Pre GE2025 Rais Hussein Mwinyi tunakutaka utuletee Maendeleo Bara kama unavyofanya Zanzibar

Pre GE2025 Rais Hussein Mwinyi tunakutaka utuletee Maendeleo Bara kama unavyofanya Zanzibar

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CDF alitushtua viongozi wengi sio wazalendo wengi ni mamluki wa mataifa jirani.

Ndio maana hawaoni aibu kutuhujumu.
Kweli Mkuu..
Usije kuta tunaongozwa na watoto wa wakimbizi bila kujua
 
Kama Hujui Maendeleo Ya Zanzibar Yanatokana Na Pesa Tunazokopata Tanzania Sasa Nyingi Kule Zinaelekezwa Kwenye Miradi.Huku Tunatazama Wahuni Wao Wanagawana Tu
Nguvu Kubwa Wamezielekeza Kwenye Madaraka Yaani Chaguzi Zote Wabaki Kwenye Viti
 
🚮🚮 Mwendazake alianzisha na kukamilisha miradi gani Kwa wakati?

Pili tuoneshe figures za mfumuko wa bei huko Zanzibar tuthibotishe.

Mwisho kwani Bara Kuna mfumuko wa bei upi?

Hater wa Samia acha kutapatapa wewe ,Samia amefunika ligacy zote yaani Kwa miaka 3 ni game changer
Kwa hiyo kwa akili yako ulitegemea SGR, JNHPP, SERIKALI KUHAMIA DODOMA, BUSISI/JPM BRIDGE, ZILE NDEGE ZA ATCL, KIJAZI INTERCHANGE, SALENDAR BRIDGE, FLYOVERS (KAMATA NA TAZARA-DSM) N.K viishe ndani ya muda wa miaka mingapi?
Figures za Mfumko wa bei zanzibar ni karibu asilimia 0 (nimesema hapo juu) ilhali huku kwetu nadhani unazidi hata asilimia 7!
Hiyo ya Samia kufunika sina uhakika, labda atakuwa amefunika mfukoni mwako kwa vile karuhusu Kula kwa urefu wa kamba!
Vinginevyo, binafsi naona kwa sasa huu mwendo tunaoenda nao, hata wa kinyonga una nafuu!
 
Hussein Mwinyi yupo vizuri. Mimi namkubali.
Tuko pamoja Mkuu.
Hata mwamba Hayati JPM alimkubali sana.
Kwanza ni mchapa kazi hodari, pili hana makuu kama baba yake, tatu Hataki mzaha linapokuja suala la nidhamu serikalini
 
Halafu je unajuwa kuwa Rais Samia anasukuma miradi mingi ZNZ kwa fedha za kutoka Serikali ya Muungano?
Hata uwaambiaje, hawaelewi! Pesa zooote za Tanganyika zimeelekezwa Kizimkazi, sasa sehemu yenye bajeti ya 450bn kwa mwaka, leo unawapa 400bn kwa mkupuo, nje ya bajeti!

Usipofanya hiyo miradi, utakuwa ni fisadi kiwango cha msoga sasa!
 
Wakati Rais Hussein Mwinyi anaingia madaralani, uchumi wa Zanzibar ulikuwa kunakuwa kwa asilimia zisizozidi 5. Lakini ndani ya kipindi cha miaka 3 tu uchumi wa Zanzibar leo unakua kwa asilimia 6.8 huku wa bara ulikuwa unakua kwa asilimia 7 kabla ya kifo cha Rais Hayati JPM tena katikati ya janga la dunia Covid 19, lakini mwaka mmoja tu baadaye (baada ya kifo cha JPM), uchumi wetu ukadorora hadi kufikia asilimia 4!

Leo hii Zanzibar miradi imekuwa inaanzishwa na kukamilika tena kwa wakati na ubora wa hali ya juu tena kwa Gharama zile zile zilizowekwa. Lakini kwa upande wa bara tumekuwa tunapigwa tu kalenda (mfano SGR, JNHPP, JPM Bridge n.k)!

Mfumko wa bei kwa Zanzibar ni karibu asilimia 0, lakini kwa huku bara toka aondoke Rais aliyepewa dhamana na wengi, leo mfumko wa bei kila mmoja ni shuhuda! Na bahati nzuri wengi wetu (ukiondoa mafisadi na familia zao) tunapigika ipasavyo. Mfano nauli za daladala toka 300 hadi 600, nauli za mabasi ya mikoani kama vile Mwanza hadi Dsm kutoka elfu 60 hadi zaidi ya elfu 80, sukari toka 1,600 hadi 5,000 kwa kilo, mche wa sabuni toka 1,500 hadi 3,500! N.k.

Kwa hayo machache, naona kama Mtanzania mzalendo, ninayeipenda nchi yangu na raslimali zake zote ikiwemo watu, Rais Hussein Mwinyi atatufaa zaidi akija huku Bara. Mama tunampenda sawa, lakini amalizie tu hii miaka yake ya urithi aende zake akalee wajukuu zake huko Kizimkazi.
Umenena
 
Hii nchi imekosa watu had huyo mwinyi mumpambe kila kukicha? Au kuna mgao wenu umeandaliwa?
Machawa muwage mnajistukia muda mwingne.
 
Nami nashauri kwa manufaa ya nchi hii pendwa...Rais Samia SH angempisha Rais Hussein AHM 2025 .....atupigie miaka 10....Msna amefanya kazi nzuri kutuvusha ila asiharibu akapata tamaa....hapana apumzike Abdul amkabidhi HAHM.....yeye abakie remote kake pale atspopenda...awe mshauriii.....kama anamasikio na asikie....na afanye hatajuta maishaniii
Ushauri mzuri sana Mkuu japo kwa kila utawala kuna "wanufaika" ambao hawajali maslahi ya nchi bali maslahi yao na familia zao binafsi kama ilivyokuwa kipindi cha Hayati Nyerere. Kwa hao lazima watamlazimisha agombee urais 2025, lakini kwa maslahi ya nchi, na mimi nashauri achukue ushauri wako, apumzike.
 
Mwinyi sio mjamaa mbuzi ni Rais wa reforms kama Samia ,kuanzia ubinafsishaji Hadi Demokrasia.

Bara kumejaa mbumbumbu kama wewe ambao mtu akiwa na Mali mnaumia roho.

Mwinyi alisema leta pesa kokote yeye haulizi zilikotoka,sasa thubutu kufanya hivyo ukutane na matakataka ya Bara
Wengi hatuumii kwa sababu mtu kapata fedha, ila tunaumia kwa sababu wengi wenye fedha hawazipati kihalali, bali wanazipata kwa kutuibia.
 
Kwa hiyo kwa akili yako ulitegemea SGR, JNHPP, SERIKALI KUHAMIA DODOMA, BUSISI/JPM BRIDGE, ZILE NDEGE ZA ATCL, KIJAZI INTERCHANGE, SALENDAR BRIDGE, FLYOVERS (KAMATA NA TAZARA-DSM) N.K viishe ndani ya muda wa miaka mingapi?
Figures za Mfumko wa bei zanzibar ni karibu asilimia 0 (nimesema hapo juu) ilhali huku kwetu nadhani unazidi hata asilimia 7!
Hiyo ya Samia kufunika sina uhakika, labda atakuwa amefunika mfukoni mwako kwa vile karuhusu Kula kwa urefu wa kamba!
Vinginevyo, binafsi naona kwa sasa huu mwendo tunaoenda nao, hata wa kinyonga una nafuu!
Wewe ulitaka ziishe ndani ya mda gani zaidi ya miaka 5?

Karibu na zero ndio kitu gani?

Mwisho Kwa hiyo huyo tumitadi ndio kwako unaona ni Mingi sana ku justify miaka 5 au?

Mwisho Mbona Kuna miradi Mingi sana zaidi ya hiyo inaendelea na ni mabilioni Kwa mabilioni?

Tumiradi twa Zanzibar hatufikii mradi hata mmja wa njia 4 Igawa-Mbeya zaidi 1.1Trilioni sijataja viwa ja zaidi ya 15 vya ndege vinaendelea na ujenzi Nchi nzima.
 
Wakati Rais Hussein Mwinyi anaingia madaralani, uchumi wa Zanzibar ulikuwa kunakuwa kwa asilimia zisizozidi 5. Lakini ndani ya kipindi cha miaka 3 tu uchumi wa Zanzibar leo unakua kwa asilimia 6.8 huku wa bara ulikuwa unakua kwa asilimia 7 kabla ya kifo cha Rais Hayati JPM tena katikati ya janga la dunia Covid 19, lakini mwaka mmoja tu baadaye (baada ya kifo cha JPM), uchumi wetu ukadorora hadi kufikia asilimia 4!

Leo hii Zanzibar miradi imekuwa inaanzishwa na kukamilika tena kwa wakati na ubora wa hali ya juu tena kwa Gharama zile zile zilizowekwa. Lakini kwa upande wa bara tumekuwa tunapigwa tu kalenda (mfano SGR, JNHPP, JPM Bridge n.k)!

Mfumko wa bei kwa Zanzibar ni karibu asilimia 0, lakini kwa huku bara toka aondoke Rais aliyepewa dhamana na wengi, leo mfumko wa bei kila mmoja ni shuhuda! Na bahati nzuri wengi wetu (ukiondoa mafisadi na familia zao) tunapigika ipasavyo. Mfano nauli za daladala toka 300 hadi 600, nauli za mabasi ya mikoani kama vile Mwanza hadi Dsm kutoka elfu 60 hadi zaidi ya elfu 80, sukari toka 1,600 hadi 5,000 kwa kilo, mche wa sabuni toka 1,500 hadi 3,500! N.k.

Kwa hayo machache, naona kama Mtanzania mzalendo, ninayeipenda nchi yangu na raslimali zake zote ikiwemo watu, Rais Hussein Mwinyi atatufaa zaidi akija huku Bara. Mama tunampenda sawa, lakini amalizie tu hii miaka yake ya urithi aende zake akalee wajukuu zake huko Kizimkazi.
Changamoto ni kwamba akija bara nani atamuwezesha?
 
Tanzania tuko nyuma sana kwa mambo mengi, tunapaswa kupata viongozi wenye kasi hasa kwa mambo ya maendeleo ya nchi kwa ujumla. Kwa hili naona Mh. Rais Hussein Mwinyi, atatufaa sana.

Hiyo Miradi ya Zanzibar inakamilika kwa wakati kutokana na mikopo inayokopwa na serekali ya muungano. Mwinyi akija huku kama utakavyo atatukuta kwenye kipindi Cha kulipa mikopo.
 
Nahuyo uno ona anafaa baada ya mwaka mmoja akija bongo utasema hafai,ttzo ubinafsi,ufisad na roho mbaya ndio unokusumbueni, wabongo hamuelewek mnatk kiongoz wa aina gn mkapa mlisema alibinafsisha mashirika ya umma nch kaiacha na hasara, kikwete mlisema anacheka cheka tu, jpm mkasema dikteta,ssh mnasema hafai,kwa mtu mwenye akili timamu tokea kuingia madarakan atagundua ssh amejitahid mno kaifungua nchi kidplomasia na demokrasia imekuwa ya hali ya juu na uchumi umeanza kuimarika hatua kwa hatua, ilifikia hatua wafanya biashara, wanasiasa walikimbia hii nchi tusijitowe ufaham lkn uyo mnoona hafai ssh ndie aloweka mazingira wafanya biashara na wanasiasa kurudi na kuendeleza nchi,km binadam ssh hawez kuwa na ubora wa utendaji wa jambo lolote kwa asilimia 100 kwa upande wa znz tokea awamu ya aman karume utagundua znz kumekuwa na ujenzi wa miundo mbinu kwa kasi sana kulingana na awamu nyengine kwa kila awamu mfno dkt shein kwa kila mzanzibar anajua nn alifanya katika kuijennga znz mpya unayo yaona mafanikio leo znz nimuendelezo na mikakati ilojiwekea smz ya ujenzi wa znz, wamejielewa siasa za majitaka haina faida kwao,namna ya wasaidiz wa rais wa smz pengine kuna utafaut wa mikakati na utekelezaji wk ndio mana unaona kasi hii ya kutisha ya maendeleo inatarajiw znz baada ya miaka 20 kutakuwa na mabadiliko makubwa ya maendeleo ya kiuchumi,sasa nadhani wa bongo kuna jambo nilzima muelew jee ttzo liko kwa rais au wasaidiz wk ndio wanokwamisha maendeleo ya kiuchumi vyenginevo msubir ashuke malaika aje aku ongozen ndio mtaridhik uongoz wk
 
BREAKING: Chanzo chetu cha uhakika kinatutaarifu kwamba, Mh. Simai amejiuzulu kutokana na swala la ufutwaji wa leseni za kampuni 3 za vileo. Huu ni uamuzi ambao umefanywa na Rais Hussen Mwinyi ili makampuni yake yachukue hizo nafasi. Tuna taarifiwa kuwa Mwinyi ana ikamua Zanzibar
20240127_102607.jpg
20240127_102603.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom