Rais kateleza kutumia lugha za vijiweni kutetea Katiba - Matamko Kurugenzi Ikulu yafanana

Rais kateleza kutumia lugha za vijiweni kutetea Katiba - Matamko Kurugenzi Ikulu yafanana

Mkuu utakuwa umevurugwa pakubwa kwa hapa tanzania hakuna kiongozi hata mmoja mwenye uwezo kama jk wa kuchambua mbaswala.

hizi data za kusema jk alikwepa mdahalo ni za uongo na unafiki kama wa lisu hakijawahi kutokea kitu kama hicho slaa mwenyewe akimuona jk nguo zinabana anatafuta pakutokea.

Hivi lugha za matusi na kupigana kunakofanywa na biongozi wa chadema unaweza kulinganisha na hotuba mwanana aliyotoa jk.

Ni kweli JK ni bingwa wa kuchambua mbaswala na sio muswada/maswala ingawa ilibidi useme hoja. Biongozi ndio nini?

Tuliza presha mkuu. Haina haja ya kukurupuka, jipange kama kupigwa chini mtapingwa tu 2015 hata ukifanya nini...

Uzuri unajijua kama unalofanya halina faida hata kwa watoto zako ila njaa ndio tatizo chemba.
 
Sioni sababu ya kuendelea kujadiliana nawe wakati unatetea kitu kilicho wazi ambacho Kikwete na CCM walikataa kata kata midahalo uchaguzi Mkuu uliopita, nadhani kwa kauli yako ni kundi moja na taswira za kikwete ndio maana huoni aibu kutamka kitu kisicho na ukweli.

wewe sioni hoja yako ambayo inakufanya utoke povu kiasi hicho. CHADEMA wamepotoka sana na wanachokifanya sasa ni jitihada za kumsafisha Lissu
 
JK ni mzushi sana yeye ansema mambo ya kuambiwa,kwanini hakusikiliza hoja za upande wa pili?ndio atoe kauli yake hiyo?
 
Nimepata wakati mgumu kujobu maswali ya mwanangu wa kike darasa la Pili, alianza hivi:
Rais wetu ni Nani? Mimi Kikwete Tundu Lisu ni nani? Mini ni Mbunge na mwanasiasa pia mwanasheria? Mwanangu , mbona ameongezewa vyeo vingi wakati baba huna hata kimoja? mimi cheo kipi? amepewa Mnafiki, Mzandiki kingine nimekisahau, mimi hivyo vyeo sio nitakwambia baadaye kalale kwanza.
 
"unafiki, fitina na uzandiki" ni lugha za mitaa gani? au kiswahili kinawasumbua? Hoja hapa ni huyu bwana Tundu Linsu ambaye ana sifa hizi mbaya sana! yahani ni mtu ambaye hatuwezi kumwani tena na hawezi kupewa mamlaka ya kuwa kiongozi katika nchi hii kwa sifa chafu kama hizo.
 
Hapa lugha ya kijiweni iko wapi?
"... Mheshimiwa Tundu Lissu alitoa maoni yake."

"Siyo tu kauli ya Mheshimiwa Tundu Lissu ni uzushi na uongo mtupu, bali pia ni ya unafiki, fitina na uzandiki wa hali ya juu."

"... (K)wa Mheshimiwa Tundu Lissu kudai kuwa mapendekezo ya TEC na CCT hayakuheshimiwa ni uongo wa mchana usiokuwa na kichwa wala miguu."

"Kama ni kwa sababu za Mheshimiwa Tundu Lissu nimeshasema hazina ukweli wowote."
kwani Tindu Lissu siyo mzushi, mwongo na mnafiki?
 
exactly ila nahisi anayafikiria baada ya kuonekana kuna uwongo ambao alidanganywa,makumbuka wakat anakabidh ambulence aliwai kumkemea mtu hadharan na baadae ikadhihirika,hao watu wake walijikanyaga,,,,,

Hilo la kujichanganya imemtokea mara nyingi....

Kuna wakati alitoa tamko eti yale majengo ya Wakandarasi pale Jangwani yavunjwe ili kuwapa ruhusa vijana kufanya mazoezi nyakati za jioni...

Baadaye akaja kuambiwa wale ni Wakandarasi na wapo kwenye maandalizi ya Ujenzi wa Kituo cha Mabasi ya Kasi...

Imagine aibu kama hiyo mkuu!!!
 
"... (K)wa Mheshimiwa Tundu Lissu kudai kuwa mapendekezo ya TEC na CCT hayakuheshimiwa ni uongo wa mchana usiokuwa na kichwa wala miguu."

Inaelekea Tundu Lissu na TEC na CCT ni damdamu.
 
Rais anapaswa kuwa mwazi na mkweli kama anavyofanya JK. Tundu Lissu ni mtovu wa nidhamu, mzandiki, mnafiki, mwongo na mzushi

Mkuu ngoja nikujulishe jambo moja, lugha za "mzandiki, mnafiki, mwongo na mzushi" hazimaanishi ukweli na uwazi. Na vilevile sifurahishwi sana na mheshimiwa Tundu Lissu anavyopambana na Rais japo hoja zake ni za msingi.

Unapokua na wadhifa mkubwa kama wa JK lazima uangalie na uwe makini sana na maneno unayoyatumia.
 
niliwahi kusikia raisi kaenda kwenye mashindano ya mamisi sasa sidhani kama ntashangashwa na hizi kauli
 
Unakumbuka kipindi cha Kampeni uchaguzi Mkuu uliopita Kikwete alikimbia na kukataa kata kata kufanya debate na presidential candidates wenzake. Aliogopa udhaifu huu usijejulikana. Viongozi wa aina hii mara nyingi utaona wanakwepa sana maswali toka kwa waandishi na watu mbalimbali. Pia ikibidi wanaambiwa wapeleke maswali kabla wayaone na wakiona pagumu wanakwepa press conference kwa vile hawakosi visingizio.
Umenikumbusha mkuu.....Lazima tubadilike, sio kuwa na viongozi tusioweza kuwatofautisha na vijana na vijiweni. Lazima kiongozi awe na nidhamu ya uongozi na sio kuropoka kama mtoto mdogo.
 
yaani wana ccm wamekosa kabisa point za kumsapoti rais,ukisoma points zao unaona kabisa wanachoandika hakilingani kabisa na wanachofikiri,simiyu umebanwa hapo let it go,we have dot com president.
 
Hapa lugha ya kijiweni iko wapi?
"... Mheshimiwa Tundu Lissu alitoa maoni yake."

"Siyo tu kauli ya Mheshimiwa Tundu Lissu ni uzushi na uongo mtupu, bali pia ni ya unafiki, fitina na uzandiki wa hali ya juu."

"... (K)wa Mheshimiwa Tundu Lissu kudai kuwa mapendekezo ya TEC na CCT hayakuheshimiwa ni uongo wa mchana usiokuwa na kichwa wala miguu."

"Kama ni kwa sababu za Mheshimiwa Tundu Lissu nimeshasema hazina ukweli wowote."
kwani Tindu Lissu siyo mzushi, mwongo na mnafiki?

Mkuu, hapo jibu lipo wazi kabisa. Nashangaa kuona wafuasi wa CHADEMA wakimkingia kifua Lidu wakati kaongea maneno ya uongo na uzushi bungeni
 
Mkuu ngoja nikujulishe jambo moja, lugha za "mzandiki, mnafiki, mwongo na mzushi" hazimaanishi ukweli na uwazi. Na vilevile sifurahishwi sana na mheshimiwa Tundu Lissu anavyopambana na Rais japo hoja zake ni za msingi.

Unapokua na wadhifa mkubwa kama wa JK lazima uangalie na uwe makini sana na maneno unayoyatumia.

Nakuomba uchukue kamusi ya TUKI au waulize wanaojua ili wakuambie ni nini maana ya mzandiki, mnafiki, mwongo na mzushi. ukishapata tafsiri zake, linganisha hicho ulichokipata halafu uone kama Lisu hastahili kuitwa majina hayo
 
Kuna mambo mengine Marais wa Nchi huongea kwa kuwa wanajua hakuna mtu yoyote wa kuwafanya kitu chochote...

ni kutokana na dhana hiyo ndio maana wengine wamegeuka miungu watu ktk nchi zao.
 
Back
Top Bottom