Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rais Kikwete amemteua Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi Mpya wa Mashtaka nchini (DPP). Kabla ya uteuzi wake, Biswalo alikuwa Mkurugenzi msaidizi katika ofisi hiyo ya mashtaka. Uteuzi umeanza rasmi ijumaa iliyopita.
Dr Eliezer Feleshi ndie alikuwa akishikilia wadhifa wa DPP kabla ya uteuzi huu wa DPP mpya kufanyika.
==============
Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) nchini.
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam, leo, Jumatatu, Oktoba 6, 2014, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Bwana Peter Ilomo imesema kuwa uteuzi huo umeanza Ijumaa iliyopita, Oktoba 3, mwaka huu, 2014.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mganga alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka na Wakili wa Serikali Mfawidhi.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
6 Oktoba, 2014
kuna kitu jiwe alikuwa anajaribu ku prove!Mkiambiwa kuna mtu ameshika remote control na kutuonesha channel anazotaka yeye mnabisha sasa mnaona ushahidi
kuna kitu jiwe alikuwa anajaribu ku prove!
watu wake hao hao walipitia mikono ya huyu jamaa!
haya na kazi iendelee!
Tupe mrejesho sasangoja tumfuatilie tuone uwezo wake .
Anaburuzwa mahakamani keshoTupe mrejesho sasa
Sio kwamba anaapishwa kuwa jajiAnaburuzwa mahakamani kesho