Rais Kikwete akanusha kumuokoa Ridhiwani katika kesi ya dawa za kulevya China

Rais Kikwete akanusha kumuokoa Ridhiwani katika kesi ya dawa za kulevya China

Ila kwa kutetea tu nakuaminia, tatizo tu ni kuwa uko biased, hoja ikitolewa inayohusu upande flani unatamani uwaaminishe watanzania wote uongo wako, bila shaka wanakulipa vizuri. Congr....
Hakika Mkuu. Wananilipa vema sana. Buku saba per post si hela ndogo
 
Toka 2012 leo 2014 ndio wanakanusha?
 
......``Haya ni maneno ya kipuuzi.....ni kuota jinsi ya kuyumbisha ajenda yetu ambayo imefanikiwa sana katika kubadilisha hali ya maisha ya Watanzania"_ jamani, ni maisha yapi hayo yamebadilishwa?
 
Rais Kikwete akiwa Marekani ameongea na watanzania na kukanusha madai kuwa alimuokoa
mwanae Ridhiwani nchimi China baada ya kukutwa na dawa za kulevya.

Rais amesema huo ni upuuzi na hawezi kuongelea upuuzi wa aina hiyo ambao ni uzushi usio na maana.

JK pia amewaambia watanzania waishio marekani kuwa sio kweli kwamba kusainiwa mikataba 12 kati ya Tanzania na China ilikuwa ni sehemu ya masharti yaliyotolewa na China wakati wa kumuachia Ridhiwani.

Jakaya-Kikwete.jpg


=======================================

Kurugenzi ya habari ya Ikulu inapaswa kulaumiwa kwa kukaa kimya juu ya sakata hili huu wanaouita uzushi umesemwa muda mrefu sana ni zaidi ya mwaka na hakuna mtu wala taasisi iliyekanusha wananchi wanakosa imani na kurugenzi hii inapoamua kuona jambo kubwa kama hili na mengine kuwa ni dogo kwa kutolitolea ufafanuzi mapema
 
......``Haya ni maneno ya kipuuzi.....ni kuota jinsi ya kuyumbisha ajenda yetu ambayo imefanikiwa sana katika kubadilisha hali ya maisha ya Watanzania"_ jamani, ni maisha yapi hayo yamebadilishwa?
Yake pamoja na mafisadi. Si unakumbuka wale jamaa waliokwapua pesa za EPA walivyosameheana kimtindo? Sasa hivi anakula bata Marekani. Naona tujenge ikulu ndogo kule. Kila siku Marekani, hebu mara moja moja awe anakwenda Somalia na Palestina!
 
Hakukuwa na swali la Nyongeza juu ya list ya wauza unga, hasa baada ya kujua kwamba Riz1 alikuwamo?
 
Pamoja na yote hayo, Ikulu imeamua kutoa Press Release kwa ajili ya hiyo issue tu? Hamna vitu vingine vya maana alivyozungumzia?
 
Hivi kwa akili zetu kweli kabisa mtoto wa raisi aende kubeba unga kupeleka China?
Amekosa nini hicho hadi akabebe unga?
 
Huu upuuzi mi niliukataa toka mwanzo ni moja ya uzushi uliopikwa vizuri na kukubalika miongoni mwa watu even Great thinker
 
Maisha gani kayaborosha huyu JK?
Kiukweli kadri siku zinavyozidi kwenda mbele na uwongo wa Jk na ccm yake ndo maisha yetu watanzania yanazidi kuwa mabaya sana!!
Huku gesi yetu ameiweka rehani kwa wachina ili kumuokoa mwanae!!!
 
Back
Top Bottom