Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha watushangaee tu kwani sisi ni wakwanzaa?watanzania wengi ni wajinga wa kutupa.... eti tunaanza kushtakiana nje ya nchi si ujinga kabisa huu... hata wao ICC wanatushangaa kwa kweli...
mfia maji haachi kutapatapa
Tena lifungwe maisha kabsa hatutaki kuliona kwenye nch yetu
ICU ni Intensive Care Unit.Nendeni huko ICU lakini nchi yetu hatuwapi iwe nyinyi ama hao ICU ...mmeshiñdwa kwenye kura sasa mnaanza kujitoa akiri, mnalo na kumbwela mbwela
Ulaya mawakala wanaaminika sana huwa hawachukui Rushwa, huku Tanzania Membe na wahindi matajiri wamechanga mabilioni huku Membe akitoa yale mapesa ya Marehemu Gadafi kwa ajili ya kazi moja tu kuwanunua mawakala wote wa Ukawa na vyama vingine usifananishe Tanzania na ulaya wala kenya hii Tanzania ina vitabia vya kipekee ndiyo Maana ICC itawakamata watoa kauli pekee si wapiga kura au walinzi wa kuraHuko mlikopeleka safi sana, maana mzungu ukimpelekea kitu anaanza kuku investigate kwanza mtoa taarifa. Maana hata kwao wanafahamu ukipiga kura unaenda nyumbani, sasa watashangaa kuona unamshitaki mtu eti kakwambia urudi nyumbani kutoka mita 200. Mzungu kwa hakika ataanza na CHADEMA, if any.
Hata akina Rutto walifikiri mwizi wa kura ndo atapelekwa ICC kinyume chake wao waliosema wameibiwa ndo bado wanaburutwa ICC Kenya. Waliotuhumiwa kuiba kura karibu wote wako free
sifa ya kuwa shabiki wa chadema uwe na akili ya kiwendawazimu.
Hizo ni dalili za kushindwa uchaguzi hakuna hoja naona wanataka kubadilisha cd baada ya kushindwa miaka yote chadema ni waleta fujo
Dalili za kushindwa? Huna ht aibu atashindwa Magufuli na ccm yenu.Lowassa ndie rais haki ya mungu wewe hujui tu huku kitaa mambo ni mazito.
hata hao wawndesha mashtaka wa IC hawawezi kumtuhumu JK kwa hilo labda afanye kosa jingine.
kwani tanzania hakuna mahakama.... mbona watz mnajivua nguo wenyewe..!
Ni punguani pekee ndo anaweza asijue REPUTATION YA JK KIMATAIFA, jipeni moyo mazoba! Nadhani kuna midudu ya kiyahudi Tanzania isiyojua hata majukumu ya ICC
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemshitaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete. Anaandika Josephat Isango.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mchana ukumbi wa Kisenga uliopo Millenium Tower, wakili wa Chadema, John Mallya amesema Kikwete ameshitakiwa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Mahakama ya kihalifu Uholanzi kwa sababu anatumia madaraka yake vibaya kutisha wananchi kuelekea uchaguzi mkuu.
Mallya alisema kuwa Mashitaka hayo yameelekezwa Umoja wa Mataifa lakini pia nakala za tuhuma dhidi ya Kikwete zimepelekwa pia Umoja wa Afrika (AU) na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita iliyopo The Hegue Uholanzi.
Kwa mujibu wa wakili huyo wa Chadema, barua hiyo ya tuhuma dhidi ya Kikwete imesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Prof. Abdallah Safari.
Mashataka haya yanakuja ikiwa ni miezi miwili tangu Rais Kikwete kuilamu Mahakama hiyo ya kihalifu kwa kusema kuwa viongozi wa Afrika hawafurahii kwa namna ambavyo mahakama hiyo inavyofanya kazi zake kwa kuwashughulikia zaidi viongozi wa mataifa ya Afrika.
Kauli hiyo ya Rais Kikwete aliitoa jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa 16 wa Umoja wa Wanasheria wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini mwa Afrika-SADC,
Hiyo ilikuwa ni siku tu moja baada ya ICC kueleza kwamba inafuatilia mwenendo wa uchaguzi nchini Tanzania.
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda, alikaririwa na vyombo vya habari vya Aljazeera na Gambia Today akisema kuwa Mahakama hiyo inatazama kwa umakini mkubwa yanayotokea Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu kama ilivyofanya katika nchi za Kenya, Ivory Coast na Congo na kwamba itachukua hatua za haraka kama kutakuwa na uvunjaji wa haki za binadamu.
Kauli hiyo ya Bensouda ilitanguliwa na ile iliyotolewa na mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.
Lowassa alilazimika kusema hayo katika ziara ya kutafuta wadhamini katika mikoa ya Arusha na Mwanza, Lowassa akilitahadharisha Jeshi la Polisi juu ya uwepo wa Mahakama ya ICC kutokana na kitendo chake cha kutumia nguvu dhidi ya wapinzani kwa kuupiga mabomu msafara wake.
Porojo nyingi sana chadema, ukishaona watu wanaacha taaluma zao na kuwa wanasiasa, ni balaa tupu, hawa chadema mwaka 2010 hawakuwa wanajua hizo mahakama ziko wapi? acha kwanza tumchague Makufuli alafu wao waendelee na porojo zao, kwani hizo ndo nyimbo za Mbowe na wafuasi wake.
Ashtakiwe tu maana huyu kikwete na monges wameifilisi nchi kwa kuigeuza kama ndio geto lao la kufanyia upumbavu
Na safari hii watakoma ubishi, na baada ya uchaguzi na vyama vyao vitakuwa vimefika mwisho, hivi wanadhani ICC ni mazuzu au wanadhani pia ICC ni wanasiasa, kwanza Mbowe na Lowasa ndo wanavunja sheria kimsingi ndo wanatakiwa kushitakiwa, wao ndo wanavunja sheria za tume kwa kuwambia vijana wasiondoke vituon baada ya kupiga kura.
Utatokwa povu sana. Safari hii jiandae kisaikolojia tu maana hamna namna nyingine isipokuwa ccm kuwa chama pinzani.
Mmezoea kuiba ndio maana mnasema hamna kulinda kura... Kura tutapiga na kuzilinda tutazilinda maana ni zetu
HAPA KAZI TU DKT MAGUFULI NDO RAIS WETU JMT