Rais Kikwete akifungua Hoteli Mpya ya Kitalii ya Bilila Lodge Kempinski

Du kweli viongozi tunao,kwanini sasa wasifute zile gharama za kuwahudumia mawaziri wakuu na maraisi wastaafu.kwani wote wanamudu maisha yao tena zaidi ya vijisenti vya serikali yetu, kweli wATU tuna ubinafsi
 
ukisha vuka ikoma Robanda'mbele kidogo mnapoacha Magari kuna kiberenge Maalum na zile Baloon za kuwapandisha kule hotelini,Mie nilifanya kazi pale kama kibarua enzi za ujenzi jamani Mahari pale ni kufuru' hii ndio Serengeti karibuni mjionee vya rais wetu.
 
Miusiku miwili itatugharimu dola ngapi mimi na baba chanja kama tutaenda kwa kujipongezea kumbukumbu ya miaka 15 ya ndoa?
 
Je, hawa ndio waliochukua na 77 Hotel pale Arusha kama godown yao?

"Nchi hujengwa na wenye moyo na huliwa na wenye meno"
 
inawezekana kwa sababu tangu inaanza kujengwa mh amekuwa karibu nayo sana, na safari nyingi zinaishia hapo. SOROI nayo yasemwa ni ya SHEIN je ukweli ukoje? Kama ni kweli basi uongozi wote wa juu wa chama chetu kitukufu cha nyinyiem ni mafisadi papa. jk-Bilila, Shein-Soroi, Mangula-Epa, Kinana-Pembe za Ndovu
 
Weka evidence na sio maneno tu, siku za nyuma hapa JF watu walikuwa wanaweka na ma evidence, siku hizi tofauti kabisa!
 
Soroi ni ya Shein ni muhindi mmoja anyemiliki kampuni ya ndege ya Zantasair na sio yule Rais wa Zanzibar kama unavyofikiria.
 
Buko hizo picha ni TZ au? nani mmiliki wake?
weka rodha hapa ili baada ya uchaguzi 2015 tujue ni wapi pa kuanzia kurudisha vilivoibwa
 
Lokissa kama hujui vitu kaa pembeni, mmiliki wa Bilila ni Ali Bawardy tycoon wa kiarabu. Hotel haijawahi kuwa chini ya Serena ila Kempinski walipewa kufanya management na sasa management wanafanya Four Seasons na si kwamba wameuziwa.

Kuhusu JK kuwa na shares siwezi kulizungumzia kwani sijaona Memorandum kuweza ku identify shareholders.
 
Bongo hii hakuna siri tena ndio sababu CDM ikichukua nchi watakimbilia Uswissi. Hosea na Mkuchika wanasema wapelekewe majina kumbe wanayo hawajui wataanzia wapi kuwataja. Usalama wa Taifa uko macho na kila mtanzania na upinzani ukichukua, wananchi tukae mkao wa kugawana mali za vigogo. Vitu vizuri vinatakiwa lakini kwa mgongo wa kuwanyima watoto wa wakulima elimu ya kusoma na kuandika. Inauma! Nape anasema kuvua gamba lazima sijui ni gamba lipi anazungumzia! Aanze kwa bosi wake tuone.
 
Hawa wa mama wasubiri tu, walikuwa na KM machachari pale Afya, akaangalia tumbo lake tu na maadhimisho 77 88! kumbukumbu yao?
 
Hotel nzuri sana.Kweli Tanzania imeendelea
 
hii serikali hii, puuuuuuuuuuuuu, nawatema!
 
Mh hii kitu ni noma,kama picha zipo hongeza zaidi mkuu
 
@ Ndugu Original Kama hujui kitu nyamaza tu.JK ndiyo mmliki wa Bilila Lodge na hakuna ubishi.Na amekuwa kuwadi mzuri wa huyo mwarabu aliyemuonga SUTI TANO rejea wikileakes report.
Kwa taarifa yako ni kuwa wakati hotel hiyo inajengwa kulipatikana madini ya dhahabu sehemu hiyo na watu walipiga sana mawe hapo na inasemekana bado kuna migodi haramu sehemu hizo.Singita lodge na mali za akina Sir George Kahama wakongwe wa siasa za ccm tangu enzi za mwalimu ingawa sasa umri ummechakaza anachungulia kaburi na Mmarekani moja tajiri.
JK NI BONGE LA FISADI NA KAMA ANA UBAVU WA KUKEMEA UFISADI MUULIZE SHERIA YA KUTENGANISHA BIASHARA NA SIASA ILIISHIA WAPI NA AMESHINDWA WAPI ?, MBONA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA ILITOLEWA BILA AHADI?.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…