Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Hapo ulipotaja mapungufu ndipo penye tatizo. Wewe unaona ni mapungufu madogo madogo wakati hayo ndiyo makubwa.Siwezi kukulazimisha kuona kama mimi nilivyoona Mkuu.
Lakini nina imani kwa kila Mtanzania mwenye akili timamu atakiri wazi ya kuwa mwamba alifanya kazi ukiachilia mbali mapungufu yake madogo madogo (ambayo hata hivyo hayakuwa na madhara kwa wanyonge, isipokuwa kwa mafisadi na mafisi wa raslimali za nchi hii na familia zao). Miradi kama JNHPP, SGR, serikali kuhamia Dodoma, Daraja la JPM-Busisi, Salendar Bridge, JNIA Terminal 3, Flyovers, Ubungo Interchange (Kijazi Interchange) n.k.
Yote hiyo ilikuwa ni miradi ya kizalendo na yenye kuhitaji kujitoa kafara kuianzisha.
Kingine, hata wewe utakiri kwamba matatizo ya TANESCO na katakata ya umeme yalipungua sana wakati wake.
Mtu anayetawala bila kufuata Katiba, mtu anayetisha Mahakama zisifanye kazi, mtu anayesimamisha shughuli za vyama vya siasa na mtu anayekandamiza uhuru wa maoni siyo mapungufu madogo.
Magufuli alinyang'anya fedha za wafanyabiashara, akawarundika rumande kwa kesi za uhujumu uchumi ma kesi zenyewe zikakosa ushahidi ndiyo unasema mapungufu madogo madogo??
Magufuli aliua wakosoaji kama kina Ben Saanane, alishambulia wapinzani kwa bunduki kama Tundu Lissu, bado unasema mapungufu madogo?
Unaongelea suala la kujenga Busisi, SGR sijui na flyover? Kwani kuna Rais amewahi kutoka madarakani bila kujenga miundombinu yeyote?
Kama yupo Rais kabla ya Magufuli ambaye hakujenga miundombinu mtaje hapa, nami nikuwekee kazi alizofanya!!
Magufuli angekuwa mwema basi angekuwa hai mpaka leo!! Ila amekufa kwa madhambi yake. Muache aendelee kuungua na moto wa jahanam