Rais Kagame ataka M23 watambuliwe na Serikali ya DR Congo

Rais Kagame ataka M23 watambuliwe na Serikali ya DR Congo

Serikali ya DRC itawezaje kuwatambua Banyamulenge wakati wako na silaha mkononi, huku wakipigana kutaka kuipindua serikali halali ya DRC?
hiki kikao cha leo ndo kimewahalisha wanyamurenge kuwa sasa nao ni wananchi halali kabisa wa drc maana hadi wametajwa kabisa kwenye makubaliano ya kikao na tshisekedi kaagizwa akae nao na awasikilize.

drc kwishnei. na hiki ndo alichokuwa anakitafuta PK sikuzote hizi. kikao cha leo ni pigo kubwa sana kwa tshisekedi na jamaa zake wa drc. haya maazimio ya leo hayatekelezi kwa tshisekedi. ni back to square one vita itaendelea.
 
Kagame kaongea ukweli mtupu

Hatuwezi kupotezeana muda wa mavikao yasiyo na tija kila siku wakati tatizo linajulikana.
Tatizo lenyewe sasa ni yeye Kagame. Suluhishio ni SADC-EAC kuwapa kipigo M23 kisha kutengeneza Buffer Zone katika mpaka wa Rwanda.
Au wawafurushe hadi Rwanda ndani kabisa ili Rwanda wapate joto la vita
 
Kagame ameleta msimamo wa M 23 kuwa watambulike na congo DR, sijui ni kivipi serikali ya Congo haiwatambui Wanyamulenge?

RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, amesema nchi yake haiwezi kukaa kimya wakati usalama wake unahatarishwa na DRC na kubainisha kuwa Rwanda imejaribu mara nyingi kuzungumza na Congo bila mafanikio huku akisisitiza kuwa suluhisho la kudumu linahitajika badala ya lawama zinazoelekezwa kwa Rwanda kila tatizo linapotokea DRC.

"Congo hawawezi kutuambia tukae kimya wakati wanasababisha matatizo makubwa ya kiusalama dhidi yetu, hakuna wa kutuambia tukae kimya, tumeongea na Congo mara nyingi tumewaita tukae tuongee hawataki, Mimi naomba tusiwe na vikao vingi sana kama ambavyo tayari tumeshakuwa navyo.” — amesema Kagame akizungumza kwenye mkutano wa EAC-SADC.

“Hatuwezi kila siku kukaa kujadili matatizo maana kinachoendelea pale ni vita ya Kikabila ni suala la kutambuana, kujadiliana na kuwapa haki yao, tutumie kikao hiki kupata suluhu ya kudumu na sio matatizo yatokee Congo kisha ubaya anapewa Rwanda" — amesema Kagame.
Bila kufanya hivyo nini itakuwa suluhu?
 
Hapo aliposema vita ya kikabila yuposahih. Nkweli ni vita ya kikabila. Ila kuhusu congo kukaa na m23 amebugi, kwani yeye kama nani mpaka congo wakubali anachotaka?.
Kwanin hafikilii ugumu au hatari anayoipata kukaa meza moja na FDLR?badala yake anaona ni rahisi kwa congo kukaa na m23?.
Sema jambo zuri ni kwamba ameeleweka vizuri sana.
We nae hueleweki kama kagame
 
Naye akaae chini na waasi wa kihutu wamalize tofauti.
Dawa ya Kagame ni kumchapa tu, naamini zikiungana nchi tatu au nne hatoboi.

Hao wanyamulenge anataka wapewe haki gani?

Wanyamulenge ni watusi wanaokaa DRC kinyemela, vipi wapewe haki?

Huyu Kagame ni mpuuzi, anaongea kana kwamba yeye ndiyo msemaji wa M23?
 
Kagame ameleta msimamo wa M 23 kuwa watambulike na congo DR, sijui ni kivipi serikali ya Congo haiwatambui Wanyamulenge?

RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, amesema nchi yake haiwezi kukaa kimya wakati usalama wake unahatarishwa na DRC na kubainisha kuwa Rwanda imejaribu mara nyingi kuzungumza na Congo bila mafanikio huku akisisitiza kuwa suluhisho la kudumu linahitajika badala ya lawama zinazoelekezwa kwa Rwanda kila tatizo linapotokea DRC.

"Congo hawawezi kutuambia tukae kimya wakati wanasababisha matatizo makubwa ya kiusalama dhidi yetu, hakuna wa kutuambia tukae kimya, tumeongea na Congo mara nyingi tumewaita tukae tuongee hawataki, Mimi naomba tusiwe na vikao vingi sana kama ambavyo tayari tumeshakuwa navyo.” — amesema Kagame akizungumza kwenye mkutano wa EAC-SADC.

“Hatuwezi kila siku kukaa kujadili matatizo maana kinachoendelea pale ni vita ya Kikabila ni suala la kutambuana, kujadiliana na kuwapa haki yao, tutumie kikao hiki kupata suluhu ya kudumu na sio matatizo yatokee Congo kisha ubaya anapewa Rwanda" — amesema Kagame.
Na yeye awatambue wahutu waliokimbilia uhamishoni
 
PK ameimaliza kazi yake jana pale dar. M23 wameshatambuliwa rasmi na T'Kedi kaagizwa akakae nao wakubaliane. kitachofata apo M23 wanapewa Kivu. PK ataitawala Kivu kwa mgongo wa hao M23.
Huyo Shekedi atakuwa anaumwa, unakubali kuwapa waasi nchi kwa sababu gani?

Hizo vita huwa zinapiganwa hadi tone la mwisho.

Tshekedi ashauriwe, aache huo upumbavu.
 
Huyo Shekedi atakuwa anaumwa, unakubali kuwapa waasi nchi kwa sababu gani?

Hizo vita huwa zinapiganwa hadi tone la mwisho.

Tshekedi ashauriwe, aache huo upumbavu.
mkuu umeisoma komunikee ya jana? itafute uisome km bado ipo humu.
 
Na yeye awatambue wahutu waliokimbilia uhamishoni
Kwake kuna Vita kwani ? Congo wanazingua wenyewe na ilo jimbo heri liwe chini ya utawala mwingine kuwe na amani, wao wameshindwa kuilinda ,
 
Back
Top Bottom