Tatizo pia ni sisi.Kwa mfano huu mtazamo kuwa kuteuliwa kwake maana yake "Kaula" ni lini utatutoka?
mkuu ben,chukua like ''1000'' za mdomo,maana hapa natumia simu. Hakuna jambo linalonisikitisha kama kusikia kauli hii ya ''kaula''. hivi mtu anayeteuliwa katika nafasi fulani ya kiuongozi au mamlaka ya umma,inakuwaje awe ''ameula'' na si amebebeshwa msalaba mzito!!!???
Kuula huko maana yake ni kutumia STK kumpeleka mtoto shuleni, kumpeleka ''housegirl'' sokoni,kumpeleka mama vicobani, kwenda kuchukua vyakula vya mifugo,n.k pamoja na kuiba mali za uma na si mzigo mzito wa kuwatumikia watanzania na kuwaletea maendeleo!!!????
kama kweli tunataka hawa watumishi wa umma (wawe wateuliwa ama la) watekeleze majukumu yao ipasavyo na kutuletea maendeleo,basi sisi watanzania kwa ujumla (kaka,dada,mama,baba,babu,bibi,shangazi,mjomba,binamu,mpwa,shemeji,mkwe,mkamwana) wa mteuliwa/mchaguliwa/muajiriwa, tuache na kukemea kabisa tabia ya kutegemea manufaa kwa wale ndugu zetu wanaopata nafasi katika uongozi ama ajira.