Rais Kikwete amethibitisha kuwa ni kigeugeu na ndumilakuwili

Rais Kikwete amethibitisha kuwa ni kigeugeu na ndumilakuwili

Lizabon wewe ndio mpuuz wa mwisho!!! Unayoyasema ni utashi na kutetea io hongo yako wanayo kuhonga hao sisiemu!
Ulipo kosea ni kusema kua chama cha CUF wanataka nchi ya Pemba?! Jambo ambalo hata kwenye historia hakuna, inaonesha hata histry hujui, huna tafaut na wazir wako wa elimu aliposema Tanzania ni muungano wa pemba na.....
JIANGALIE USIFUATE KUNDI TU!!

Said
 
hivi huyu Kiwete si ndo alisema hamjui yule sheikh wa Richmond wala hana uhusiano naye halafu yule sheikh akaja akaenda ikulu kiwete akamkimbia au nimekosea? Usishangae hayo ndo mambo ya kuwa na rais mswahili!!!!!!!! anaongea halafu anasahau ameongea nini!
 
10155453_10203803214067111_1759039546_n.jpg

Hahahaaaaa.... He is listed to Cameroon.... Teh teh.... Bora M7 alie ikataa kabisa......
 
Lizaboni kama wewe siyo Kikwete basi utakuwa na matatizo ya kusifia hata yasiyo na sifa
 
Wapo watu humu wazembe kusoma, pia wazembe kufikiri. Mtoa mada hajataja Chadema w Dr. Slaa maana hawa hawako kwenye chama kinachoongoza wala serikali. Ila inaonekana ni watu mwiba sana kwa watawala. Leteni hoja kama mnazo si kutaja ambao hawajatajwa kwenye mada. Hapo mbakimbia mada.
 
Wana JF,

Nimeonelea nilete mada hii ili kuonyesha namna kiongozi wetu Mkuu wa nchi Rais Jakaya Kiwete alivyo mnafiki,mwongo,kigeugeu na ndumila kuwili.Hoja yangu itazungumzia maeneo muhimu matatu ambayo Rais amewadhihirishia Watanzania na dunia yote kuwa ni mnafiki.

Kwanza wakti Rais Kiwete akiunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliutangazia umma wa Watanzania kwamba kuna haja ya kuwa na Katiba Mpya itakayoipeleka Tanzania kwa miaka mingine 50-100. Tume iliundwa alimaarufu kama Tume ya Warioba ambayo iliafanya kazi kwa umakini na ustadi mkubwa sana. Tume ikamaliza Rasimu zote 2 na hatimaye kumkabidhi Rais Kiwete na akaisifia sana Tume hiyo.

Lakini shida imeanza kuonekana baada ya Tume kukabidhi Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba na kufuatia kuundwa kwa Bunge Maalumu la Katiba-BMK na yeye kwenda Dodoma kulizindua Bunge hilo. Hapa ndipo Rais alianza kuonyesha rangi zake za undumila kuwili. Kile alichokizungumza Rais Kiwete Bungeni hakika hakikutarajiwa na Mtanzania yeyote mwenye kuitakia mema nchiu hii. Hotuba hii ambayo haikuwa hotuba baali kujibu mapigo kwa Tume ya Jaji Warioba na hotuba yake wakti akikabidhi Rasmu ya Tume yake.

Kila mtanzania alipigwa na bumbuazi kwa maneno hayo yaliyokuwa yamejaa kejeli,kebehi na dharau kwa Tume ya Jaji Warioba.Rais Kiwete aliisahmbulia kwa lugha ya kifedhuli na kukosoa mapendekezo yaliyomo kwenye Rasmu hiyo na hasa kipengele cha Muundo wa Serikali TATU na Ukomo wa Ubunge.

Jambo la lushangaza kabisa ni juzi alipokuwa London,Uingereza alipoongea na Watanzania na kuwaambia kuwa hana tatizo na Muundo wa Serikali 3 kama Watanzania wataamua hivo! Hapa ndipo penye unafiki wa Kiwete.Hii ilikuwa ni kauli ya ajabu sana maana ilikuwa inapingana na Hotuba yake ya Bungeni. Bungeni alitetea Serikali 2 kama msimamo wa CCM yake badala ya kutetea MAONI YA WATANZANIA 60% WANAOTAKA SERIKALI 3 KUPITIA TUME YA WARIOBA!!

Lakini pia kebehi,dharau na matusi ya Kikwete kwa Tume yaliendelezwa na Katibu wake Mkuu wa CCM Bwana Abdulrhaman Kinena alipohutubiwa wana CCM katika Viwanja vya Kidongo chekundu akihoji uhalali na umakini wa Tume ya Warioba ya kupendekeza Serikali 3. Kinena alisema kuwa kulikuwa ati na Mabaraza zaidi ya 110(ya CCM) yaliyopendekeza Serikali 2 lakini kwenye Rasimu ya Wariona haikuonyeshwa. Tume ikiulizwa inasema makabrasha yamepotea!!! Hapa Kinena alikuwa anaiponda Tume kwamba haikufanya kazi iliyotumwa baali imefanya kazi yake yenyewe!!!Ni dhahiri Kinena alikuwa nazungumza maneno haya kwa kujiamini kwa vile ndicho kilichomo ndani ya nafsi ya Kikwete!

Juzi Jaji Warioba ametupiwa virago kama kocha wa mpira aliyeshindwa kuifundisha Timu ya mpira. Ikulu ya Kiwete imedai kuwa Tume ilishamaliza kazi kwa hiyo kila mali waliyokuwa wakiitumia TUME yakiwemo magari virudishwe mara moja Ikulu.Je, kulikuwa na uharaka gani wa amri hizi za kibabe na kijeshi? Hivi kosa la Warioba na Tume yake ni kuingiza maoni ya Watanzania walio wengi kuwa wanataka Muungano wa Serikali 3?

Ni dhahiri kabiosa kuwa Kikwete na CCM yake wamewadhihirishia Watanzania na Dunia yote kuwa ni wanafiki na walitaka Tume ya Warioba iweke mapendekezo ya CCM kwenye Rasmu na siyo mapendekezo ya Watanzania walio wengi. Hii ni aibu kwa Kiwete, CCM na Serkali yake. Upuuzi huu ndiyo unaoendelezwa hata ndani ya BMK ya kutetea mawazo na maoni ya CCM na siyo mapendekezo ya Watanzania!!!

Tafakuri.

Ila wakati mwingine tunamchanganya na sisi wenyewe, hasa pale inapofikia"za kwake achanganye na za kwetu" Sisi tupo million 45, yeye yupo peke yake!
 
Mtoa mada una upungufu mkubwa sana wa ufahamu. Ngoja nikupe somo kidogo. Mada yako imejikita kwenye hoja ya katiba. Well umeelezea jinsi Rais alivyotangaza kuwa anadhamiria kuunda tume itakayokusanya maoni ya wananchi juu ya katiba mpya. Ukaeleza kuwa Jaji Warioba ndiye aliyepewa kazi hiyo. Well umeeleza kuwa Warioba amefanya kazi yake vizuri kiasi cha kupongezwa na Rais Kikwete. Well ukasema kuwa wakati anaenda kulizindua Bunge Maalum ndipo hali ya hewa ilipochafuka hasa baada ya Rais Kikwete kukosoa Rasimu hiyo. Well ukasema kuwa Rais alieleza akiwa London Uingereza kuwa hana matatizo na mfumo wa serikali tatu ikiwa wananchi wataamua. Hizo ndizo hoja zako juu ya Rais Kikwete.

kwanza, unapaswa kuelewa kuwa msukumo wa kuwa na katiba mpya haukutokana na utashi wa serikali. Msukumo huo ulitokana na tamaa za madaraka za viongozi wa vyama vya upinzani. Ukumbuke kuwa CHADEMA hawakubaliki Zanzibar. Kwao Zanzibar haina umuhimu wala faida kwao. CHADEMA hawana hata mbunge mmoja kule. CUF haikubaliki zaidi Tanzania Bara. Kwa sasa ina wabunge watatu tu ambapo wawili ni wa kuchaguliwa tena wote wakitoka mkoa mmoja tu wa Lindi na mmoja ni wa viti maalum. CUF nguvu yao kubwa ipo visiwani Zanzibar tena kwenye kisiwa cha Pemba tu. Unguja hawana kabisa nguvu. Hivyo shinikizo la vyama hivi juu ya katiba mpya hususan huu muundo wa serikali tatu linatokana na tamaa ya madaraka. CHADEMA wanaamini kuwa ikiwa kutakuwa na serikali ya Tanganyika, wao wanaweza kushinda kwa kile wanachoamini kuwa wanakubalika zaidi Tanzania Bara japo uhalisia uliopo ni kwamba hiki ni chama cha Kaskazini. CUF nao wanaamini kuwa ikiwa katiba mpya itapatikana yenye muundo mwingine zaidi ya uliopo, ni kwamba wao wanaweza kupata fursa ya kutawala Zanzibar na shauku yao kubwa ni kuwa na nchi huru ya Pemba. Katika mazingira hayo, ni wazi kuwa vyama hivi vilizunguka mlango wa nyima ili kuirubuni tume ya Warioba ikubaliane na matakwa yao. Hapo Rais Kikwete alikuwa na haki ya kuonesha wasiwasi wake juu ya hiyo tume.

kuhusu kuipongeza tume na baadaye kuikosoa, ni jambo la kawaida kumpongeza mtu unapomtuma kazi na akaimaliza. Sasa unapoiangalia kazi uliyomtuma halafu ukagundua kuwa ina mapungufu mengi na pengine ameenda kinyume na maelekezo yako, je utaendelea kumsifia? Ni wazi kwamba utaikosoa kazi hiyo na kuonesha mapungufu yaliyopo. Ndivyo alivyofanya JK. Aliipokea Rasimu ile na akaipongeza tume kwa kazi waliyofanya. Ila baada ya kuipitia, akagundua mapungufu kadhaa ambayo ni vema kuyaeleza tena kwenye bunge ambalo ndilo lenye maamuzi ya mwisho juu ya Rasimu hiyo. Ningemshangaa sana Rais Kikwete kama angeyaona mapungufu hayo halafu akayanyamazia.

Kuhusu kauli yake kuwa yupo tayari kuunga mkono muundo wa serikali tatu ikiwa wananchi wataamua, well. Namponyeza pia kwa uamuzi huo. Ikiwa wananchi wote au kwa kiwango kikubwa tumekubaliana kuunga mkono muundo huo, ni wazi kuwa hata yeye Rais ataungana nasi kwa vile anajua kuwa ni maamuzi ya wengi. Ila haiingii akilini kati ya watu laki tatu walioohojiwa na Warioba, watu 47,000 waonekane ni wengi kuliko wale 300,000. Hapa ni wazi kuwa Warioba na timu yake wameonesha udhaifu wa hali ya juu sana. Katika hali hiyo, ni wazi kuwa Warioba amejitakia kudharauliwa si na Rais tu bali na kila anayeitakia mema nchi hii.

Kauli ya kinana nayo ni ya kuungwa mkono. Mathalan, Kinana amehoji wapi zimeenda takwimu za mabaraza ya kata na wilaya. Mbona taarifa zake hazikutolewa? Ni wehu tu na watu wenye upeo mdogo wa kufikiri kama mtoa mada ndio watakaomshambulia Kinana

Msikwepe ukweli kwa hoja za kitoto za kinana eti mabaraza ya kata!! Mabaraza mliyoyajaza wanaccm ulitegemea kuwa ndio reference ya wananchi wa Tanzania!!. Ukweli ni kuwa Zanzibar wana katiba yao ambayo ina baraka za Rais wa Jamuhuri sasa unataka TAnganyika tufanyeje!

Hata hivyo kwa uelewa wenu mdogo ulifikiri nchi hii ni mali ya CCM??? Usitegemee watanzania ni wabovu wa kufikiri na kuwa kinana ndio yuko sahihi !! Anatwanga maji kwenye kinu tu!!
 
Jibu kwa hoja mkuu. Si kulalamika tu. by the way, nchi hii ni mali ya CCM. wengine ni wadandiaji tu
 
Lizaboni anakwambia wao ndiyo vijana wa Lumumba a.k.a vijana wa Muhindi Shiv.ji.
Sera yao ni Chama kwanza Taifa baadae
Anakutemea alicholishwa na chama, ila nataka kukujuza tu siku hizi usemi wa wengi wape hau-apply.
Siku hizi wachache wanasikilizwa na maoni yao yanapita
 
Last edited by a moderator:
Kama kuna kosa ambalo hatupaswi kulirudia ni kumpa madaraka ya urais mtu aliyekulia tui la nazi kama huyu Kiwete.
 
dr slaa ndio kigeugeu namba moja afrika

Jibu hoja kwa hoja, si ndo wan ccm mnasemaga hivyo!! Hapo dr slaa ametokea wapi? Dadadvua kama mleta hoja alivyofanya, leta ushahidi na mengineyo kupinga kama si kweli! Haya mengine ni ya kawaida tu, au unaweza kuwa uko kwenye list ya buku saba eeh?
 
Kuhusu kauli yake kuwa yupo tayari kuunga mkono muundo wa serikali tatu ikiwa wananchi wataamua, well. Namponyeza pia kwa uamuzi huo. Ikiwa wananchi wote au kwa kiwango kikubwa tumekubaliana kuunga mkono muundo huo, ni wazi kuwa hata yeye Rais ataungana nasi kwa vile anajua kuwa ni maamuzi ya wengi. Ila haiingii akilini kati ya watu laki tatu walioohojiwa na Warioba, watu 47,000 waonekane ni wengi kuliko wale 300,000. Hapa ni wazi kuwa Warioba na timu yake wameonesha udhaifu wa hali ya juu sana. Katika hali hiyo, ni wazi kuwa Warioba amejitakia kudharauliwa si na Rais tu bali na kila anayeitakia mema nchi hii.

Sina hakika kama Warioba alienda kuwahoji watu maana hapo ingemlazimu kuwa na maswali kwaajili ya kuwahoji hao wananchi. Lakini ninachojua ni kwamba alienda kukusanya maoni kwa wananchi waliokuwa tayari kueleza chochote wanachoona inafaa kuingizwa kwenye Katiba mpya. Hii inamaana kwamba watu walikuwa na uwanja mpana wa kueleza mambo yao kwa muda mfupi. Pia kumbuka kwamba kutotoa maoni juu ya muungano uliopo haimaanishi kwamba wewe huridhiki au unaridhika juu ya muungano huo. Huenda wengine hawakutoa maoni juu ya muungano kwasababu waliona wenzao waliokuwepo kwenye huo mkutano tayari walikwisha toa maoni juu ya muungano. Lakini ili kukata mzizi wa fitina basi iitishwe kura ya maoni juu ya aina ya muungano tuutakao.

Kuhusu idadi ya watu waliotoa maoni juu ya muungano, Warioba anatoa mfano unaofanana na huu; Tanzania ina idadi ya watu 25mil wanaostahili kupiga kura ya kumchagua Rais wa JMT. Watu waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 20mil, Watu waliopiga kura walikuwa 8.5mil, kati ya hao watu 6mil walimchagua JK kuwa Rais wa JMT. Je, utasema huyo Rais aliyechaguliwa si Rais halali wa JMT kwasababu tu amechaguliwa na watu 6mil tu kati ya watu 20mil waliojiandikisha kupiga kura?

Tuache kuwapotosha watu kwa maslahi binafsi, Warioba ametolea ufafanuzi mzuri wa takwimu zilivyokokotolewa, na mimi sitaki kuamini kwamba wewe huelewi alichokiongea Warioba.
 
Lizabon wewe ndio mpuuz wa mwisho!!! Unayoyasema ni utashi na kutetea io hongo yako wanayo kuhonga hao sisiemu!
Ulipo kosea ni kusema kua chama cha CUF wanataka nchi ya Pemba?! Jambo ambalo hata kwenye historia hakuna, inaonesha hata histry hujui, huna tafaut na wazir wako wa elimu aliposema Tanzania ni muungano wa pemba na.....
JIANGALIE USIFUATE KUNDI TU!!

Said

wewe ndo m.pu.mb.a.v.u na .wa.j.i.n.g.a wenzako ccm unaowatetea
 
Hapo penye rangi nyekundu, huyo ndiyo nani?

bantulile,

Huyo ni Kinena Katibu Mkuu wa Chama Twawala CCM almaarufu kama KINANA na mtaalamu wa KUUA NA KUUZA MENO YATEMBO(PEMBE ZA NDOVU) NJE NA NDANI YA TANZANIA!
 
Wana JF,

Nimeonelea nilete mada hii ili kuonyesha namna kiongozi wetu Mkuu wa nchi Rais Jakaya Kiwete alivyo mnafiki,mwongo,kigeugeu na ndumila kuwili.Hoja yangu itazungumzia maeneo muhimu matatu ambayo Rais amewadhihirishia Watanzania na dunia yote kuwa ni mnafiki.

Kwanza wakti Rais Kiwete akiunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliutangazia umma wa Watanzania kwamba kuna haja ya kuwa na Katiba Mpya itakayoipeleka Tanzania kwa miaka mingine 50-100. Tume iliundwa alimaarufu kama Tume ya Warioba ambayo iliafanya kazi kwa umakini na ustadi mkubwa sana. Tume ikamaliza Rasimu zote 2 na hatimaye kumkabidhi Rais Kiwete na akaisifia sana Tume hiyo.

Lakini shida imeanza kuonekana baada ya Tume kukabidhi Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba na kufuatia kuundwa kwa Bunge Maalumu la Katiba-BMK na yeye kwenda Dodoma kulizindua Bunge hilo. Hapa ndipo Rais alianza kuonyesha rangi zake za undumila kuwili. Kile alichokizungumza Rais Kiwete Bungeni hakika hakikutarajiwa na Mtanzania yeyote mwenye kuitakia mema nchiu hii. Hotuba hii ambayo haikuwa hotuba baali kujibu mapigo kwa Tume ya Jaji Warioba na hotuba yake wakti akikabidhi Rasmu ya Tume yake.

Kila mtanzania alipigwa na bumbuazi kwa maneno hayo yaliyokuwa yamejaa kejeli,kebehi na dharau kwa Tume ya Jaji Warioba.Rais Kiwete aliisahmbulia kwa lugha ya kifedhuli na kukosoa mapendekezo yaliyomo kwenye Rasmu hiyo na hasa kipengele cha Muundo wa Serikali TATU na Ukomo wa Ubunge.

Jambo la lushangaza kabisa ni juzi alipokuwa London,Uingereza alipoongea na Watanzania na kuwaambia kuwa hana tatizo na Muundo wa Serikali 3 kama Watanzania wataamua hivo! Hapa ndipo penye unafiki wa Kiwete.Hii ilikuwa ni kauli ya ajabu sana maana ilikuwa inapingana na Hotuba yake ya Bungeni. Bungeni alitetea Serikali 2 kama msimamo wa CCM yake badala ya kutetea MAONI YA WATANZANIA 60% WANAOTAKA SERIKALI 3 KUPITIA TUME YA WARIOBA!!

Lakini pia kebehi,dharau na matusi ya Kikwete kwa Tume yaliendelezwa na Katibu wake Mkuu wa CCM Bwana Abdulrhaman Kinena alipohutubiwa wana CCM katika Viwanja vya Kidongo chekundu akihoji uhalali na umakini wa Tume ya Warioba ya kupendekeza Serikali 3. Kinena alisema kuwa kulikuwa ati na Mabaraza zaidi ya 110(ya CCM) yaliyopendekeza Serikali 2 lakini kwenye Rasimu ya Wariona haikuonyeshwa. Tume ikiulizwa inasema makabrasha yamepotea!!! Hapa Kinena alikuwa anaiponda Tume kwamba haikufanya kazi iliyotumwa baali imefanya kazi yake yenyewe!!!Ni dhahiri Kinena alikuwa nazungumza maneno haya kwa kujiamini kwa vile ndicho kilichomo ndani ya nafsi ya Kikwete!

Juzi Jaji Warioba ametupiwa virago kama kocha wa mpira aliyeshindwa kuifundisha Timu ya mpira. Ikulu ya Kiwete imedai kuwa Tume ilishamaliza kazi kwa hiyo kila mali waliyokuwa wakiitumia TUME yakiwemo magari virudishwe mara moja Ikulu.Je, kulikuwa na uharaka gani wa amri hizi za kibabe na kijeshi? Hivi kosa la Warioba na Tume yake ni kuingiza maoni ya Watanzania walio wengi kuwa wanataka Muungano wa Serikali 3?

Ni dhahiri kabiosa kuwa Kikwete na CCM yake wamewadhihirishia Watanzania na Dunia yote kuwa ni wanafiki na walitaka Tume ya Warioba iweke mapendekezo ya CCM kwenye Rasmu na siyo mapendekezo ya Watanzania walio wengi. Hii ni aibu kwa Kiwete, CCM na Serkali yake. Upuuzi huu ndiyo unaoendelezwa hata ndani ya BMK ya kutetea mawazo na maoni ya CCM na siyo mapendekezo ya Watanzania!!!

Tafakuri.
Kwani Jk sio Mtanzania?
 
Mkuu, usihangaike na huyo jamaa. Amedhamiria kuandika hivyo. Anastahili kupigwa ban ya maisha ili iwe fundisho wa wengine

Lizaboni,

Usitake kuminya uhuru wa watu wengine kujieleza kwa namna ambayo wanaona inafaa ili kufikisha ujumbe uliokusudiwa.Unaposema nipigwe ban, kwa kosa lipi hapo? Kutamka Kinena badala ya Kinana kuna tatizo gani mkuu? Kila mtu lazima awe na kitu inaitagwa, ''nickname'' au kwa lugha ingine''a.k.a''.

Nickname siyo tusi baali ni jina mbadala wanaloweza watu kukuita kutokana na tabia,hulka au mwenendo wako katika jamii. Sioni tatizo la kumwita Kinana kuwa Kinena au Kikwete kuwa Kiwete. Kama Baba wa Taifa Mwl. JK Nyerere watu walimwita 'Mchonga' au 'Haambiliki' kuna ajabu gani ya kuwaita hawa vigogo wa CCM kwa majina haya ya utani???

Jenga hoja acha umbeya!!
 
Back
Top Bottom