Rais Joe Biden ajikwaa mara mbili na kudondoka akijaribu kupanda ndege maalumu ya Air Force One

Rais Joe Biden ajikwaa mara mbili na kudondoka akijaribu kupanda ndege maalumu ya Air Force One

Mbwe mbwe za kupanda ngazi. Kama anajijua vizuri si apande taratibu kama hayati BEN MKAPA alivyokuwa anafanya au kibabu PAUL BIYA cha Cameroon
 
Ingekuwa ni hapa kwetu hiyo habari ingefanywa siri kubwa na angeweza kutokea waziri na kusema hilo jambo sio la kweli bali ni uvumi wa maadui zetu wa kiuchumi. Kweli nchi hii ndani ya hii miaka mitano na nusu tuligeuzwa mazuzu.
Na huyo Nyani Ngabu aliyeweka hiyo Video angekua kashakamatwa Kwa kusambaza taarifa za uzushi na uchocheza na taharuki na jinai.
Halafu mawaziri kama watatu hivi akiwemo wa ma telephone, wa criminal law na wa polisi wangetoa matamko mbali mbali tofauti kuwatisha watu
kuacha mara moya kumdhihakii Raisi.
Vyombo kadhaa vya habari vingefungiwa Kwa kutoa taarifa hiyo.

conclusion: Uzuri viongizi wanaenda na mdundo wa raisi. Naamini mama Samia Hassan Suluhu ataongoza kama mama so wale wa akina ma-Babalevo na ma-mamaLevo watapoa na kutahayari utadhani sio wao KMMK.
 
Ingekuwa ni hapa kwetu hiyo habari ingefanywa siri kubwa na angeweza kutokea waziri na kusema hilo jambo sio la kweli bali ni uvumi wa maadui zetu wa kiuchumi. Kweli nchi hii ndani ya hii miaka mitano na nusu tuligeuzwa mazuzu.
mungu wa Tanzania hajikwai, haumwi na hawezi kufa yeye ni jiwe.

Au nasema uongo Ndugu zangu..
 
Sasa kitu cha ajabu ni nini hapo?
Ni kawaida mtu akiwa kwenye uchovu kujikwaa
Mbaya zaidi mzee wa zaidi ya miaka 70 anajikwaa kijana anachekelea
Mbadilike
 
Back
Top Bottom