Rais Kenyatta asaini muswada unaotaka Serikali kugawa pedi bure kwa wanafunzi wa kike

washa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2007
Posts
626
Reaction score
370
Rais Uhuru Kenyatta amesaini muswada ambao sasa utakuwa sheria kamili, inayoitaka serikali kugawa pedi bure kwa wanafunzi wa kike nchini humo.
Hapa kwetu ushauri kama huu ulipoletwa bungeni na Mh. Upendo, jamaa wale waliukunjakunja na kuutupilia mbali.
Hivi sisi tunatatizo gani ktk kupanga masuala yanayohusu ustawi wa watu wetu?...
 
Kenyata is simply destroying Kenya by expanding the size of entitlements programs.
 
Huku mngo wamefanya mradi ea kupiga mpaka clouds inasisitiza hioo michangoo
 
Aisee hii hatari sasa. Hivi Pedi ndilo hitaji la muhimu kwa wakenya? Kwanini asiwawezeshe wakenya waweze kununua pedi?
Yaani wakenya wanautoto fulani.
 
Nani ametuc mwingine
Hahahaha!! Nimesema uwezo wa wakenya kufikiri ni mdogo sana. Hivi pads ndicho kipaumbele cha msingi? Ndio maana Tanzania inasita kidogo kwenye hii EAC mpaka Kenya watakapopatikana viongozi wanaojali maisha ya waafrica.
Hiyo ni moja ya mradi wa kula pesa za serikali. Mtakuja kuambiwa kila mwezi serikali inatumia $1billion. Amkeni wakenya acheni kujinga.

 
Acha ujinga wewe mzee. Haya ni mambo madogo madogo ambayo yana impact kubwa kwa mwanafunzi wa kike. Suluhisho la mwanafunzi kukosa kufika shuleni limepatikana. Inamaanisha kwamba baadae ataweza kujikimu kimaisha kama ataaendelea kusoma bila hitilafu. Wewe mwanaume mzima mambo ya pedi yanakuwashia nini?
 
Badala ya kuwapa pads wapatieni chakula wale washibe. Hizo pads zina mbadala wake wanaweza wakatumia vitambaa. Lakini njaa haina baunsa.
 
Hili ndilo tatizo lenu wakenya, kutotumia utafiti katika kufikia maamuzi ya miradi ya serikali, kila mtu anasema vile mawazo yake yanavyomtuma, matokeo yake miradi mingi inayotekelezwa na serikali yenu inakuwa haifanyiki ipasavyo, au ni ghali sana, au sio kipaumbele. Jaribu kupanga vipaumbele vya primary education hapa Africa katika haya yafuatayo; vyumba vya madarasa, desks, vitabu, chakula, maji, umeme, laptops, nyumba za walimu, vifaa vya kufundishia, pedi za kike, na masilahi ya walimu.

Hivi mlishanya tafiti zozote zilizoonyesha kwamba pedi za kike zinachangia kwa % ngapi wa utoro wa wanafunzi?, hivi mnaweza kulinganisha na njaa?
 
Badala ya kuwapa pads wapatieni chakula wale washibe. Hizo pads zina mbadala wake wanaweza wakatumia vitambaa. Lakini njaa haina baunsa.
Nani amekuambia wako na njaa,
mkiona njaa turkana mnadhani ni kenya yote,stupid
 
Pads Always hunaga point
 
wewe ndio akili yako bado sana ,maana maadam wewe upo kwenye AC HUJUI ATHARI ZINAZOWAKABILI WASICHANA WETU WANAPOKUWA KWENYE MPs,sometimes tumia kichwa kufikiri sio miguu
 
wewe ndio akili yako bado sana ,maana maadam wewe upo kwenye AC HUJUI ATHARI ZINAZOWAKABILI WASICHANA WETU WANAPOKUWA KWENYE MPs,sometimes tumia kichwa kufikiri sio miguu
Kwani mimi nakataa kuwa wanakuwa na matatizo kipindi hicho? Lakini kweli hilo ndilo tatizo la msingi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…