MWEEN
JF-Expert Member
- Feb 6, 2010
- 482
- 207
Sasa naona bora kazi ya uteuzi ifanywe na JF, maana kila anaemteua Rais wanasema ni wale wale tu hakuna jipya.
Mkuu,
Mzee Mkapa alishaweka taratibu nzuri tu za kuwateua watu kama hawa. Ulishaanza mpango wa kutangaza hizi nafasi halafu watu wote wakapata nafasi ya ku-apply. Halafu wanachaguliwa katika ushindani wa CV na utendaji. Kama unakumbuka, wakurugenzi wote wizarani na wale wa Wilaya walishaanza kuajiriwa kwa njia hii.
Aliposhika Kikwete mwaka 2005, wakakosa namna ya kuwazawadia marafiki hivyo kidogo kidogo wakaipuuzia sheria hii na baadaye wale wote walioajiriwa kwa mpango wa kushindanisha wakaondolewa na kuwekwa wakwao. Nakumbuka kuna kurugenzi moja ilikaa kwa zaidi ya mwaka na nusu ikiwa na Acting Director kwa sababu huyo aliyekuwa ana-act hakuwa na sifa zinazotakiwa hapo hapo Lowassa alikuwa anataka yeye ndio apewe hiyo nafasi. Baadaye sana walichukua kilaza mmoja toka mikoani kwenye hiyo nafasi.
Mimi nilikuwa mmoja wa waliyoomba hiyo nafasi mpaka leo sijui maombi yale yaliishia wapi. Kwa kifupi, usitegemee chochote kutoka kwa hawa wanaoteuliwa kwani wanasimamia maslahi ya waliowateua. Ni chungu kile kile ila kilichomo kinakorogwa kidogo halafu anaokota jina.