Rais Kamuzu Banda alizitaka Mbeya, Njombe na Songea kuwa sehemu ya Malawi


Malawi, tunayoipa msaada, inafanya nini kati ya hayo?
 
Sisi ambao tuko mipakani karibu na Malawi ikitokea tukapiga kura ya kuwa sehemu ya Malawi hatukatai.Malawi kunamifumo mizuri ya kielimu,kiuchumi , kibiashara na,kijamii kuliko Tanzania.

Uchumi gani? Mabeki tatu wote siku hizi kusini wanatoka Malawi. Shortage ya mafuta, chakula, umeme nk. Hamia Malawi usisubiri boarder dispute.
 
Tungekomaa na kwenye Dhahabu na Gesi yetu ingependeza sana !

Alisikika Mwamba mmoja akisema
“Tumepigwa “ 😳😱
Rest in peace JPM 🙏🙏

Dhahabu na gesi vimefanya nini? Kuna tatizo gani? Mnaibiwa? How? Wapi? Breakdown bila vague statements za vijiweni.
 
Hizii stori za kijiweni
 

Maeneo yote ya mipakani yapo hivyo dunia nzima. Unaweza sema hayo maeneo yaende Malawi na TZ inaweza sema maeneo ya Malawi yawe Tanzania sababu ya muingiliano. Mipaka ni imaginary lines, natural landmarks zilitumika kutengenesha nchi au mikoa au majimbo kwa nchi zingine ndo maana unaona mara nyingi mipaka ni mito, milima, maziwa na landmarks zingine. Watu wa mipakani wataendana tu duniani kote.
 
Mipaka ya ukoloni haikuangaliq setup ya makabila ya eneo husika. Ukienda kaskazini kuna masai wa Kenya na Tanzania, jaluo hivyo hivyo. Kusini utakuta Makonde wa Msumbiji na Tanzania. Yaani hivyo

Kwa kawaida mipaka haiangalii makabila bali landmarks hii ni duniani kote sio Africa tu. Ni kawaida watu wa mipakani kuendana sababu mipaka ni imaginary lines tu. Sehemu nyingi mipakani utakuta mito, milima, ziwa au any other natural landmark regardless ya watu wa upande mmoja na mwingine kuwa wamoja.
 
Kama Tanzania inaweza kutikiswa hata na Malawi basi sitakuwa tena na sababu ya kunivunia kuwa Mtanzania.Suala la kutamani sehemu ya nchi nyingine limekuwepo tangu kitambo na Mwalimu alionesha mfano wakati Mzee Idd alipoitamani sehemu ya Kagera, na Kamuzu alijionea mwenyewe kilichotokea wala hakuhadithiwa.Na kama kuna wa kuogopwa iwapo ataitamani sehemu ya jirani yake basi ni sisi Tanzania, na si Tanzania kumuogopa Malawi,Uganda,Zambia,Kenya,Uganda n.k.
 
Kuingia frontline kupigania mpaka ? 😅🤣 Mimi nitakua wa mwisho kuvaa hizo kombati. Nitavaa kombati kupigania amani na utulivu na sio mipaka. Mipaka ni mamno ya kipuuzi tu haya. Watu wanaoishi pande zote ni wale wale tu na tena wengine wana ndgu upande huu na ule.
 
Ziwa Victoria tumepigwa pini gani.
 
Eti Mpare wa Mbaga anunue kiwanja ufukweni?Wapare hawahawa ninaowajua?labda ufukwe wa ziwa Jipe.
 
Eti Mpare wa Mbaga anunue kiwanja ufukweni?Wapare hawahawa ninaowajua?labda ufukwe wa ziwa Jipe.
Mkuu, hujakutana na wapare wenye ukwasi? Kuna wapare kina mchome, mndeme, wagonja, msuya wapare wa ugweno wana ukwasi sana tu, sema tofauti yao na makabila kama watani zao kina mushi, kimaro, shao, temu wao hawajui kunyanyuana. Mchaga akifika sehemu akafanikiwa ni suala la muda tu atavuta wachaga wenzie ila wapare siwaoni wakifanya haya ndo maana wengi wanabaki choka mbaya.
 
Ni Watani zangu hao nawajua mimi nje ndani.Any way niko kiutani zaidi.
 
Reactions: Tsh
Huyo ni hayawani Tu. Malawi nchi masikin kweli kweli na imejaa walevi
 
Zamani Wakazi wengi wa Mbeya walikuwa wa kabila la Kingoni, ambalo pia linapatikana Malawi. Viongozi wengi wa Malawi wakiongozwa na Banda Waliona uhusiano wa karibu na Malawi kuliko Tanzania, na walitaka baadhi ya mikoa ya Tanzania iliyokaribu na Malawi kujiunga na nchi hiyo. JW wapo makini na mipaka yetu
 
Ingia mwenyewe front mimi naenda zangu ulaya kama mkumbizi wa vita mambo ya kuyapigania ma ccm siwezi mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…