Mwanadiplomasia Mahiri
JF-Expert Member
- Nov 4, 2019
- 491
- 1,907
Mwaka 2005 wakati Jakay Mrisho Kikwete akijinadi kuomba kura katika uchaguzi mkuu, siku ya kufunga kampeni alianguka pale Jangwani.
Hii ikaleta mabadiliko makubwa ya kiulinzi katika korido za PSU.
Kabla ya Kikwete, yaani kuanzia Nyerere, Mwinyi hadi Mkapa walikuwa wakisimama jukwaani kuhutibia basi nyuma yao huwa amesimama ADC (Mpambe) tu.
Lakini baada ya tukio lile la mwaka 2005, idara ya Usalama ikaanza kuwawekea Marais waliofata utaratibu wa kuwa na Mpambe (yule mwanajeshi) pembeni yake akiwepo na Mlinzi anayevaa kaunda suti.
Walifanya hivyo ili kuhakikisha kuwa ikitokea dharura basi waweze kusaidiana kama ni kumdaka ili Rais asipate matatizo zaidi.
Ikumbukwe, Rais huwa ana walinzi wengi sana ila sio wote wanakuwa karibu nae zaidi hasa majukwaani. wengine huzunguka jukwaa na maeneo mengine.
Utarativu huu wa Rais kuwa anahutubia huku nyuma akiwa na Mlinzi pamoja na Mpambe unafanywa hapa Tanzania tu kwa nchi za Afrika ya Mashariki.
Ahsanteni kwa kunisoma!!