Rais Kenyatta: Hatuwezi kuendelea na lockdown

Rais Kenyatta: Hatuwezi kuendelea na lockdown

It's no brainer that the more you increase on the number of tests, the possibilities of having an increased number of infected persons!..
What matters is the fact that, there is big number of new infections recorded daily, that needs measures to curb the spread need to be tightened not otherwise

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndio unasema vipimo vinakuja na maambukizi wala sio Mimi. Kukiwa na wale ambao washaa ambukizwa bila ya kupima utaona ni Kama hakuna maambukizi. Ukipima wachache, vilevile utapata idadi chache. Inamaanisha ukiongeza vipimo ndio uwezekano ya kunasa wengi wa waathiriwa.
Uganda wamepima watu wengi kuliko Kenya, mbona maambukizi ni machache?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maambukizi yameongezeka lakini sio kama vile hakungekuwa na hizo hatua zikizowekwa. Halafu ukumbuke idadi ya vipimo vimeongezwa hapo lazima idadi ya waathiriwa itaenda juu!..
Kuna uwezekano kweli maambukizi yameongezeka au vipimo fake vimeongeza idadi ya wagonjwa ambao ni wazima.
Screenshot_20200521-145855.png
 
- Rais alisema serikali imeafikia uamuzi wa kuwa haiwezi kuendelea kuwafungia watu

- Alisema sasa itafikia wakati wa watu wenyewe kujilinda dhidi ya maambukizi ya coronavirus

- Nchi jirani ya Tanzania ni mojawapo wa zile ambazo hazikufunga shughuli zake za kuchapa kazi kwa ajili ya covid-19

Rais Uhuru Kenyatta ameashiria huenda 'curfew' iliyowekwa ikafunguliwa baada ya kukamilika wiki ijayo siku 21 zilizowekwa zikikamilia.

"Tumeona sisi kama serikali kuwa hatuwezi kuendelea kuwa na lockdown . . . na 'curfew'. Sasa ni lazima Wakenya warudi kwenye makazi yao na shughuli zao," Rais alisema.

Rais alisema sasa nijukumu la Wakenya kuhakikisha kuwa maambukizi ya coronavirus yanakabiliwa wakati ambapo taifa litafunguliwa.

"Sasa kwa sababu hatuwezi kuendelea na kufunga, tukifungua, halafu ugonjwa huu uendelee ujue ni wewe, na mimi na Matiang'i kuhakikisha kuwa tunalinda kila mmoja," alisema Rais.

Rais Uhuru Kenyatta alisema serikali imeafikia uamuzi wa kuwa haiwezi kuendelea kuwafungia watu.

"Nimewaeleze hawa mawaziri, haswa wa Afya kuwa Wakenya sasa wajue ni wakati wa kulindana.

Wewe ukienda kazi ni wajibu wako kulinda mama na watoto, kama serikali zile zingine kila pahali hatuwezi kuendelea kufungia watu," aliongeza Rais.

Rais alisema hayo wakati ambapo idadi ya maambukizi imefikia watu 1192 na watu 50 kufariki.

Wakenya wamekuwa kwenye kafyu ya kutokuwa nje ifikapo saa moja usiku kwa siku 28.
Kaunti tano za Nairobi, Mombasa, Kwale, Kilifi na Mandera pia zilifungiwa kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi.
Mitaa ya Eastleigh Nairobi na ule wa Kale Mombasa pia ilifungwa na hakuna watu kuingia au kutoka.
Awakumbushe na kupiga ngungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom