Rais Kikwete amteua George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Ndugu wana JF, nimefurahi sana kwa uteuzi huu wa Bw. George Mcheche Masaju. Kwa ufupi: Ndugu Masaju, amewahi kufanyakazi ofisi ya mwanasheria mkuu kanda ya Dodoma, Mtwara, kanda maalumu ya Dar es salaam, mshauri wa sheria wa rais, na naibu mwanasheria mkuu. Ni mhitimu wa sheria Chuo kikuu cha Dar es salaam. Kiimani ni msabato. Furaha yangu imejikita katika mambo yafuatayo;
1. Ni mwanasheria mwenye uzoefu na uelewa wa kutosha. Akiwa amefanikiwa kuitetea serikali kwa mafanikio makubwa katika kesi mbalimbali, mfano; mtikila, pinda, na nk.
Najua wengi wetu (nikiwemo na mimi) hatukupenda matokeo ya kesi ya mtikila, na pinda (wapigwe tu), lakini ukiwa mwanasheria kazi yako kubwa ni kutetea maslahi ya mteja wako, na kwa upande wa Ndugu Masaju, ni serikali.
2. Ndugu Masaju amekulia na kulelewa ktk ofisi ya mwanasheria mkuu, hivyo anaijua vyema na itakuwa ni rahisi kwake kuifanyia mapinduzi ya kutosha. Tofauti kama angeteuliwa "outsider", yaani nje ya ofisi ya mwanasheria mkuu, angekuwa na kazi kubwa; kwanza, kujenga mahusiano na aliowakuta; pili, kuelewa utendajikazi wa ofisi ya AG na kuzoea kazi ambayo hakuwahi kuifanya.
3. Tuliofanikiwa kusoma report ya CAG, na PAC kuhusu escrow account, na kwa huo mchezo mchafu ulivyochezwa kwa usiri na ukihusisha AG ni wazi kabisa Ndugu Masaju asingeweza kujua kinachoendelea, ukizingatia waliohusika walijua kuwa ni msabato!
4. Ni utumaduni mzuri wa kupandisha vyeo watu walioitumikia serikali kwa uadilifu mkubwa. Utamaduni huu hujenga hamasa wa kujituma miongoni mwa wafanyakazi wa serikali. Ni vibaya sana, na inaua moyo wa kujituma, hasa unaposikia Judge au Professor kawa AG au wakili kawa Judge huku kuna mamia ya Mahakimu na state attorneys waaminifu.

Asante wana JF!
 
mbona nyie mnapenda propaganda na uzandiki wa kidini? ebu pendeni amani umoja na ushirikiano nyie watu

.........mlianza lini kupenda wenzenu nyie !?....kama mna mapenzi ya kweli mngerudisha pesa za escrow !:cool2:
 
Ndugu wana JF, nimefurahi sana kwa uteuzi huu wa Bw. George Mcheche Masaju. Kwa ufupi: Ndugu Masaju, amewahi kufanyakazi ofisi ya mwanasheria mkuu kanda ya Dodoma, Mtwara, kanda maalumu ya Dar es salaam, mshauri wa sheria wa rais, na naibu mwanasheria mkuu. Ni mhitimu wa sheria Chuo kikuu cha Dar es salaam. Kiimani ni msabato. Furaha yangu imejikita katika mambo yafuatayo;
1. Ni mwanasheria mwenye uzoefu na uelewa wa kutosha. Akiwa amefanikiwa kuitetea serikali kwa mafanikio makubwa katika kesi mbalimbali, mfano; mtikila, pinda, na nk.
Najua wengi wetu (nikiwemo na mimi) hatukupenda matokeo ya kesi ya mtikila, na pinda (wapigwe tu), lakini ukiwa mwanasheria kazi yako kubwa ni kutetea maslahi ya mteja wako, na kwa upande wa Ndugu Masaju, ni serikali.
2. Ndugu Masaju amekulia na kulelewa ktk ofisi ya mwanasheria mkuu, hivyo anaijua vyema na itakuwa ni rahisi kwake kuifanyia mapinduzi ya kutosha. Tofauti kama angeteuliwa "outsider", yaani nje ya ofisi ya mwanasheria mkuu, angekuwa na kazi kubwa; kwanza, kujenga mahusiano na aliowakuta; pili, kuelewa utendajikazi wa ofisi ya AG na kuzoea kazi ambayo hakuwahi kuifanya.
3. Tuliofanikiwa kusoma report ya CAG, na PAC kuhusu escrow account, na kwa huo mchezo mchafu ulivyochezwa kwa usiri na ukihusisha AG ni wazi kabisa Ndugu Masaju asingeweza kujua kinachoendelea, ukizingatia waliohusika walijua kuwa ni msabato!
4. Ni utumaduni mzuri wa kupandisha vyeo watu walioitumikia serikali kwa uadilifu mkubwa. Utamaduni huu hujenga hamasa wa kujituma miongoni mwa wafanyakazi wa serikali. Ni vibaya sana, na inaua moyo wa kujituma, hasa unaposikia Judge au Professor kawa AG au wakili kawa Judge huku kuna mamia ya Mahakimu na state attorneys waaminifu.

Asante wana JF!

Hivi hao SDA hawana Benki eeeh !?........ndo maana asingekubali kushiriki !?
 
Jakaya anajuwa fika watu wa imani yake uwezo mdogo. Asa kama yeye mwenyewe anajijuwa ana uwezo mdogo atafanya vipi kosa la kuteua wasaidizi wenye uwezo mdogo?
Ng'wanangwa

...wenye uwezo mkubwa ni wale wanao weza kuiba pesa za wananchi bila ya aibu na wakamshirikisha na Yesu (Kanisa) katika wizi huo !:eek2:
 
Last edited by a moderator:
George masaju ni mwanasheria mzuri, mjita wa bunda, product ya umbwe high school(a-level) na chuo kikuu cha dsm, msabato mzuri na si fisadi anamuogopa mungu

mmmh... ! mungu yule wa kwenye picha !?........huyo hata Kilaini hamuogopi !:A S 109:
 
Napita tu,il a ofsin kwetu once ukiwa kwenye Management level basi wewe hushiriki kwenye kupokea taarifa,kuandaa daily report,mapendekezo,kutoa maamuzi na kumshauri kwa busara Boss wako,vipi yeye?
 
Scandal ya Escrow ni vipi hahusiki,naamini alishauriana na Boss wake,yeye msimamo wake ulikuwa upi?
 
Ndugu wana JF, nimefurahi sana kwa uteuzi huu wa Bw. George Mcheche Masaju. Kwa ufupi: Ndugu Masaju, amewahi kufanyakazi ofisi ya mwanasheria mkuu kanda ya Dodoma, Mtwara, kanda maalumu ya Dar es salaam, mshauri wa sheria wa rais, na naibu mwanasheria mkuu. Ni mhitimu wa sheria Chuo kikuu cha Dar es salaam. Kiimani ni msabato. Furaha yangu imejikita katika mambo yafuatayo;
1. Ni mwanasheria mwenye uzoefu na uelewa wa kutosha. Akiwa amefanikiwa kuitetea serikali kwa mafanikio makubwa katika kesi mbalimbali, mfano; mtikila, pinda, na nk.
Najua wengi wetu (nikiwemo na mimi) hatukupenda matokeo ya kesi ya mtikila, na pinda (wapigwe tu), lakini ukiwa mwanasheria kazi yako kubwa ni kutetea maslahi ya mteja wako, na kwa upande wa Ndugu Masaju, ni serikali.
2. Ndugu Masaju amekulia na kulelewa ktk ofisi ya mwanasheria mkuu, hivyo anaijua vyema na itakuwa ni rahisi kwake kuifanyia mapinduzi ya kutosha. Tofauti kama angeteuliwa "outsider", yaani nje ya ofisi ya mwanasheria mkuu, angekuwa na kazi kubwa; kwanza, kujenga mahusiano na aliowakuta; pili, kuelewa utendajikazi wa ofisi ya AG na kuzoea kazi ambayo hakuwahi kuifanya.
3. Tuliofanikiwa kusoma report ya CAG, na PAC kuhusu escrow account, na kwa huo mchezo mchafu ulivyochezwa kwa usiri na ukihusisha AG ni wazi kabisa Ndugu Masaju asingeweza kujua kinachoendelea, ukizingatia waliohusika walijua kuwa ni msabato!
4. Ni utumaduni mzuri wa kupandisha vyeo watu walioitumikia serikali kwa uadilifu mkubwa. Utamaduni huu hujenga hamasa wa kujituma miongoni mwa wafanyakazi wa serikali. Ni vibaya sana, na inaua moyo wa kujituma, hasa unaposikia Judge au Professor kawa AG au wakili kawa Judge huku kuna mamia ya Mahakimu na state attorneys waaminifu.

Asante wana JF!

Kweli ana uwezo, kama anaweza kumshauri bosi wake aseme hela za escrow sio za umma ana uwezo. Kama bunge lina azimia waziri aachie ngazi bado rais anamuacha na anaendelea na uteuzi wa wajumbe kweli ana uwezo.
 
Yalaaa ndo nini hiki. Tobaaa. Ngoja nikemee pepo tokaaa.
 
Maskini JK.Anajitahidi sana kuteua na kuwabebesha Biblia na Quran kuapa na anaangukia pua. Aisee JK polr, Utawala wako umekuwa kama umelaaniwa....
 
Wana JF, heri ya Mwaka Mpya na wa Mageuzi 2015.

Kuteuliwa kwa ndg. George Mcheche Masaju kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ni mwendelezo wa ombwe la utawala kulindana hasa kwenye sula la Escrow account.

Wakati Mwanasheria mkuu mpya alikuwa msaidizi wa Werema, jamaa huyu pia anatoka mkoa mmoja na Werema.

Mchezo mzima wa Escrow ulichezwa na Werema na kama alivo andika kwenye barua yake ya kujiuzuulu kwa mhe. Raisi, alisema anajiuzulu -kwa sababu ushauri wake " ulichafua hali ya hewa"... Wote tunajua jinsi serikali inavo fanya kazi. Kuchotwa kwa pesa za Escrow kulikuwa na mawasiliano mengi sana ya barua ndani ya ofisi ya AG, hakuna uwezekano kwamba bwana Masaju hakuwa na habari jinsi mchezo mzima ulivo chezwa. Pia ikumbukwe huyu alikuwa ni msaidizi wa Werema, katoka nae mkoa wa Mara na kuna wakati werema alikuwa anamwachia ofisi akaimu wakati yeye anapo kuwa likizo au amesafiri. Kwa kifupi Masaju ni mwendelezo wa Werema kwenye ofisi ya AG.

Gazeti la Tanzania Daima jumapili la leo katika ukurasa wake wa 5 chini ya kichwa cha habari " ikulu imetudhalikisha", mbunge mmoja wa CCM amesema, kwa bahati mbaya bodi mpya ya Tanesco iliyo chaguliwa na Mh.Prof. Muhongo, nusu ya wajumbe wa bodi ni kutoka mkoa wa Mara. Wakati bodi hii ndo yenye kazi kubwa katika msitakabali wa Tanesco, Muhongo anae tuhumiwa kwa wizi, ameteua wajumbe nusu toka mkoani mwake ili waweze safisha hali ya hewa.-

Uteuzi wowote wa AG kutoka nje ya mfumo ulio kuwepo ingeweza chafua hali ya hewa zaidi na Muhongo kaisha iweka Bodi ya Tanesco sawa kwa kuchagua watu wa mkoa wake.

" ukiona manyota jua......"

My take: ni wakati muafaka sasa tuwe na katiba inayo mbana mh. Raisi asiteue tu wa
 
My take: ni wakati muafaka sasa tuwe na katiba inayo mbana mh. Raisi asiteue tu watu anao wataka katika nafasi muhim za kitaifa mpaka wapitishwe na bunge-
 
Napita tu ila acha mambo ya ukanda, hivi hao nusu wa kutoka mkoa wa mara sio wa tz, hata kama wangekuwa wote wanatoka mkoa wa Mara hakuna tatizo mradi tu kama wanaweza fanya kazi kwa ari
 
Watasema Kikwete mdini!haya wagalatia anzeni kutoa kasoro na kashfa!uzuri ni kuwa tumeshawazoea

ule mkwara aliochimbwa humu JF umesaidia la sivyo kweli angempa hiyo nafasi mwalimu wa riz prof ibrahim juma...maana jamaa sometime huwa hana aibu..
 
Ungefanya vp kwani kama ingetokea hivyo zaidi ya kulialia tu na mambo yangeendelea kama kawaida
 
Hivi si kwamba ushauri wa Werema uliochafua hali ya hewa uliandaliwa na George Masanju na kusainiwa na Werema?

Maana yangu ni kwamba, mara nyingi mabosi huwa wanagawa kazi kwa wasaidizi wao, na Bosi mara nyingi ni kusaini tu? Isijekuwa aliyechafua hali ya hewa ni George!
 
Back
Top Bottom