Rais Kikwete amteua Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi mpya wa mashtaka (DPP)

Rais Kikwete amteua Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi mpya wa mashtaka (DPP)

Hapa ndipo ule utaratibu uliopendekezwa na Tume ya Warioba ulipopaswa kufanya kazi kabla ya kuingia ofisini. Kulitakiwa kuwe na chombo kingine kama Bunge ambalo sasa lingeingia kazini kumfanyia usaili mteule huyu kujua uwezo wake na kama anastahili kweli kushika wadhifa huu au lah. Hii ingeepusha utaratibu wa Rais kuteua washkaji au watu wa kulinda maslahi binafsi. Lakini masikini wabunge wa CCM wameukataa utaratibu huu na kuendelea kumrundikia Rais madaraka mazito!!!!

haitoshi kulalama humu peke yake. Chukua hatua za kizalendo dhidi ya mfumo usiofaa. Nipo njiani kuingia msituni ... full mass in order!
 
Hongera DPP mpya, karibu tuchape kazi, tutakupa ushirikiano wa kutosha.
 
Tumpe hongera kwa uteuzi wake huo mpya

Hata hivyo itakuwa vyema Mkurugenzi huyo mpya wa mashitaka,kama kazi yake na 1 atakapoingia ofisini,ataamua kuwaburuza mahakamani, vigogo wote waliokwapua zile shilingi bilioni 200 za kwenye akaunti ya Escrow.
mmeishaambiwa ni bilioni 400, lakini bado mnapotosha uma kua ni 200.
 
Kwakuwapamba viongozi hatujambo ?

Hata kama hatujui utendaji wake tunajikita kusifiatu
Hamjui kua watu wana tafuta namna ya kufunika kombe ?
 
Kama huyo Biswalo ana ubavu, mtu wa kwanza kumburuza mahakamani kwa corruption ni Andrew Chenge kwa ile CHENJI ya radar kwani ushahidi upo, ila Feleshi alimlinda kwasababu ya undugu wao!!
 
Mojawapo ni kesi ya madawa kilo tisini iliyoendeshwa na jaji Mussa Kipenka mkoani Tanga mwaka jana na watuhumiwa kuwa sentenced thirty years imprisonment.
 
Tumpe hongera kwa uteuzi wake huo mpya

Hata hivyo itakuwa vyema Mkurugenzi huyo mpya wa mashitaka,kama kazi yake na 1 atakapoingia ofisini,ataamua kuwaburuza mahakamani, vigogo wote waliokwapua zile shilingi bilioni 200 za kwenye akaunti ya Escrow.
hao watu woote mnaoongea hawawezi kupelekwa mahakamani hadi dr.hosea alete ushahidi. tatizo ushahidi hawapelekei hawa, ndio maana. walishaleta hapa jinsi kesi ya uda hosea alivyoshindwa kuleta ushahidi na baadhi ya washitakiwa akawaweka kama mashahidi dpp alipowakamata na kuwabadilisha wawe washitakiwa (simon group mr.kisena) ndio hosea hajapeleka ushahidi ikabidi ili kuokoa jahazi kesi ifutwe kwa nolle (nolle matokeo yake ni kwamba anytime ushahidi ukiletwa kesi inaanza upya hivyo hosea kama ana ushahidi hata leo hii iddi simba na kina simon group wanaweza kuburuzwa). hapo utamlaumu nani? offisi ya dpp au takukuru?
 
mmeishaambiwa ni bilioni 400, lakini bado mnapotosha uma kua ni 200.
Nashukuru kwa marekebisho hayo, kumbe 'visenti' vilivyokwapuliwa ni mara 2 ya vile vinavyoripotiwa kwenye vyombo vya habari?

Hata hivyo, hatumtegemei DPP mpya bwana Biswelo Mganga afuate nyayo za Bosi wake aliyemteua, ambaye wakati wa skandali ya EPA, aliwapa 'msamaha' wote waliojichotea mabilioni huko benki kuu, na kuwaambia warejeshe tu hayo mabilioni waliyoiba, na mchezo ndiyo utakuwa umeishia hapo!
 
mkuu kapu ni lilelile sema limebadirishwa mshikio.
 
hao watu woote mnaoongea hawawezi kupelekwa mahakamani hadi dr.hosea alete ushahidi. tatizo ushahidi hawapelekei hawa, ndio maana. walishaleta hapa jinsi kesi ya uda hosea alivyoshindwa kuleta ushahidi na baadhi ya washitakiwa akawaweka kama mashahidi dpp alipowakamata na kuwabadilisha wawe washitakiwa (simon group mr.kisena) ndio hosea hajapeleka ushahidi ikabidi ili kuokoa jahazi kesi ifutwe kwa nolle (nolle matokeo yake ni kwamba anytime ushahidi ukiletwa kesi inaanza upya hivyo hosea kama ana ushahidi hata leo hii iddi simba na kina simon group wanaweza kuburuzwa). hapo utamlaumu nani? offisi ya dpp au takukuru?
I see!
 
kwasababu ofisi ya dpp haikusanyi ushahidi na haikamati watuhumiwa, inategemea takukuru wakusanye ushahidi na kukamata watuhumiwa wapeleke kwa dpp. kama takukuru wakiamua kumsaidia mshitakiwa wanaweza kuharibu ushahidi washitakiwa wakawaweza mashahidi n.k ili kujifanya wanafanya kazi wakapeleka jalada kwa dpp aendeshe, hivi hapo dpp atashinda kesi? mnajua kama ili kushinda kesi upelelezi iwe polisi au takukuru wanatakiwa kuwa wamefanya upelelezi mzuri na kukusanya vielelezo vizuri sana? ofisi ya dpp kama kuna vielelezo vyote, mashahidi, haina jinsi ila kumshitaki mtu hadi afungwe.hivi ndivyo nionavyo mimi.
 
Mganga ni mchapakazi wa kuigwa.... anastahili uteuzi huu. Nampongeza kwa dhati. Nimefanya naye kazi kwa karibu sana. Uwezo wake ni mkubwa na ameendesha mashauri mengi magumu kwa ufanisi. Hongera Mganga. Piga kazi kwa bidii zaidi.

Maelezo gani haya? Ni kama yale ya Nape, Sitta au Lukuvi! Unawezaje kutumia maneno yasiyopimika? Mkubwa, mengi, ufanisi... nini hii sasa? Takataka.

Tuambie hayo mengi ni mangapi? uwezo mkubwa ni upi na alifanya nini kikubwa? Huo ufanisi ni upi. Kama huna la kuandika acha kampeni za bungeni wakati unajua hao wanajua kusoma na kuandika tu!
 
hao watu woote mnaoongea hawawezi kupelekwa mahakamani hadi dr.hosea alete ushahidi. tatizo ushahidi hawapelekei hawa, ndio maana. walishaleta hapa jinsi kesi ya uda hosea alivyoshindwa kuleta ushahidi na baadhi ya washitakiwa akawaweka kama mashahidi dpp alipowakamata na kuwabadilisha wawe washitakiwa (simon group mr.kisena) ndio hosea hajapeleka ushahidi ikabidi ili kuokoa jahazi kesi ifutwe kwa nolle (nolle matokeo yake ni kwamba anytime ushahidi ukiletwa kesi inaanza upya hivyo hosea kama ana ushahidi hata leo hii iddi simba na kina simon group wanaweza kuburuzwa). hapo utamlaumu nani? offisi ya dpp au takukuru?

Hosea ushahidi anao ila tu ni fisadi wa aina yake pia. Tangu akiwa kusini kazi yake ilikuwa kusimamia kampuni yake ya u-advocate. Mara zote ilikuwa ukiwa na kesi ya rushwa lazima uipe kampuni yake ili mambo yaharibiwe. Ni mtu ambaye hawezi kufanya kazi yake.

Lakini pia hiyo kazi imekuwa ni ya kisiasa. Wanaongozwa na ikulu na marafiki wa ikulu. wakisema acha, wanaacha. Wakisema endelea, wanaendelea. Makao makuu ya TAKUKURU wanashindana kuchota rushwa pia. Ukiwa na kesi mikoani ukasumbuliwa na vijana wa mikoani, wewe tafuta mtu wa makao makuu na mara moja watatoa amri ya kuachana nayo. Ndivyo ilivyotokea Tarime kwa viongozi wa Wilaya waliokuwa wakipewa pesa na mgodi wa nyamongo kila mwezi ili kuwatia adabu wananchi. Ushahidi ulikuwepo tena wa maandishi na sahihi zao za malipo.
 
Nchi hii kwa Udini sasa uarabu umeigiaje,mfumo kristo mbaya sana.nyinyi endeleeni kutubeep beep tu.tusipoangalia Nchi nzuri tutaiharibu hii.

Bila shaka ww ndo unaleta udini hapo,kusikia neno 'Kiarabu' tayari unafikiria uislamu wakati mwenzio anaongelea uandishi wa kiarabu.
Hivi kila mwarabu ni muislamu eh?
 
Rais Kikwete amemteua Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi Mpya wa Mashtaka nchini (DPP). Kabla ya uteuzi wake, Biswalo alikuwa Mkurugenzi msaidizi katika ofisi hiyo ya mashtaka. Uteuzi umeanza rasmi ijumaa iliyopita.

Dr Eliezer Feleshi ndie alikuwa akishikilia wadhifa wa DPP kabla ya uteuzi huu wa DPP mpya kufanyika.

==============

Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) nchini.

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam, leo, Jumatatu, Oktoba 6, 2014, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Bwana Peter Ilomo imesema kuwa uteuzi huo umeanza Ijumaa iliyopita, Oktoba 3, mwaka huu, 2014.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mganga alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka na Wakili wa Serikali Mfawidhi.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

6 Oktoba, 2014

Biswalo! !!! Hiyo ni mashine toka kanda maalum! !!!
Kwa vyovyote, hilo ni jembe. ...

Hilo jembe huwa linakulima wewe! Ile kesi ya Samaki wa magufuli iliishaje?
 
Back
Top Bottom