Rais inawezekana vipi kujibizana na Josephat Gwajima? Mbona sielewi!

Yapo majina 83 kwenye list ya Gwajina yenye watu waliotekwa na kupotezwa....

Kwahiyo Vyombo vya ulinzi vijitokeze ama vikanushe au vithibitishe..mbona simpoooo.

Sasa mambo ya kushughulikiana yanakujaje 🤣🤣🤣
Mahakama hazipo? Ikiwa kuna upotoshaji.
 
Yesu alitoka mbinguni na kuja kuwakombo wa duniani
Yesu hajawahi gombea cheo chochote cha kidunia hata wayahudi walipotaka kumkamata na kumfanya mfalme wa wayahudi alikataa akawatoroka
 
Mavi matupu
 
Yaani unaunga mkono mauaji au na wewe ndio genge la wauaji?

Gwajima kasema watu wametekwa na wameuwawa serikali kwanini haitoi majibu juu ya matukio hayo.

Watu wataelewaje nani mhusika kama serikali ipo kimya?

Miezi 9 sasa tangu mzee Kibao auwawe hakuna ripoti hata moja ya uchunguzi wa kifo chake .

Soka aliitwa kituo cha polisi Chang'ombe hadi leo ni miezi 10 hajulikani alipo.

Mdude kavamiwa kwake na watu walipojitambulisha kuwa ni polisi wameondoka nae hadi leo hajulikani alipo.

Sativa katekwa Dar es Salaam kaenda kuokotwa Katavi mbugani , checkpoint zote hawa watekaji walipita , geti la mbugani la kutoka na kuingia walipitaje bila kukaguliwa .

Kitima kashambuliwa na mtu mmoja siku chache kabla alitoa tishio mtandaoni tukaambiwa anashikiliwa ila hakuna mahali tumeona amefikishwa mahakamani.

Nani atupe majibu kama sio serikali?


Polisi wako busy kuzuia watu wasiende kusikiliza kesi mahakamani ila hawatimizi jukumu lao kuu la kulinda raia na mali zao.

Badala ya kujibu hizo hoja nyie mmesema rais anatukanwa?

Hivi rais huyu kwa matusi yake ya kutoa kauli kama.
Your browser is not able to display this video.


"MBWA WAPUMBAVU"

"JITU"

"KIFO NI KIFO "


Hamjawahi kuyasikia?
 
Hakika kwa Uthubutu GWAJIMA anakuwa na uzalendo na Utanzania na asiye pendezwa na uharibifu wa kishetani juu ya Taifa letu

Itoshe kusema tumuombee sababu ameitwa kamati ya maadili ya Bunge kwa kusema ukweli.
 
OMG… Is this ignorance or idiocy? Wewe na wengine wa aina yako ndio mnampotosha huyo kenge na kumfanya awekeze muda mwingi katika mipango ya kuteka, kutesa na/au kuua raia wanaomkosoa. That’s barbarism!
 
Tanzania ina watanzania milioni 60 Mungu hasemi na yeye tu

Gwajima nabii wa uongo aliahidi wana Kawe atatupeleka Birmingham hajawahi tupeleka
Mwenzenu anafanya anayosikia na kuambiwa na Mungu wake.....

Nyie nanyi fanyeni yale ambayo miungu yenu inawaambia.

Hata Waisrael waliotoka Misri walikuwa karibu 600,000 Lakini aliyekuwa anasema na Mungu ni mmoja tu, Musa au Moses..

Musa au Moses wetu wa leo na kiongozi wa ukombozi wa Tanganyika ni Mch. Josephat Gwajima...
 
Kwani Gwajima kafanyaje?
 
Mpaka saivi hakuna hoja ya gwajima iliyo jibiwa hata moja lkn kunamaneno yasio kuwa na hoja kuhusu alicho kisema gwajima
 
Mbona ume base sana kwenye dini pekee na sijaona ukigusia vyeo vya dini vya msemwa B. Ningependa pia uje katika elimu,uwezo wa kuibua hoja na uwezo mkubwa wa kujieleza. Je, na haya sio vigezo vinginevyo vinavyomfanya Gwiji MA kuwa Bora zaidi.


Acha nimkumbushe, katika ukristo utumishi wa mungu ni kujitoa kiimani kumtumikia muumba na sio kifungo Cha maisha ya utendaji, wapo watumishi Madaktari, Walimu, Wasanii na wapiga vyombo, Wanasheria. Sasa kama Hawa wote wanayonafasi ya kuzitumikia taaluma zao ajabu iko wapi Kwa mtumishi wa mungu kuwa Mwanasiasa? Elimu inamruhusu na dini yake iko wazi haimfungi kuwa akiwa mtumishi asifanye mambo mengine halali katika kutumika katika jamii. Mbona mnawapeleka watoto wenu seminari na hamsemi wale watumishi waache kuongoza shule wakaongoze Misa kanisani.

Open your mind mkuu.
 
Mbona mnawapeleka watoto wenu seminari na hamsemi wale watumishi waache kuongoza shule wakaongoze Misa kanisani.

Open your mind mkuu.
Seminary za katoliki huzijui wewe
Wanafundisha masomonya kawaida shule za sekondari zote form one hadi form six na unalipa mzazi au mlezi hawasomeshwi kuwa lazima wawe mapadre kinachoongezeka ni masomo ya dini bible knowledge nk kwa Seminary za kiislamu linaongezeka somo la Islamic knowledge nk

Lakini kote hawaandaliwi kuwa mapdre au mashehe .Huo ni wito Wanaotaka wakimaliza sekondari na kufaulu mitihani ya taifa huenda kujiunga vyuo vya upadri au ushehe huko.Wengine huenda vyuo vya kawaida waendelee na maisha fani zingine za kidunia

Shida inakuja kwa watu kama Gwajima kusema cheo chake anasema kikubwa kuliko vya dunia lakini huyo mbio anaenda kugombea ubunge na vyeo CCM

Papa hana mpango huo anaamini cheo chake kikubwa kuliko vya dunia

Na maraisi na wafalme dunia nzima wanamheshimu akiwa huko huko kanisani kwake akiwa sio mbunge ,wala kiongozi wa siasa
 
Nchi ni yetu sote. Kiongozi anawekwa na Wananchi Kwa kipindi Fulani baada ya hapo anweza kuja mwingine. Katiba yetu inaruhusu Uhuru wa mawazo. Pia sioni shida iko wapi tukikosoa mahali tunapoona hapako Sawa Kwa maslahi ya taifa. Shida iko wapi na sioni inamuathiri vipi kiongozi.
 

iCcm ni chama kinacho heshimu demokrasia na uhuru wa kujieleza hacha kukifundisha uzandiki. Watu kama wewe ndio mnaharibu taswira ya chama kwa ushauri wenu wa hovyo.
Usimfundishe raisi wetu kazi anayoijua kaa kimya hacha kujipendekeza. Tafuta kazi fanya riziki Yako itakukuta huko, sio katika hizi fitina dhidi ya binadamu mwenzako anayetumia katiba ya nchi inayompa uhuru kuelezea hisia zake.
 
Sio kwa nia mbaya ila niseme tuu kwamba, Mama ana feli sana. Hana subira.. Hivi alishindwa kumuita Gwajiboy na kumsikiliza? Mambo ya aibu sana haya
 
Rais anajibizana na Gen Z wa Kenya nini Gwajima.
 
Mkuu hayo mambo ya kufundshwa kuwa mapadre umesema wewe, Mimi hoja yangu ni watendaji na uhuru walionao wa kufanya mambo mengine ikiwa pamoja na kumtumikia taaluma nyinginezo ukitoa utumishi wa mungu, hyo njo nafasi inayomfanya pia gwajima kuwa Mwanasiasa ukiachilia mbali kuwa kiongozi wa dini. Huku sisi hatuna mambo ya elimu dunia Wala ahela, Kila kimoja kinanafasi Kwa Kila kuumbe hai

Nimeanza kuhofia pia uwezo wako wa uelewa mkuu, kama hoja ndogo kama hizi unashindwa kuzielewa utaweza kuelewa maono mapana yaliyopo kwenye kampeni ya "NO REFORMS NO ELECTION".

Watawala Wana supporters wengi sana ambao ukiwaweka chini uwahoji hawajui wanabisha Nini Wala Wana support Nini🤣🤣 vyama sio ukoo wakuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…