingereza unaokuhusu sana unapojaribu kujivua u-chawa kwa lugha za kisomi: "If you sound too good to be chawa, you are probably a chawa pro max!"
 
Bado hamjasema
 
..barabara zikijengwa tunasema amefanya Mama.

..vyombo vikiuwa wananchi tunasema Mama hahusiki?

..kule kwenye barabara wakati mwingine huwa tunasema Mama ametoa fedha.

..sasa tuseme Mama hakuonekana mitaani akitwanga watu risasi.

..Je, hakutoa fedha na silaha zilizotumika siku mauwaji yanafanyika?

..Kwenye barabara Mama ametoa fedha. Kwenye mauwaji nani ametoa fedha?

..Na watoa amri na wasimamizi siku mauaji yanatokea ni wateule wa nani? Je, wamewajibishwa? Nani anapaswa kuwawajibisha?
 
Mkuu mtu asiposoma hadi hii paragrafu anaweza kukuogesha matusi lukuki
 
Basi tumsifu
 
Rejea kesi ya hayati Mwinyi alipojiuzulu kwa makosa ya polisi. Je, alishika mapanga na bunduki kuwaua wale wazee? Na je, issue ya mzee Mayala ilikuwaje ilihali yeye hakwenda eneo la tukio bali waliokuwa chini ya uongozi wake ndio waliofanya makorokocho. Kipi kiliwakuta hadi watakiwe kuondoka kwenye ofisi za umma? Mbona unajisahaulisha ilihali unao ushahidi wa kutosha na mifano hai?
Rais ndiye amiri jeshi mkuu kwa maana anamiliki dola, nini kinamzuia kufuata nyayo za mzee Mwinyi?
Na kwanini hataki kuwashitaki hao waliohusika kuua kwa niaba yake? Au unataka kutuaminisha kuwa yule trafiki aliyeonekana kwenye picha akiwalenga watu waliokuwa vibarazani kwao alivunja ghala la silaha na kuchukua bunduki na risasi bila maelekezo? You must be kidding right?
 
Rejea kesi ya hayati Mwinyi alipojiuzulu kwa makosa ya polisi. Je, alishika mapanga na bunduki kuwaua wale wazee?
Mkuu Mna, Mnasihi , mimi najihesabu ni mmoja wa jf tulioandika sana kuhusu October 29, nikasema wazi tena bila kigugumizi, PostGE2025 - Pascal Mayalla: Kama tungekuwa na media makini, waandishi wangechunguza nani alitoa amri ya kupiga watu risasi za moto Oktoba 29
Mbona nimeeleza kila kitu and I'm not kidding!.
P
 
Tuwawajibisje Wauwaji,Mambao sasa wametamalaki kibinafsi,
Huyo rais unayemsemea hapa, kama hahusiki na mauaji yale, umeona wapi akiwa na nia ya kuwawajibisha wauwaji? Au wewe unataka tuwawajibishe vipi kama rais anawakingia kifua?
 
Wanaharakati wanajitoa ufahamu tu ila hawawezi kwepa lawama katika hili.

Zile vurugu walizichochea wao.
 
Sehemu pekee ambayo ingemtenganisha na mauaji ni Ripoti ya Jaji Chande… ilikua ndio kete yake ya kutoa Kafara Jini litulie lakini…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…