Elections 2015 Rais Jakaya Kiwete ashitakiwa Mahakama ya Kimataifa ya ICC

Elections 2015 Rais Jakaya Kiwete ashitakiwa Mahakama ya Kimataifa ya ICC

sifa ya kuwa shabiki wa chadema uwe na akili ya kiwendawazimu.
hizo ni dalili za kushindwa uchaguzi hakuna hoja naona wanataka kubadilisha cd baada ya kushindwa miaka yote chadema ni waleta fujo
Kuweni wapole Chadema ya leo siyo ya Slaa mliyekuwa mmemuweka mfukoni.
 
The International Criminal Court (ICC or ICCt)[SUP][2][/SUP] is an intergovernmental organization and international tribunal that sits in The Hague in the Netherlands. The ICC has the jurisdiction to prosecute individuals for the international crimes ofgenocide, crimes against humanity, and war crimes. The ICC is intended to complement existing national judicial systems and it may therefore only exercise its jurisdiction when certain conditions are met, such as when national courts are unwilling or unable to prosecute criminals or when the United Nations Security Council or individual states refer investigations to the Court.
 
Bila Security council ama bunge la Tanzania kupeleka kesi ICC sidhani kama kuna kitu, nafikiri CHADEMA wana muhemko usio na tija. either wanajiandaa kufanya fujo makusudi ili wapigwe walie ICC si mumeona.

Serikali iwaelekeze kwa wingi wakaguzi wa kimataifa sehemu ambapo CHADEMA wanafahamika kwa kuanzisha fujo, ili wapige picha wenyewe.
 
Bila Security council ama bunge la Tanzania kupeleka kesi ICC sidhani kama kuna kitu, nafikiri CHADEMA wana muhemko usio na tija.
Sheria ya wapi hiyo niumizwe mimi nisubiri bunge likashitaki, Chadema ni taasisi inayotambulika kisheria ina haki ya kushitaki popote pale.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemshitaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete. Anaandika Josephat Isango.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mchana ukumbi wa Kisenga uliopo Millenium Tower, wakili wa Chadema, John Mallya amesema Kikwete ameshitakiwa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Mahakama ya kihalifu Uholanzi kwa sababu anatumia madaraka yake vibaya kutisha wananchi kuelekea uchaguzi mkuu.

Mallya alisema kuwa Mashitaka hayo yameelekezwa Umoja wa Mataifa lakini pia nakala za tuhuma dhidi ya Kikwete zimepelekwa pia Umoja wa Afrika (AU) na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita iliyopo The Hegue Uholanzi.

Kwa mujibu wa wakili huyo wa Chadema, barua hiyo ya tuhuma dhidi ya Kikwete imesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Prof. Abdallah Safari.

Mashataka haya yanakuja ikiwa ni miezi miwili tangu Rais Kikwete kuilamu Mahakama hiyo ya kihalifu kwa kusema kuwa viongozi wa Afrika hawafurahii kwa namna ambavyo mahakama hiyo inavyofanya kazi zake kwa kuwashughulikia zaidi viongozi wa mataifa ya Afrika.

Kauli hiyo ya Rais Kikwete aliitoa jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa 16 wa Umoja wa Wanasheria wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini mwa Afrika-SADC,

Hiyo ilikuwa ni siku tu moja baada ya ICC kueleza kwamba inafuatilia mwenendo wa uchaguzi nchini Tanzania.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda, alikaririwa na vyombo vya habari vya Aljazeera na Gambia Today akisema kuwa Mahakama hiyo inatazama kwa umakini mkubwa yanayotokea Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu kama ilivyofanya katika nchi za Kenya, Ivory Coast na Congo na kwamba itachukua hatua za haraka kama kutakuwa na uvunjaji wa haki za binadamu.

Kauli hiyo ya Bensouda ilitanguliwa na ile iliyotolewa na mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

Lowassa alilazimika kusema hayo katika ziara ya kutafuta wadhamini katika mikoa ya Arusha na Mwanza, Lowassa akilitahadharisha Jeshi la Polisi juu ya uwepo wa Mahakama ya ICC kutokana na kitendo chake cha kutumia nguvu dhidi ya wapinzani kwa kuupiga mabomu msafara wake.
12038093_528849780603880_4421614170556598052_n.jpg
 
Sheria ya wapi hiyo niumizwe mimi nisubiri bunge likashitaki, Chadema ni taasisi inayotambulika kisheria ina haki ya kushitaki popote pale.

Sina hakika na unachosema na sina haja ya kubishana
 
Ni punguani pekee ndo anaweza asijue REPUTATION YA JK KIMATAIFA, jipeni moyo mazoba! Nadhani kuna midudu ya kiyahudi Tanzania isiyojua hata majukumu ya ICC
Mdharau mwiba.....nyie endeleeni kupuuza siku mkimuona kapandishwa ndege akili zitawarudi.
 
Sina hakika na unachosema na sina haja ya kubishana
Siyo kwamba huna hakika ila hujui unachoongea...unatuambia eti bunge ndilo lenye uwezo wa kupeleka mashtaka ICC sheria ya wapi hiyo.
 
Siyo kwamba huna hakika ila hujui unachoongea...unatuambia eti bunge ndilo lenye uwezo wa kupeleka mashtaka ICC sheria ya wapi hiyo.

9. Is the ICC meant to replace national courts?No. The ICC does not replace national criminal justice systems; rather, it complements them. It caninvestigate and, where warranted, prosecute and try individuals only if the State concerned does not,cannot or is unwilling genuinely to do so. This might occur where proceedings are unduly delayed orare intended to shield individuals from their criminal responsibility. This is known as the principle ofcomplementarity, under which priority is given to national systems. States retain primary responsibilityfor trying the perpetrators of the most serious of crimes.

http://www.icc-cpi.int/iccdocs/PIDS/publications/UICCEng.pdf
 
Huko mlikopeleka safi sana, maana mzungu ukimpelekea kitu anaanza kuku investigate kwanza mtoa taarifa. Maana hata kwao wanafahamu ukipiga kura unaenda nyumbani, sasa watashangaa kuona unamshitaki mtu eti kakwambia urudi nyumbani kutoka mita 200. Mzungu kwa hakika ataanza na CHADEMA, if any.

Hata akina Rutto walifikiri mwizi wa kura ndo atapelekwa ICC kinyume chake wao waliosema wameibiwa ndo bado wanaburutwa ICC Kenya. Waliotuhumiwa kuiba kura karibu wote wako free
 
hata hao wawndesha mashtaka wa ICC wawe wajinga kiasi gani hawawezi kumtuhumu JK kwa hilo labda afanye kosa jingine.

kwani tanzania hakuna mahakama.... mbona watz mnajivua nguo wenyewe..!

Hv mahakama za tz zina hyo jurisdiction?
 
Bora siku kadhaa hizi ziishe ili watu wanyamazishwe kwa kura watulie kabisa kama maji mtungini.
 
Back
Top Bottom