Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 12,599
- 26,263
Mkuu ukiangalia kwa jicho la Tatu utagundua mipaka iko wazi kabisa kwa sababu dunia ya leo watu wanaiba kwa kutumia kalamu , watu wanatumia akili, sisi tunapumbazwa na maneno ya kitapeli tu utasikia mara Diplomasia Mara uwekezaji, hiyo yote ni wizi tu.
Wenzetu siasa zao wanafanya kisayansi na kutumia hesabu kali ila sisi tumekalia porojo tu. Hivi unajua kuna ndege binafsi zinatua direct huko migodini na mbugani? Unajua zinabeba mali kiasi gani? Unajua mwelekeo wa dunia kwenye matumizi ya Nishati ya Gesi? Unajua sisi tuna huge deposit ya Gesi ila hatuwezi kunufaika ipasavyo? Jeshi badala ya kulinda rasilimali za nchi linatumika kulinda maslahi ya watu wachache na kuizanisha nchi.
Shtuka mkuu dunia ya sasa haipigani vita kwa mitutu na mabomu bali kwa maneno, kalamu, akili kubwa na mahesabu makali.
Malawi, tunayoipa msaada, inafanya nini kati ya hayo?