Rais Kikwete amteua Prof. Mussa Assad kuwa CAG mpya akimrithi Ludovic Utoh

Assad yuko vizuri.

Ndo na mimi niende huko kwa CAG rasmi sasa.
 
Mimi si mdini lakini........mhuuuu...!!!?
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu wa Wizara kwa kuteua Makatibu Wakuu wanne wapya na kuhamisha mmoja.
Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa.
Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba 5, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa walioteuliwa kuwa Makatibu Wakuu ni Dkt. Donan Mmbando ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Yohana Budeba ambaye anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Mbogo Futakamba kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Dkt. Adelhelm James Meru ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Maliasili.
Kabla ya uteuzi wake, Dkt Mmbando alikuwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Budeba alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mifugo, Mhandisi Futakamba alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Dkt. Meru alikuwa Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA).
Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Rais Kikwete amemhamisha Bibi Maimuna Tarishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria
Kuhusu uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa, Rais Kikwete amemteua Bw. Charles Pallangyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Bw. Adoh Steven Mapunda, Mkurugenzi Mtendaji, Manispaa ya Bukoba kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Severine Kahitwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro na Dkt. Faisal Issa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Kanali (Mst) Joseph Simbakalia, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa EPZA.
Uteuzi huo unaanza leo na Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wataapishwa kesho, Alhamisi, Novemba 6, 2014, Ikulu, Dar es Salaam.
 
Kwani Rais atakaechaguliwa analazimika kuendelea kuwatumia atakao wakuta si anaweza kuteua anaoona wanamfaa kwa manufaa ya nchi sio uongozi alioupokea!
Sio kwamba ukishachagua cag umechagua mpaka asitaafu au afe?
 
Kwani Rais atakaechaguliwa analazimika kuendelea kuwatumia atakao wakuta si anaweza kuteua anaoona wanamfaa kwa manufaa ya nchi sio uongozi alioupokea!

Kutengua uteuzi wa watu kama hao siyo rahisi ..................... hiyo ni kampuni ya serikali!! They are on contracts!!
 
Rais kikwete leo amemteua prof,Mussa J Assada kuwa mthibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali(CAG),ATAAPISHWA KESHO.Yamkini ndio jitahada zake za kujibu mapendekezo ya bunge lilimalizika mwishoni mwa wiki lilipita

Chanzo;ikulu

Hivi kumbe uteuzi wa CAG ulikua miongoni mwa maazimio ya bunge siyo?
 
kweli kabisa mkuu, ma professor wengi ni janga katika kazi za serikali, labda wanafanya vema katika taasisi binafsi.
Mfano :Nani alitegemea kwa CV aliyokuwa Mh. Prof. muhongo , PROFESSOR anna Tibaijuka, PROFESSOR Maghembe, PROFESSOR @Msola , nani alitegemea kuwa watakuja kufanya madudu namna hii.
Kuna mtu alikuwa na CV safi na yenye kuvutia kama Mh. Nundu? peruzi CV yake utaona, ila mwisho wa siku ni aibu tupu.

Umemsahau Professor Kapuya hapo!
 
Last edited by a moderator:
kwann asinge mwacha huyo aliyekuwa anakaim ili ampromoti au ameweka kama kumkomoa rwakapalila? mbona kasubiri hadi maamuzi ya bunge yafanyike?

Kwanini unawaza negative tu?
Kwa nini amkomoe Huyo rwakapalila?
Ni mapema sana kutathmin.
 
Kutengua uteuzi wa watu kama hao siyo rahisi ..................... hiyo ni kampuni ya serikali!! They are on contracts!!

Una maana wana mamlaka ya kuteua tu sio kutengua uteuzi wanaoufanya?
 
Hata Professor Mark Mwandoswa naye ni mzigo tu ndio maana kapewa wizara isiyokua maalum!

Jamaa anamgwaya Mwandosya yupo smart ndomana anambania na alimteua baana ya kuona watu watampigia kelele, hata Magufuli alimbania akampa Wizara ya kijinga lakini jaamaa akaenda kudaka Meli, kaamua kumrudisha Miundombinu baada ya maswahiba wake wote kuwa wanamwangusha baada ya kuwapa wizara za ukweli. Alianzaga na Mawaziri 60 wakati 60% ya bajet tunategemea wahisani, me cjasoma bt cwez fanya ujinga huo. Mkapa aliacha nchi ina pesa balaa lakini jamaa anaondoka nchi anadaiwa mbaya. Me cjawahi ona viongoz wa namna hii jaman
 
Hv kuapishwa kuna maana tena? Hata wakishika vitabu ishirini kwa wakati mmoja. Ni bure
 
Una maana wana mamlaka ya kuteua tu sio kutengua uteuzi wanaoufanya?

Siyo kuwa hawezi ila kuna implications zake .......................It's a political game!! Teuzi nyingi za mwishoni huwa ni za kulinda maslahi zaidi. Huo mchezo hata US unachezwa kihivyo between Repulican na Democrat!! Majaji wa Republican ndiyo waliomsave Bush 2000 kama unakumbuka!! Anyway, as long as CCM still in power nothing much will change ...... that's why we need a game changer in Tanzanian politics!!
 
Hivi ni yule Jamaa alikua anafundisha na projector UD?

Kama ni Yeye jamaa n Jembe balaa.
 
Kikwete anatengeneza zengwe kuhusu suala la escrow. The new cag will clarify that,escrow money is clean and legit.

Haha thanks baba rizone. Very smart!!
 
annabrenda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu wa Wizara kwa kuteua Makatibu Wakuu wanne wapya na kuhamisha mmoja.
Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa.
Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba 5, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa walioteuliwa kuwa Makatibu Wakuu ni Dkt. Donan Mmbando ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Yohana Budeba ambaye anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Mbogo Futakamba kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Dkt. Adelhelm James Meru ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Maliasili.
Kabla ya uteuzi wake, Dkt Mmbando alikuwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Budeba alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mifugo, Mhandisi Futakamba alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Dkt. Meru alikuwa Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA).
Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Rais Kikwete amemhamisha Bibi Maimuna Tarishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria
Kuhusu uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa, Rais Kikwete amemteua Bw. Charles Pallangyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Bw. Adoh Steven Mapunda, Mkurugenzi Mtendaji, Manispaa ya Bukoba kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Severine Kahitwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro na Dkt. Faisal Issa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Kanali (Mst) Joseph Simbakalia, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa EPZA.
Uteuzi huo unaanza leo na Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wataapishwa kesho, Alhamisi, Novemba 6, 2014, Ikulu, Dar es Salaam.
 
Last edited by a moderator:
hii cv hata frank wood haifikii,swali ni je,unaweza kubishana na aliyekuteua ukiona madudu yake?hapa ndipo katiba ya warioba inapotakiwa.
 
Back
Top Bottom