Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
Kikwete hajaonyesha ukomavu wa kisiasa na kushindwa kujibu hoja badala yake kumshambulia Tundu Lissu kwa lugha za vijiwe kitu kisichokubalika kwa nafasi na heshima yake kama Rais. Lugha hii aliyotumia hapa chini katika nukuru pengine amehamasika na labda kuelekezwa namna ya kujibu kwa vile amezoea ya kuambiwa bila kufanyia utafiti kujiridhisha na kile anachoambiwa.
Kwa namna nyingine lugha aliyotumia si ya kiwango chake na kwa nafasi yake na kabisa anapolihutubia taifa, amejiruhusu kushuka chini mno kiasi cha kutoa lugha isiyostahiki kwa jamii na pengine si kile kilichotazamiwa na watanzania walio wengi kusikia live toka kwake mwenyewe.
Kwenye kumbukumbu zangu zimetokea lugha za vijiweni toka Kurugenzi ya Habari Ikulu inapotoa matamko ya utetezi mara kadhaa, na lugha hizo zilizotumika hazitofautiani sana na hii ambayo Kikwete ameitoa safari hii kwenye hotuba yake ya Mwisho wa Mwezi alipoamua kumtolea uvivu Mbunge na Mnazimu Bungeni Tundu Lissu.
"... Mheshimiwa Tundu Lissu alitoa maoni yake."
"Siyo tu kauli ya Mheshimiwa Tundu Lissu ni uzushi na uongo mtupu, bali pia ni ya unafiki, fitina na uzandiki wa hali ya juu."
"... (K)wa Mheshimiwa Tundu Lissu kudai kuwa mapendekezo ya TEC na CCT hayakuheshimiwa ni uongo wa mchana usiokuwa na kichwa wala miguu."
"Kama ni kwa sababu za Mheshimiwa Tundu Lissu nimeshasema hazina ukweli wowote."
Kama nilivyoainisha mara moja kuhusu Dr Slaa katika mada mojawapo hapa juu kuhusu kupima lugha ambayo inatakiwa kama kiongozi mwenye nafasi kubwa kitaifa kutuliza kichwa na kutoa kitu ambacho kinaonekana hekima, busara na uvumilivu kuwepo.
Hivyo basi Kikwete naye kama rais wa nchi hii kauli aliyotoa hailingani na nafasi, wajibu, hekima na busara kwa nafasi aliyo nayo na wakati alipoitoa. Kwa nchi zilizopaa kidemokrasia hiyo lugha ingekuwa gumzo kubwa na pengine kuwa ni kashfa kitaifa, lakini kwa kuwa tumezoea basi tunaendelea na mazoea.
Sehemu ya majibu ya Tundu Lissu kwa kauli ya Kikwete:
Kuhusu uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nilisema yafuatayo: "... Uteuzi wa Wajumbe wa Tume uliofanywa na Rais na ambao unatumiwa Kama mfano (wa kuteua Wajumbe 166 wa Bunge Maalum) wenyewe ulikuwa na walakini kubwa. Katika hili, kuna ushahidi wa Wawakilishi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) na asasi mbali mbali za kiraia zikiwemo za walemavu waliowasilisha maoni ya taasisi zao kwa Kamati juu ya Muswada huu. Wawakilishi hao waliiambia Kamati kwamba ijapokuwa waliandikiwa na Rais kuwasilisha majina ya Wajumbe wao kwa ajili ya kuteuliwa kwenye Tume, na walifanya hivyo, hakuna hata moja ya majina waliyopendekeza aliyeteuliwa na Rais kuwa Mjumbe wa Tume. Badala yake, Rais aliteua watu aliowaona yeye na washauri wake wanafaa. Kama taarifa za wadau hawa ni za kweli maana yake ni kwamba Rais na Mwenyekiti huyu wa CCM Taifa hawezi kuaminika tena kuteua Wajumbe halisi wa taasisi hizi katika Bunge Maalum...."
To wind up, Kamati ilitengeneza orodha ya taasisi na watu binafsi wa Zanzibar ambao ilitaka kupata maoni yao. Hatukuonana na hata mmoja wa taasisi na watu binafsi hao kwa sababu Kamati haikuruhusiwa kwenda Zanzibar. Aidha, Kamati haikukutana na mwakilishi hata mmoja wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Pili, Wawakilishi wa TEC (Father Dr. Charles Kitima), CCT (Mchungaji Rohho) na wa SHIVYAWATA (nimemsahau jina) ndio walioiambia Kamati kwamba mapendekezo yao hayakuheshimiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Tume. Mimi sikuyatoa uchochoroni, yalisemwa hadharani mbele ya Kamati!
Sasa kama ni uongo, fitina, uzandiki na mapambo ya aina hiyo aliyonipamba nayo Rais, basi ninakiri kuwa I'm guilty as charged!!!
Tundu