COARTEM
JF-Expert Member
- Nov 26, 2013
- 3,603
- 3,658
Lengo la Serikali kufanya ugatuaji wa Madaraka lilikuwa bora sana na kila mtu analipongeza. Kwa sasa mambo yanavyokwenda SEKTA ya Afya ni kama kuna Wizara Mbili tofauti za Afya, yaani WIZARA MAMA YA AFYA (MOH) na WIZARA NDOGO YA AFYA (Idara ya Afya OR-TAMISEMI).
Ukienda Halmashauri na Mikoani, Waganga wakuu wa Wilaya (DMOs) na Waganga wakuu wa Mikoa (RMOs) wanasikiliza maelekezo ya Viongozi wa OR-TAMISEMI zaidi kuliko maelekezo ya Viongozi wa Wizara ya Afya (MOH).
Mambo yakienda mrama sekta ya Afya huko Halmashauri na Mikoani, wizara inayolalamikiwa ni WIZARA YA AFYA na siyo OR-TAMISEMI. Utendaji wa Watumishi wengi wa OR-TAMISEMI kwakweli una mashaka sana, wengi wao wakienda Mikoani na Halmashauri kazi yao ni kuzurura tu.
Viongozi wa Wizara ya Afya wakipita Halmashauri na Mikoani ambako tayari watendaji wa OR-TAMISEMI walipita kufanya usimamizi shirikishi wanayakuta madudu mpaka mtu unajiuliza, hivi hata jambo dogo kama hili OR-TAMISEMI-Afya hawakuliona?
Mhe. Rais Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati vikiwa na huduma Mbovu, lawama zote zinapelekwa WIZARA YA AFYA. Hapo OR-TAMISEMI haiwezi laumiwa na Wananchi kwani Mwananchi yeye anaijua Wizara ya Afya.
Kwahiyo ili kuipa nguvu Wizara ya Afya, inatakiwa utendaji wa kila siku wa Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya, Zahanati usimamiwe na Wizara ya Afya.
Kwahiyo RMO na DMO wanapaswa wawajibike moja kwa moja kwa CMO ili mambo yaweze kwenda vile unavyotamani kuiboresha sekta ya Afya.
Mbaya zaidi kumezuka kiburi kwa hawa DMOs na RMOs kutotii ziara za Viongozi wa MOH wakidai wao wanawajibika moja kwa moja OR-TAMISEMI. Mheshimiwa Rais Maboresho sekta ya Afya hayatafanikiwa kama kutaendelea kuwepo kwa Idara ya Afya-OR TAMISEMI. "Hata Biblia inasema huwezi tumikia mabwana wawili maana utampenda huyu na kumchukia yule."
Ushauri:
Irudishe Idara ya Afya -OR TAMISEMI iende kuwa chini ya Mganga Mkuu wa Serikali (CMO) ili uwajibikaji wao usimamiwe na Wizara Mama ya Kisekta. Kwa kufanya hivyo utakuwa umesaidia sana kuimarisha utendaji kazi wa SEKTA YA AFYA Halmashauri na Mikoani.
Naomba kuwasilisha Ushauri wangu huu.