Rais Kikwete amteua Prof. Mussa Assad kuwa CAG mpya akimrithi Ludovic Utoh

Rais Kikwete amteua Prof. Mussa Assad kuwa CAG mpya akimrithi Ludovic Utoh

Assad namkubali Mwalimu wangu pale UDBS.....enzi za mwaka 2010
 
Inaonekana atastaafu mwakani kabla hata raisi hajamaliza muda wake, JK ni noma kwa fadhila. Namkemea anayeendekeza mambo ya udini kwa nguvu zangu zote

Really? Hivi udini maana yake ni nini haswa? Tuseme Waislam hawapaswi kuteuliwa japo kama wana sifa za kutosha?. Haya lete comparison yako na Prof Assad kwenye accounting and auditing field. Halafu uteuzi wa Assad unatofautiana vipi na ule wa Utouh?
Let you talk sense. Prof Assad ana deserve hiyo position labda tu haderserve kwa sababu ni Mwislam. Lakini tukienda kwa mwenendo huu ndugu mmmm sidhani kama tuna mwisho mwema.
 
Mkuu Uttoh hakupigwa chini, muda wake wa kustaafu kisheria ulifika.

Kwa nnavyoijua mimi hii serikali sometimes hata kama muda wako wa kustaafu haujafika utafikishwa na wakikukubali kwa maslahi yao hata kama muda wako umefika hautostafu mpaka watake wao.
 
Historia inaonyesha Maprofessor hawadumu sana katika nafasi za uongozi. They don't make good leaders in Tanzania. Mfano:
- Prof Machunda
- Prof Kapuya
- Prof Meena (Mb)
- Prof Msola
- Prof Muhongo
Endelea
-
-
-
Professor Kikwete..

Ila duh...hii picha jamaa ana fanana na Ben...
 
Mim si mdini ila for the records hawa hapa:

1. CAG
2. Commissioner General TRA
3.Director General TPA

Ingekuwa hawa wote ni wakristu wameteuliwa kungekuwa na hata this discussion hapa na need ya "kuweka for the record" au kwa kuwa ni waislam ndo kimeuma? Maana akiteuliwa John sawa hakuna anaye raise eyebrow ila akiteuliwa Juma sasa u start counting. Miaka yote hiyo ya nyuma serikali ilivyokuwa na kina george, john nk mbona hamkuweka "for the record"?! Wakati wa Mkapa kina John walikuwa wangpi kwenye hizo nyadhifa na zinazofanania hebu tupe "for our records" tafadhali...
 
daaah huyu jamaa kanifundisha AC100 udsm 2006/2007..yuko vizuri na alikua anaiponda serikali mno...
 
Hongera kwa Prof Assad you deserve it. Hongera kwako na kwa familia yako, mkeo Bevalyn mamy hongereni sana. Kwa wale wanaochukia uteuzi wa huyu jamaa simply because he is a muslim imekula kwenu nachukua nafasi hii kusema thats sheer nonsense the guy totally deserves it. Haya kama kimeuma kakojoe ukalale upumzike. Mfyuuuuu!
 
kwa kweli nimekatishwa tamaa.hilo ni changa la macho sisi kama wananchi tunataka atengue mara moja waziri wa nishati mh.muhongo,AG na wangine walo husika na escrow.tujiulizeni hapa,WHY CAG?ndo yeye aliyeiba ama ndo aliyesaidia kufichua maovu?hili ni changa la macho kwa watanzania.hukumu imetoka kwa asiye husika,kww taarifa zilizopo ni kwamba ameteuliwa assad ili achunguze mchakato wa escrow na atoe majibu yayayoonesha kwamba hela ile haikuchukuliwa na sio ya umma pia inasemekana cag ndo aliyetoboa siri juu ya kashfa hii ya escrow ndo maana ameondolewa mara moja kama ni adhabu na inasemekana kwamba hakuna azimio lililopitishwa na bunge ambalo mh.raisi atalikubali ndo maana amefanya maamuzi ambayo hatukuyatarajia wananchi,jee hii ni haki kweli,mwizi amesamehewa aliyekamata wizi ndo aliye hukumiwa.tutakua nawe cag daima.
 
Hongera Prof. Musa Juma Assad. Chapa kazi kama alivyo kuwa mtangulizi wako Utoh! Usimwamini kabisa JK na genge lake,waweza kukuingiza chaka muda wowote.
 
kwann asinge mwacha huyo aliyekuwa anakaim ili ampromoti au ameweka kama kumkomoa rwakapalila? mbona kasubiri hadi maamuzi ya bunge yafanyike?
 
Lazima wapewe watu watakaoweza kulinda maslahi baada ya awamu .........................!! Anyway, sidhani kama ana CV kumshinda huyu bwana!!

Kwani Rais atakaechaguliwa analazimika kuendelea kuwatumia atakao wakuta si anaweza kuteua anaoona wanamfaa kwa manufaa ya nchi sio uongozi alioupokea!
 
Haya uteuzi umeanza tunataka kusikia na wale wengine wa Bungeni waliopitishiwa maazimio tutakuwa tunakukumbushia hata kama uko maumziko ya ugonjwa.
mkuu, wale watapangiwa kazi nyingine na mh. Rais, kwa sasa wameachiwa kamuda kakukusanya chochote wanachohisi wanaweza kuondoka nacho kwenye nafasi zao.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Mussa Juma Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Desemba Mosi, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa Bwana Assad ulianza Novemba 5, mwaka huu, 2014.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bwana Assad ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 2, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Assad alikuwa Profesa Mshiriki, Idara ya Uhasibu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Bwana Ludovick Utouh ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma.
Profesa Assad ni msomi, mwenye weledi, ujuzi na uzoefu mkubwa wa uhasibu na udhibiti wa fedha ambaye ana Shahada ya Uzamivu wa Uhasibu (PHD in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Southampton, Uingereza mwaka 2001 na Shahada ya Uzamivu katika Udhibiti wa Fedha (MA in Financial Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City, Jamhuri ya Ireland mwaka 1991.
Profesa Assad pia ana Stashahada ya Kitaaluma ya Uhasibu (Professional Diploma in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City mwaka 1990 na Shahada ya Biashara (Bachelor of Commerce) ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam mwaka 1988.
Pamoja na uzoefu wa kitaaluma, Profesa Assad anao uzoefu mkubwa katika eneo la uhasibu na ukaguzi. Alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) kwa miaka saba (2007 - 2014); ni Rais na Mjumbe wa Chama cha Wahasibu Afrika (Pan African Federation of Accountants) tangu mwaka 2012; na ni mjumbe wa Bodi kadhaa za Wakurugenzi nchini Tanzania.
Katika kumteua Profesa Mussa Juma ASSAD kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Rais anayo imani kubwa kuwa elimu, weledi, ujuzi na uzoefu ambao Profesa Assad anao utamwezesha kutekeleza vema majukumu ya nafasi hiyo muhimu sana katika utawala bora wa nchi yetu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
 

Attachments

  • IKULULEO.jpg
    IKULULEO.jpg
    22.3 KB · Views: 209
Back
Top Bottom