Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
adi wanafikia maazimio kuwa T'kedi akutane na m23 maana yake drc imeshawatambua ao wanyamulenge kama ni wananchi halali wa drc. nje ya apo maazimio yangekuwa m23 kuondoshwa apo drc.Serikali ya Dr congo lazima ikiri hadharani kuwa banyamulenge ni raia wa nchi hiyo na siyo wahamiaji
Mrusi anajinyea huko Ukraine aje kwenye vita ya manyaniKatika wajinga kongo ndio hovyo kabisa,weka Mrusi mpe anachotaka kagame ataongea lugha zote,angalia mfaransa alichofanywa Afrika Magharibi
Hahahaha Tena mbwa kabisaHuyu mtu ni mnafiki sana, Kikwete akimshauri akae na wahutu wakimbizi waliopo kongo alikataa,kwa matusi na vitisho! Mbwa sana huyu
Kagame ameleta msimamo wa M 23 kuwa watambulike na congo DR, sijui ni kivipi serikali ya Congo haiwatambui Wanyamulenge?
RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, amesema nchi yake haiwezi kukaa kimya wakati usalama wake unahatarishwa na DRC na kubainisha kuwa Rwanda imejaribu mara nyingi kuzungumza na Congo bila mafanikio huku akisisitiza kuwa suluhisho la kudumu linahitajika badala ya lawama zinazoelekezwa kwa Rwanda kila tatizo linapotokea DRC.
"Congo hawawezi kutuambia tukae kimya wakati wanasababisha matatizo makubwa ya kiusalama dhidi yetu, hakuna wa kutuambia tukae kimya, tumeongea na Congo mara nyingi tumewaita tukae tuongee hawataki, Mimi naomba tusiwe na vikao vingi sana kama ambavyo tayari tumeshakuwa navyo.” — amesema Kagame akizungumza kwenye mkutano wa EAC-SADC.
“Hatuwezi kila siku kukaa kujadili matatizo maana kinachoendelea pale ni vita ya Kikabila ni suala la kutambuana, kujadiliana na kuwapa haki yao, tutumie kikao hiki kupata suluhu ya kudumu na sio matatizo yatokee Congo kisha ubaya anapewa Rwanda" — amesema Kagame.
mkuu usiwakandie sana jamaa wanatupa burdani sana (mambo ya myuziki) kwa miaka dahari sasa! kwanza apa ushanikumbusha fally Ooh Mayday🎵🎷🎼 Mayday 🎵🎼Mayday!🎷🎷🔥🔥Katika wajinga kongo ndio hovyo kabisa
Walishaambiwa siku nyingi,wafanye kazi za kiraia, ujasiriamali, kilimo,madini,wao wanang'ang'ania kwenye vyombo vya ulinzi na usalama,Wana agenda gani!?PK yupo sahihi
Hakuna namna ya kuwakwepa M23 kwenye hoja ya kuleta amani
Ni kweli wanaweza kuwa na mapungufu yao lakini pia wana haki zao za msingi ziheshimiwe
Sijaipata mkuu, kama umeisoma nipe key points.mkuu umeisoma komunikee ya jana? itafute uisome km bado ipo humu.
Yaani Kagame anataka wanajeshi wake hao M23 wawe sehemu ya jeshi la DRC?Walishaambiwa siku nyingi,wafanye kazi za kiraia, ujasiriamali, kilimo,madini,wao wanang'ang'ania kwenye vyombo vya ulinzi na usalama,Wana agenda gani!?
Una hoja nzuriRais wa Congo sidhani kama atakubali. Tatizo Kongo hawana umoja, suluhisho la hii vita au mgogoro ni mmoja ashindwe, ni aidha congo wakubali kuwatambua m23 na Rwanda waichukue east congo Kwa mgongo wa m23 au congo akubali kuivamia Rwanda au kutangaza rasmi wanaingia vitani na nchi ya Rwanda (hapa gharama kubwa italipwa)....Sioni mazungumzo yakisaidia hapo.
Kuruhusu m23 kukubaliwa ni sawa na kuruhusu jeshi la Rwanda liingie Kongo kitu ambacho mtu mwenye akili timamu hawezi kukubali, kukubaliana na waasi waache silaha zao ni haiwezekani.
Dili na kiini cha tatizo, then m23 watapukutika wenyewe, kudili na kiini cha tatizo Kuna gharama kubwa mnooo za kulipa na congo haitaki kulipa hizo gharama, kwanini maliasili zote hizo mshindwe kununua vyuma vya kijeshi vya maana kabisa, tia pesa watu wakapate mafunzo ya kutosha ya kijeshi, jipe muda then Fanya kweli.
Ana shida yuleYaani Kagame anataka wanajeshi wake hao M23 wawe sehemu ya jeshi la DRC?
Ni mwendawazimu tu anaeweza kukubali hili.