Rais kateleza kutumia lugha za vijiweni kutetea Katiba - Matamko Kurugenzi Ikulu yafanana

Rais kateleza kutumia lugha za vijiweni kutetea Katiba - Matamko Kurugenzi Ikulu yafanana

Kweli katika hotuba ya rais hakuna mahali alipoonyesha wazi uongo wa Lisu juu ya kutoheshimiwa kwa maoni ya TEC, CCT, na wengine. Nilitegemea rais aseme hivi (ilikudhibitisha uongo wa Lisu), ...."TEC, CCT, n.k walipendekeza hivi na wakatoa majina haya..nami mimi kama rais kwa fursa niliyonayo ni chagua majina haya kutoka kwenye orodha zao..." hiki kitu hakikuonyeshwa na rais...katika maelezo yake. Labda kama kuna aliyekiona/ sikia katika hotuba yake anaijuze
 
"unafiki, fitina na uzandiki" ni lugha za mitaa gani? au kiswahili kinawasumbua? Hoja hapa ni huyu bwana Tundu Linsu ambaye ana sifa hizi mbaya sana! yahani ni mtu ambaye hatuwezi kumwani tena na hawezi kupewa mamlaka ya kuwa kiongozi katika nchi hii kwa sifa chafu kama hizo.

subiri mtu aongee bungeni kama hajaambiwa afute kauli
JK aliitwa dhaifu mnyika akala ban,,,sasa dhaifu na zandiki,utacompare na kucontrast wewe
 
Hilo la kujichanganya imemtokea mara nyingi....

Kuna wakati alitoa tamko eti yale majengo ya Wakandarasi pale Jangwani yavunjwe ili kuwapa ruhusa vijana kufanya mazoezi nyakati za jioni...

Baadaye akaja kuambiwa wale ni Wakandarasi na wapo kwenye maandalizi ya Ujenzi wa Kituo cha Mabasi ya Kasi...

Imagine aibu kama hiyo mkuu!!!

bora asiwe na wasaidizi sasa
 
Zamani enzi hizo ukisikia redioni ni 'rais amesema' na wote mnaogopa na kusubiri utekelezaji.
Leo hii unasikia redio hizo hizo (japo sio za mbao kama enzi hizo) zikisema 'nimeambiwa', 'nimesikia'. Hata alivyokuja Bukoba 'akaagiza' Meya na Mbunge wamalize matatizo yao hakuna kilicho fanyika hadi leo (Ta Muganyizi twambie kama kipo). Taratibu utaanza kukubaliana na Mwalimu anaposema wengine ni 'wadogo'.
Tumuombee rais wetu jamani maana inaelekea kutawala nchi sio kazi ndogo kama kuwa katibu kata.
 
Kweli katika hotuba ya rais hakuna mahali alipoonyesha wazi uongo wa Lisu juu ya kutoheshimiwa kwa maoni ya TEC, CCT, na wengine. Nilitegemea rais aseme hivi (ilikudhibitisha uongo wa Lisu), ...."TEC, CCT, n.k walipendekeza hivi na wakatoa majina haya..nami mimi kama rais kwa fursa niliyonayo ni chagua majina haya kutoka kwenye orodha zao..." hiki kitu hakikuonyeshwa na rais...katika maelezo yake. Labda kama kuna aliyekiona/ sikia katika hotuba yake anaijuze

Kwa vile Rais Kikwete hakuweza kujibu hoja yake ila mipasho na matusi, ndio maana Tundu Lisu amekuja na majibu haya kuyaweka hadharani kubainisha hoja yake ambayo Rais alishindwa kubainisha kwa hoja uwongo na uzandiki wa Lissu ila mnipasho yake aliyozoea bila kujua mazingira na nafasi gani angeweza kuleta mipasho ile si katika nafasi ya hotuba rasmi.

To wind up, Kamati ilitengeneza orodha ya taasisi na watu binafsi wa Zanzibar ambao ilitaka kupata maoni yao. Hatukuonana na hata mmoja wa taasisi na watu binafsi hao kwa sababu Kamati haikuruhusiwa kwenda Zanzibar. Aidha, Kamati haikukutana na mwakilishi hata mmoja wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Pili, Wawakilishi wa TEC (Father Dr. Charles Kitima), CCT (Mchungaji Rohho) na wa SHIVYAWATA (nimemsahau jina) ndio walioiambia Kamati kwamba mapendekezo yao hayakuheshimiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Tume. Mimi sikuyatoa uchochoroni, yalisemwa hadharani mbele ya Kamati!

Hapa Kikwete anaonekana kutomfahamu vizuri Tundu Lissu, sasa mwenzake ameanika ukweli ili Kikwete aufanyie kazi ili kuondoa udhia ambao awali Lissu hakuuweka kwa uwazi.
 
Hilo la kujichanganya imemtokea mara nyingi....

Kuna wakati alitoa tamko eti yale majengo ya Wakandarasi pale Jangwani yavunjwe ili kuwapa ruhusa vijana kufanya mazoezi nyakati za jioni...

Baadaye akaja kuambiwa wale ni Wakandarasi na wapo kwenye maandalizi ya Ujenzi wa Kituo cha Mabasi ya Kasi...

Imagine aibu kama hiyo mkuu!!!

me napna bora asiwe na wasaidizi
 
wew anatetea ujinga kabisa.
Tunajua ameshasaini na Ikulu wanakanusha kitu kilichowazi hadi wakadiriki kuandika raisi atasaini
Ataonja joto ya jiwe ndio mtajua kama katiba ni ya CCM au ni ya wananchi wote.
Tunajua maCCM yanabaka katiba mpya kwa vile haikuwa katika ilani yenu
Lakini wananchi ndio wana ufunguo wa mwisho.
2015 hakuna kuiba kura vituoni mjiandae kuondoka
Unaposema JK sio saizi yeti kachaguliwa na nani?
kama alipata kura miliion 5 kwa nchi yenye watu Million 40 unategemea huyo atakuwa rais wa watu gani?
THINK FURTHER.

Wewe unaendeshwa na nani kwa tarifa yako jana kasaini mtapasuka mwaka huu,
hizi chuki zenu wala hazimstui wewe ungeuza kalanga na mwezako auze mandazi lakini jk siyo saizi yenu.
 
na hotuba nzuri ni inayotoka kichwani, mbona mnamtetea sana LISSU.
sawa,ila mimi sijamtetea LISSU bali nimeshangazwa na style ya majibu na matumizi ya maneno mheshimiwa Rais aliyotumia.
 
Umeeleweka kiongozi. Jk hajijui kama yeye ndo Mkuu.............ananjihisi hisi na kuwa na inferiority compl............

Kama anatoa lugha za kihuni na za mtaani kwa viongozi wa siasa na yy ni rais kwann huwa wabunge ccm wanalia na kulalamika kuwa wapinzani wanatumia lugha ya kumchafua rais,,,ukinyea kikombe jua na wewe kuna siku watakunyea,,,JK awe makinni na kauli zake lasivyo atakuwa rais kichekesho,,,
 
Wewe ulitaka mtu mnafiki amwambiaje zaidi ya kumwambia ukweli wake jk kafanya haki mnafikinlazima lazima ambiwe ukweli lisu kazidi unafiki na umbea.
Kuhusu uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nilisema yafuatayo: "... Uteuzi wa Wajumbe wa Tume uliofanywa na Rais na ambao unatumiwa Kama mfano (wa kuteua Wajumbe 166 wa Bunge Maalum) wenyewe ulikuwa na walakini kubwa. Katika hili, kuna ushahidi wa Wawakilishi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) na asasi mbali mbali za kiraia zikiwemo za walemavu waliowasilisha maoni ya taasisi zao kwa Kamati juu ya Muswada huu. Wawakilishi hao waliiambia Kamati kwamba ijapokuwa waliandikiwa na Rais kuwasilisha majina ya Wajumbe wao kwa ajili ya kuteuliwa kwenye Tume, na walifanya hivyo, hakuna hata moja ya majina waliyopendekeza aliyeteuliwa na Rais kuwa Mjumbe wa Tume. Badala yake, Rais aliteua watu aliowaona yeye na washauri wake wanafaa. Kama taarifa za wadau hawa ni za kweli maana yake ni kwamba Rais na Mwenyekiti huyu wa CCM Taifa hawezi kuaminika tena kuteua Wajumbe halisi wa taasisi hizi katika Bunge Maalum...."

To wind up, Kamati ilitengeneza orodha ya taasisi na watu binafsi wa Zanzibar ambao ilitaka kupata maoni yao. Hatukuonana na hata mmoja wa taasisi na watu binafsi hao kwa sababu Kamati haikuruhusiwa kwenda Zanzibar. Aidha, Kamati haikukutana na mwakilishi hata mmoja wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Pili, Wawakilishi wa TEC (Father Dr. Charles Kitima), CCT (Mchungaji Rohho) na wa SHIVYAWATA (nimemsahau jina) ndio walioiambia Kamati kwamba mapendekezo yao hayakuheshimiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Tume. Mimi sikuyatoa uchochoroni, yalisemwa hadharani mbele ya Kamati!

Sasa kama ni uongo, fitina, uzandiki na mapambo ya aina hiyo aliyonipamba nayo Rais, basi ninakiri kuwa I'm guilty as charged!!!

Tundu
 
I am proud, and very proud indeed because I did not waste my vote in voting for the current president of the URT. I share my observation with that of Hon. Mnyika, JJ that Mr. JK is "The weakest president the country has ever had since its independence".
 
Ni Majina gani TEC waliwasilisha kwa ajili ya Uteuzi kwenye Tume?

Ni Majina gani CCT waliwasilisha kwa ajili ya uteuzi kwenye Tume?

Yes.....kama hayo yaliyonukuliwa hapo juu yamesemwa na Lisu basi atakuwa mjinga wa kupitiliza. Kamati inaambiwa, bila kuhoji vizuri unakwenda kulalamika tu kama Mwandishi wa habari.

Kikwete anasema, baada ya majina ya vyama vikuu vya Siasa.....akachukuwa ya Taasisi za Dini....TEC, CCT, BAKWATA....

Lisu angemuumbua JK kama angesema......TEC na CCT walipeleka majina haya.............na kati hayo hakuna hata moja lililopitishwa.

Maneno mengi hupunguza hekima.

Kweli ndege mjanja hanaswa kwenye tundu bovu!

Aibu kwa Lisu.
 
Back
Top Bottom